Serikali na NSSF waoneeni huruma walimu

Mnyalu Junior

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
573
199
Walimu ni moja ya watumishi nyeti hapa nchini. Siyo tu kwa uwingi wao ukilinganisha na watumishi wa sekta nyingine bali ni matunda yanayopatikana kutokana na wao. Hii ni kwasababu walimu ndio waandaaji wa wataalamu wa fani zote kama vile; udaktari, sheria, uhasibu, uhandisi n.k.

Straight to the point;

Walimu wanapoajiriwa hutakiwa kujiunga na mojawapo ya mifuko ya hifadhi ya jamii. Mifuko hii ya jamii ndiyo huhifadhi fedha za mwanachama (mafao) na baadaye kuja kumpa pindi atakapostaafu. Kuna mifuko mingi ya jamii ambayo mwalimu huchagua kujiunga nayo km vile: NSSF, PSPF, LAPF na PPF. Sheria ya mifuko hiyo ya jamii ni kwamba kila mwezi mtumishi aliyejiunga atatakiwa kuchangia kiasi cha asilimia ishirini (20%) kulingana na kiasi cha mshahara wake kwa kila mwezi.

Mgawanyo wa uchangiaji kwa walimu:

Kwa walimu walioajiriwa na serikali mgawanyo wa uchangiaji katika hizo asilimia ishirini (20%) zinazopaswa kuchangiwa kila mwezi kwa mfuko husika ni kwamba; Mwalimu atachangia asilimia tano (5%) ya mshahara wake anaoupata kwa mwezi na Serikali ambayo ndio mwajiri wake itamchangia asilimia kumi na tano (15%).

Tatizo limekuja hususani kwa walimu walioajiriwa mwaka jana na wakajiunga na mfuko wa jamii wa NSSF. Badala ya kukatwa 5% kwenye mshahara kwa kila mwezi wanakatwa 10%! Inauma sana kwasababu mimi mwenyewe ni mhanga na hadi najuta kwanini nilijiunga na NSSF na kuacha mifuko mingine. Nilifanikiwa kufika hadi makao makuu yao hapa Dar es salaam pale jengo la Benjamin Mkapa Pension Tower lililopo posta. Niliambiwa tatizo hili ni la nchi nzima hivyo watalishughulikia. Niliambiwa pia niende kwenye ofisi zao zilizopo Water Front pale kivukoni nikutane na wahusika rasmi wanaohusika na kuunganisha mishahara ya watumishi na mfuko wa NSSF.

Majibu niliyopata yalinikatisha kabisa tamaa! Niliambiwa mfuko kama mfuko hauhusiki na kukata michango ya wanachama bali SERIKALI ambayo ndiyo mwajiri wangu ndiyo inayokata hizo 10% badala ya 5%. Aliendelea kueleza kwamba wao km mfuko wa hifadhi ya jamii hiyo michango ya wanachama wanapelekewa tu na serikali hivyo nisiwatuhumu wao niituhumu serikali ambayo ndiyo imeniajiri! Inasikitisha sana kwani hili tatizo la kukatwa 10% lipo nchi nzima hususani kwa walimu wote walioajiriwa mwaka jana.

My take;

Hivi serikali kwanini imeamua kuwaonea walimu waliojiunga na NSSF kwa kuwachangia 10% pekee badala ya 15% na hivyo kumpa mzigo mfanyakazi kuchangia 10%? Mbona walimu waliojiunga na mifuko mingine kama vile LAPF na PSPF wanachangia 5% pekee na serikali bila hiyana inawachangia 15%? Au ni moja ya ufisadi unaoitafuna NSSF ambao baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti? Serikali na NSSF tuelezeni walimu kuna nini nyuma ya pazia juu ya suala hili?

Nawasilisha wadau
 
Kiongozi kabla ya kujiunga ulikuwa na option ya kujiunga mifuko mingine. Na suala la kuchangia 10% kwa NSSF lipp hata kwenye vipeperushi vyao ulitakuwa kulijua hili kabla hujajiunga. Sio kweli kuwa mifuko yote inakata 5%, NSSF wao wanakata 10%, so, you should have known this before u made your decision to join them. I'm a victim of this swindling NSSF too and my friend do not think that things will change for you to go there and complain, it's their policy! Nkt!
 
Wewe uliingia chaka!!! Mfuko spesheli kwa watumishi wa umma ni LAPF au PSPF tatizo mlidanganyika na vi t-shirts na kofia mnazohongwa wakati wausajili now mnajuta!!!
 
NSSF iliwekwa kwa ajili ya sekta binafsi?? hivyo kutoksna na siasa, wakaruhusu hadi watumish wa umma kujiunga nsyo, hivyoo inaonekana sheria yao ya mafao hawajabadilisha, kwan sekta binafsi wanachangia hyo 10%. pole ssna, but kiukweli itachukua muda mrefu kubadilishiwa na kujitoa huwez.
 
Mwalimu aliekurupuka kujiunga na mfuko wa Penshen bila ya kusoma Masharti. Kama Mwalimu ni Mvivu wa kusoma hata kipeperushi sijui wanafunzi wake wakoje?
 
Ignorance has no excuses

Ndio tatizo la watanzania kufanya vitu bila kufata taratibu zinazotakiwa.

Sasa kama wewe mwalimu unashindwa kujua icho mwanafunzi atajua nini..shame on you.
 
Back
Top Bottom