Serikali kujenga zahanati 3 kila Halmashauri nchini

Serikali kujenga zahanati 3 kila Halmashauri nchini

Joined
Apr 4, 2020
Posts
16
Reaction score
7
1586434482545.png


Serikali imesema kila halmashauri itajengewa zahanati tatu kwa lengo la kusogeza huduma za afya karibu kwa wananchi wake.Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Wazir wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka 2020/2021 ya wizara hiyo Jijini Dodoma.

Mhe.Jafo amesema kuwa serikali itafanya Ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali 67 za halmashauri ili kuziwezesha kuweza kutoa huduma katika ubora unaohitajika.Kwa upande mwingine amesema kuwa serikali inakamilisha ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa katika shule zote za halmashauri 184.

“Mhe.Naibu Spika serikali itajenga maabara saba katika kila halmashauri ili kuwezesha masomo ya sayansi kufundishwa katika ubora unao hitajika na kutoa wanafuzi wenye ujuziunaohitajika,”amesema Mhe.Jafo.Pia Mhe. Jafo amesema kuwa serikali inaendelea kusimamia shughuli za utawala bora na Kuratibu ujenzi wa miundombinu na shughuli katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ili kuleta utendaji mzuri katika ofisi za serikali na wananchi kujifunia huduma zitolewazo na serikali yao.Aidha Mhe. Jafo amesema kuwa serikali itasimamia vyema Halmashauri 30 kuamia katika majengo yake ya utawala na Kutengeneza barabara zenye urefu wa kilomita zaidi ya elfu tatu katika miji na vijijini.
 
Mipango ya kijinga sana hii.

Kwanini wasiseme kita kijiji/kitongoji wajenge zahanati?

Hatua ya kwanza ni kutambua vijiji/vitongoji visivyo na zahanati.

Hatua ya pili piga gharama ya kujenga zahanati moja mijini na vijijini.

Tatu weka mkakati wa kumaliza jambo hili la zahanati.

Hakuna kuanzisha kijiji wala kitongoji kama hakuna huduma za jammii.

Hizo pesa mnazo tumia kununulia wabunge wa chadema na kuitisha chaguzi zisizo na kichwa wala miguu zingetosha kumaliza tatizo la zahanati in just 2 years.

Unapo sema zahanati 3 kila halmashauri ina maana katika nchi hii hakuna halmashauri iliyo kamiliki kwenye huduma.za afya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom