Serikali na mifuko ya hifadhi ya jamii

Serikali na mifuko ya hifadhi ya jamii

Marco Polo

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
13,433
Reaction score
21,447
Vijana wana hali ngumu, pesa zetu wamezikalia, mtu anafanya kazi labda miaka 5 akitegemea awekeze ili aje apate mtaji afanye shughuli zake Leo hii anafukuzwa kazi mnamwambia pesa zako mpaka miaka 55 , hii sio haki .....Kwa namna hii Tanzania ya viwanda itatoka wapi huku mitaji ya vijana mumeizuia?

Nimeandika haya yote baada ya kuona ITV Leo Dada wa watu akitokwa na machozi kuhangaikia jasho lake, na sio yeye tu kuna vijana wengi sana huku mitaani wanataabika sana.

Serikali naiomba iangalie njia nyingine nzur ya kutatua changamoto hii tafadhali.
 
Pesa za mafao ya uzeeni ni zamafao ya uzeeni, si za kudokoa dokoa kila unapokosa kazi.

Walioanzisha hizo habari, tuliowageza, wana mifumo ambayo hizo fedha zinafungiwa mpaka ufikishe miakahusika, na kuzipata kabla nikwa kukopa ukifikiwa na hali ngumusana, tena kwa penalty kubwa sana.

Mimi tatizo langu si kwamba wanazifungiampaka ufike miaka 55.

Tatizo langu ni pale wanapoanza kuzitumia katika miradi yao ya ajabu ajabu bila hata kujua zitarudije.
 
Kwa hili tumuombee kaka mkuu wa nchi T.A.L apone upesi uje kutupambania.
 
Hela ni yako, ili upewe utafikiri unaomba mikopo Benki???

Hatari sana, tusipoangalia usalama wa pesa zetu kwa kuzingatia kuwa kuna vijana wanafukuzwa kazi kabla ya mda wao.

Kamwe nchi ya viwanda kufika itakuwa vikwazo.

Hela ya mtu ni muhimu apewe sio kuzungushwa utafikiri anataka mkopo???
 
Pesa za mafao ya uzeeni ni zamafao ya uzeeni, si za kudokoa dokoa kila unapokosa kazi.

Walioanzisha hizo habari, tuliowageza, wana mifumo ambayo hizo fedha zinafungiwa mpaka ufikishe miakahusika, na kuzipata kabla nikwa kukopa ukifikiwa na hali ngumusana, tena kwa penalty kubwa sana.

Mimi tatizo langu si kwamba wanazifungiampaka ufike miaka 55.

Tatizo langu ni pale wanapoanza kuzitumia katika miradi yao ya ajabu ajabu bila hata kujua zitarudije.
Vipi fao la kutokua na ajira? Kama wanazuia watoe hilo fao "Unemployment benefits ".....Ni uuaji kusema mtu achukue fao la kujitoa baada ya miaka 55.
 
Vipi fao la kutokua na ajira? Kama wanazuia watoe hilo fao "Unemployment benefits ".....Ni uuaji kusema mtu achukue fao la kujitoa baada ya miaka 55.
Serikali inatakiwa kuwa na unemployment benefit kutoa relief kwa angalau miezi sita mtu anapotolewa katika kazi moja bila makosa, na anapokuwa anatafuta kazi nyingine.

Tusichanganye mambo na kutaka kutumia mafao ya uzeeni kama unemployment benefit.

Tutafika uzeeni bila mafao ya uzeeni halafu dhana nzima ya kuwa na mafao ya uzeeni ipoteze maana.
 
Back
Top Bottom