Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Wizara ya Uchukuzi kwa niaba ya serikali na Benki ya dunia, Trade Mark East Africa na Department For International Development (DFID) zimetiliana saini ya makubaliano ya shillingi trilioni1.5 kutekeleza mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es salaam.
Fedha hizo zitasaidia uboreshaji wa miundombinu ya Bandari na uhamishaji wa gati la mafuta la KOJ pamoja na mabomba ya mafuta katika eno la ujenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Mkurugezi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Alex Mamtei alisema kuwa makubaliano hayo yatasaidia kutatua tatizo la uchakavu wa miundombinu na kuongeza kina cha maji pamoja na lango la kuingilia kwenye meli.
"Bandari ilivyo sasa kina cha maji ni kifupi mno na miundombinu inatisha kwa uchakavu wake, hivyo wizara ya uchukuzi kwa niaba ya Serikali imeamua kuungana na wadau tajwa ili kufanya marekebisho ya haraka kunusuru Bandari na mapato yake," alisema Mamtei.
Hatua hii ni nzuri sana, keep it up Magufuli.....
Chanzo: Mwananchi