serikali na magari ya kifahari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

serikali na magari ya kifahari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ulimboka, Oct 27, 2009.

 1. ulimboka

  ulimboka Member

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 23, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina kumbukumbu kuwa waziri mkuu alionyesha uwezekano wa viongozi wa ngazi za juu serikalini kupunguza matumizi ya magari ya kifahari. Nazidi kujiuliza ni nani hasa anayeweza kutoa amri hiyo na watu wakatekeleza maana nimesikia tetesi kuwa yamenunuliwa tena.
  Hapo kwa jirani zetu kenya tunashuhudia gari aina ya Passat zikiwa tayari kwa kuwakabidhi viongozi wa ngazi za juu baada ya kurejesha yale ya kifahari. Inasemekana passat hizo zitaokoa zaidi ya nusu ya gharama za matumizi. Hivi hatuwezi kujifunza hata kwa mifano au tunaogopa kuiga? Na unajifunzaje bila kuiga? Hasa kwa mambo yenye faida?
  Wadau mnaonaje siasa hizi au hadi tume iundwe kutafakari wazo ambalo kiongozi wa serikali ameliona! Nashindwa kupata jibu la nani anayeweza kufanya maamuzi haya!
  Karibuni!
   
 2. s

  skasuku Senior Member

  #2
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ulimboka... hapo mimi nadhani mwenye uwezo waku amuru ni Rais au Waziri Mkuu. Utakumbuka wakati wa hayati Sokoine yeye alipotoa amri ya kukamata wahujumu uchumi alianza kwa kuonyesha kwa mfano pale alipo toa stock take ya mali zaki... na kuamuru walio chini yake kufanya pia.. pale alimuacha mkuu wa nchi pekee.

  So.. yoyote kati ya JK au MP atakapo pata ujasiri ataweza fanya kweli... ila usisubiri hilo kwani wote ni pumba.. kelele kibao hakuna vitendo.
   
 3. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Pinda alisema wanasubiri kufikisha suala hili bungeni katika kikao cha November ili liwe na nguvu ya kisheria. Sasa sijui kuna sheria gani iliagiza kwamba magari ya serikali yawe mashangingi tu ?! Kama kawaida, usitegemee jipya.
   
Loading...