Serikali mpya ya chuo kikuu yakwamishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali mpya ya chuo kikuu yakwamishwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 14, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MGOGORO wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (Daruso) umeendelea kuvuta kasi baada ya Utawala Chuoni hapo kuingilia kati na kuunda kamati ya watu watatu itakayofanya kazi ya kusikiliza madai ya pande zote mbili, zinazopingana na kutoa tamko la kuitambua serikali mpya au la.

  Hatu hiyo, imekuja baada ya Serikali ya mpito kukamilisha kazi ya kuunda serikali, lakini ilipokwenda kuitambulisha ikakutana na kikwazo hicho cha kusubiri tamko la kamati hiyo, baada ya kufanyika kwa uchunguzi.

  Spika wa Bunge hilo. Goodluck Mwangomango alilimbia Mwananchi jana kuwa rais wa muda Milinde Mhano na Waziri Mkuu, Kassim Warioba walikamilisha kazi ya kuunda serikali, lakini hajatambuliwa na wanasubiri tamko la kamati hiyo.

  “Tayari rais wa serikali ya muda ameshaunda serikali, lakini imeshindwa kutambulishwa kutokana na utawala chuoni hapa kuunda kamati ya watu watatu watakaosikiliza pande zote na kutoa tamko jumamosi wiki hii,”alisema Mwangomango.

  Wakati Mwangomango akitoa kauli hiyo, serikali iliyoondolewa madarakani imeendelea na msimamo wa kupinga maamuzi hayo kwa madai kuwa yalikiuka taratibu.

  Waziri Mkuu wa serikali hiyo ya zamani Paul Makul alisema wao kama watendaji bado wapo ofisini na wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na kamati hiyo, ingawa wanashishikilia msimamo kuwa maamuzi hayo yalikiuka katiba .

  “Kikao kiliendeshwa nje ya muda wa vikao na ni kinyume na kanuni ya 13 (1)(2) za kanuni za bunge,aidha baada ya vurugu kutokea bungeni, Spika alishindwa kuahirisha kikao kwa muda kinyume na kanuni ya 33 ya kanuni za bunge,”inasema sehemu ya tamko hilo.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo,kutokana na vurugu kutokea bungeni,maamuzi yaliyofikiwa bungeni ni maamuzi ya wabunge wachache na ni kinyume na kanuni ya 35 ya kanuni za bunge.

  Bodi ilifafanua kuwa katika katiba ya Daruso ibara ya 14(14) (15) ya katiba ya daruso na kanuni ya 41(10(2) ya kanuni za bunge, hakuna maamuzi ya kuondoa rais na serikali yake, kwa kuwa vipengele hivyo, vilikiukwa.
   
Loading...