mizambwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2008
- 4,422
- 1,791
Wakuu, naandika haya nikiwa na masikitiko makubwa sana:
Serikali imetutangazia kuwa itatoa Elimu bure kwa wanafunzi wote kuanzia darasa la kwanza hadi Kidato cha nne. Kwa muda mfupi toka muhula mpya wa masomo kwa shule za msingi na sekondari tayari kumekuwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo ufinyu wa pesa za kugharamia Elimu bure.
Kwa mkoa wa DSm kuna shule za msingi ambazo wamepewa Tsh. 1,500,000/= ( Tsh. Milioni moja na laki Tano Tu) pesa ambayo imewekwa katika mgawanyo wa kiasilimia. mfano 30% kwa ajili ya miundombinu ya kufundishia (450,000/=), 10% kwa ajili ya mitihani na majaribio darasani (150,000/=), 10% kwa ajili ya utawala (150,000/=) nk.
Yaani kwa ujumla ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na jumla ya wanafunzi waliopo katika shule husika. mfano shule ina wanafunzi jumla 2,600 kwa hiyo Tsh. 150,000/= ina maana kila mwanafunzi ametengewa Tsh. 58.00 ( Tsh. Hamsini na nane tu) je, hatuoni kama tunampa mwalimu mzigo mkubwa katika kugharamia majaribio na mitihani kwa kila mwanafunzi?????
OMBI: SERIKALI WANAPASWA KULIANGALIA UPYA SUALA LA ELIMU BURE VINGINEVYO WATAUA KIWANGO CHA ELIMU TANZANIA.
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!