Serikali kujenga Mgodi wa Makaa ya Mawe na Chuma wa zaidi ya Shilingi Trilioni 6

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
PIX%2B1.JPG


JUMLA ya dola Bilioni 3 za Kimarekani zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa Mgodi wa Makaa ya Mawe na Chuma wa Liganga na Mchuchuma.

Kauli hiyo imetolewa Leo mjini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage wakati akiongea na Waandishi wa habari mjini Dodoma.

Amesema mradi huo unaojengwa kwa ubia kati ya Tanzania Kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Kampuni ya China ya Sichuan Hongda Group unatarajia kuanza mwaka huu.

Mhe. Mwijage amesema kuwa fedha za kuwalipa fidia wananchi wanaozunguka maeneo ya mradi huo ziko tayari ambapo zinatarajiwa kutumika zaidi ya bilioni 13 kwa ajili ya fidia na makazi.

Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasadia kuzalisha umeme Megawati 600 ambapo 250 zitatumika katika Kiwanda cha Chuma na nyingine 350 zitapelekwa kwenye Gridi ya Taifa kwa ajili ya kuongeza nguvu katika nishati ya umeme.

‘’Pamoja na kuchimba chuma, Mradi wa Mchuchuma na Liganga utahusisha ujenzi wa Kinu cha Umeme chenye uwezo wa Megawati 600”, alisema Mhe. Mwijage.

Ameongeza kuwa, Tanzania kwa sasa itakuwa na umeme wa gesi, maji na umeme wa makaa ya mawe ambapo umeme wa makaa ya mawe utakuwa msaada mkubwa kwa nchi kwani hautegemei tabianchi kama ilivyo vyanzo vingine vya umeme.

Mhe. Mwijage amesema kuwa katika mradi huo, Tanzania itakuwa na hisa asilimia 20 na Mwekezaji kutoka China atakuwa na asilimia 80, lakini hisa za Tanzania zinaweza kuongezeka hadi kufikia 45.
Chini ya mradi huo, Mwekezaji huyo anatakiwa kutoa elimu kwa Vijana katika ngazi zote za teknolojia zitakazohusika kutengeneza mgodi huo.

"Tutafundisha vijana wetu kwa ngazi tofauti kwani kampuni hii ni ya ubia kati ya Tanzania na China, tuna mamlaka sawa, tuna Wakurugenzi wetu wa Tanzania ndani ya hiyo kampuni, kwahiyo tutashiriki na hatutakuwa watazamaji”, alisema Mhe. Mwijage.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayosimamia Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambaye pia ni Mtaalam katika masuala ya madini, Mhe. Dkt. Dalaly Kafumu amesema kuwa, lengo la kuwajengea makazi wakazi wa maeneo ya mradi huo ni kuwawezesha wakazi hao kuwa na uhusiano mzuri na mgodi unaotarajiwa kujengwa.

‘’Serikali imeamua kuwajengea makazi wananchi ambao wanazunguka mradi Ili kuepusha wakazi hao kutumia pesa watakayolipwa kama fidia kwa matumizi mengine na kukosa makazi baadaye kuja kuilaumu Serikali kwamba imewadhulumu kwa kutowapa pesa za kutosha za kujenga nyumba”, alisema Dkt. Kafumu.

Chanzo: Michuzi
 
duh! CAG aliliongelea hili na alitoa maoni yake ambayo nafikirii yalikuwa mazuri kuliko kutuaminishankuwa mna mamlaka sawa wakati hisa mlizonazo ni 20 na wao wana hisa 80.

Labda husiwe mwelewa kwenye mfumo wa kibepari wa hisa ndiyo utaaamini haya.
 
Hayo mamlaka mtayatoa wapi na hiyo asilimia 20 yenu?
Hapo mmeuza tu na kwa managements za Kichina wafanyakazi mpaka watapigwa bakora.
 
We are tired of porojo lakini inakuaje hadi wao wawe na 80% vs 20% za Tanzania afu kuwe na nguvu sawa? Kwa mchina bora mzungu utumwa kwa vibarua wakitanzania utakua kama kwenye migodi ya shaba huko Zambia
 
Kweli amechuja 20%Tz and 80% Chinese.Really,can someone tell me where are we heading?
 
...Fedha inayohitajika kwenye hiyo miradi miwili ni ndefu, ndio maana. Kitu cha muhimu ni nafasi ya kuongeza hadi kufikia 45%.


Bora tukope tudaiwe lakini 100% ya mradi tumiliki wenyewe baadae tunawauzia wafanyabiashara wazawa hisa serikali inabaki kuchukua kodi
 
...What if tungemwachia yote, kama dhahabu.

...Uwekezaji huo unahitaji hela ndefu, ambayo hatuna kwasasa, na hata kama ipo, inahitajika kwengine.

...Cha muhimu ni nafasi ya "kuhamisha goli" mpaka 45% tukiwa na hiyo fedha.
Tuiache mpaka tutakapokuwa na uwezo.Huoni tunaibiwa mchana kweupe.Fungua ubongo mkuu.
 
Kwani hayo madini tukiyaacha Kuna tatizo?, 20:80 hii ni ngumu kumeza
...Ndio, tunahitaji hiyo fedha, ajira, teknolojia na ufundi, maendeleo, n.k., kutoka kwenye hiyo miradi.

...Nia ya kuwa na viwanda haiwezi kutekelezeka kama miradi hiyo itabaki kwenye maandishi.
 
Bora tukope tudaiwe lakini 100% ya mradi tumiliki wenyewe baadae tunawauzia wafanyabiashara wazawa hisa serikali inabaki kuchukua kodi
...Mpaka sasa tunadaiwa kiasi gani? Hatuwezi kukopa bila kikomo!

...100%? soko liko wapi? wateja kina nani? supply chain ikoje? Si rahisi kuzalisha chuma kiasi hicho na kutegemea utamuuzia mChina au mwengine yeyote kirahisi.
 
Back
Top Bottom