mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,208
- 1,109
Ninapongeza kwa dhati juhudi kubwa za kukomboa wananchi toka katika lindi la umaskini,maladhi,ufukara,shida na tabu.Napongeza utendaji wa kasi wa serikali ya awamu ya tano katika kurejesha nidhamu ya juu/maadiri na uwajibikaji katika utumishi wa umma.Nina kila sababu ya kushiriki kuiunga Mkono serikali sikivu na yenye uzalendo wa kweli chini ya His Excellency JPM,PM {MKM}..
Kwa unyenyekevu mkubwa nawakirisha hili ili hekima itumike kuendelea kulijenga taifa letu kwa kuokoa ajira,mapato,na kuepuka kukimbiza baadhi ya wawekezaji ambao ni chachu kwa tulio wengi kuifinyanga Tanzania mpya ya viwanda vikubwa vya vyenye kukidhi mahitaji ya wananchi wetu katika nyanja mtambuka hivyo kuepuka uagizaji usio na tija ktk uchumi kama toothpick,karatasi,furniture,stapler pins,matairi,vipuri,nguo,n.k.
Kuna kampuni ya kimataifa {toka thailand yenye viwanda takribani 15 katika nchi mbalimbali Duniani} iliowekeza katika utengenezaji wa chakula cha kuku/mifugo takribani miaka 3 hapa nchini..Kiwanda cha kampuni hii kipo maeneo ya chang'ombe,jirani na kiwanda cha konyagi.Kiwanda hiki kimeajiri zaidi ya watanzania 50 wenye elimu ya juu na kati wakiwemo {Mechanical engineers,chemical engineers,Food engineers,etc etc},Kiwanda hiki ni mnunuaji mzuri wa nishati ya umeme;malighafi mbalimbali za kilimo {mafuta ya alizeti,mahindi,madawa,pembejeo,] hivyo kuchangia kwa namna moja ukuaji wa uchumi wetu,pato la taifa hata kwa kiwango kidogo.
Kiwanda hiki kimesimamisha na kufunga uzalishaji kwa zaidi ya miezi miwili sasa na kwa sasa wapo katika mchakato wa kuuza mitambo yao yenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni tatu {3} sababu kubwa ni kodi ya VAT {Value Added Tax} katika bidhaa zinazozalishwa..Kilio cha wawekezaji hawa ni soko kuwa dogo na linalobembelezwa kukua ili kukidhi mapana ya uwekezaji katika sekta ya ufugaji..VAT inafanya bidhaa kuwa na bei kubwa ukilinganisha na bidhaa zinazoagizwa toka katika mataifa yasiochaji VAT.
Kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu ,wakati huo huo ni ngumu sana kutenganisha kilimo na mifugo katika muktadha wa maendeleo ya taifa letu tukufu..Ufugaji umekuwa ukifanywa kwa miaka nenda rudi na kaya za kipato cha chini,kati na juu..Ufugaji wa kisasa umekuwa chachu ya wafugaji kukidhi soko la bidhaa za ufugaji kama maziwa,mayai,nyama,asali,n.k.
Nina amini kwa dhati kabisa serikali yetu italifuatilia hili,pata taarifa za kina na kulipatia ufumbuzi makini kwa manufaa mapana ya taifa letu sasa na baadae kwani Mh. Rais wetu na serikali ni wasikivu sana,wenye ufahamu mkubwa sana,wenye hekima sana,na busara nyingi.
Mungu Ibariki Afrika,Mungu Ibariki Tanzania bara na Tanzania Visiwani {Zanzibar}.
CC:Wizara Ya Kilimo na Mifugo
CC:Wizara ya Viwanda na Biashara
CC:TIC