Serikali na mikataba 1000 ya umeme

mseseve

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
511
89
WAKUU KABLA YA YOTE NAOMBA NINI MAANA YA CONTRACT/ MKATABA kwa sababu nimeshindwa kabisa kushangaa hii mikataba ya kuzalisha UMEME inayosiniwa kila siku na kila mwaka na serikali yetu ilioko madarakani ni lini itakamilika na tujulishwe kwamba mradi wa mwaka fulani tuliosaini na kampuni fulani umekamilika na utakabidhiwa serikalini! jana kama sikosei serkali imesaini tena mkataba na kampuni ya kichina wa kuchimba makaa ya mawe na pia kuzalisha chuma na UMEME wa megawat 600.

SERIKALI... Ni mikataba mingapi ilokwishasaini ya umeme na hakuna kilichofanyika?au hii mikataba inakua ni ZUGA adui? ili wananchi waone serikali iko kazini kikamilifu... mimi nimechoka kusikia kila siku waziri fulani kasaini kwa ajili ya maswala ya umeme, ni miaka mingapi tunasikia mikataba inasainiwa ya umeme na hatuoni mabadiliko yoyote aliyotokea kwenye secta ya umeme?

Bora wafanye mambo yao kimya kimya tisijue kabisa kuliko kusikia madudu yao ya kutufariji na kisha hakuna jipya litendekalo. TUMECHOKA na NTAVUNJA UKIMYA sasa hivi..........
 
Back
Top Bottom