MTV MBONGO
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,261
- 1,222
Serikali imekuwa ikishindwa katika kesi nyingi sana ambazo makosa yake yanaonekana wazi na wajuzi katika sheria wanakuwa wanajua ni adhabu gani itatolewa. Lakini cha ajabu hata makosa ya wazi utaona mtu anaaibuka mshindi.
Mara unasikia serikali wamekata rufaa na wakati mwingine wanashindwa hata rufaani. Wakati mwingine hawahangaiki tena na kesi hizo. shida iko wapi? ni udhaifu wa mawakili wa serikali na taasisi za dola kama TAKUKURU au ni rushwa kukithiri mahakamani? tafakari kesi chache zifuatazo:
1. Kesi maarufu ya Zombe na wenzie ambapo walidaiwa kuwaua watu wanne na kubeba mali zao. waliachiwa huru na mahakama kuu. waliokufa sasa waliuliwa na nani? serikali inadai inakata rufaa.
2. Hivi karibuni mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ilimwachilia huru aliyekuwa mkurugenzi wa TANESCO bw. Mhando ktk kesi ya matumizi mabaya ya madaraka ambapo mke wa Mhando alipewa tenda na TANESCO na hakimu akadai inawezekana Mhando hakuhusika. Wakili wa TAKUKURU alidai mahakama ya Kisutu imejaa rushwa. Wadau mnaonaje katika haya mkizingatia kesi nyingi mzijuazo?