comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inaandaa utaratibu wa kutaifisha mifugo yoyote itakayoingizwa katika maeneo yaliohifadhiwa ili kuokoa uharibifu wa mazingira unaosababishwa na mifugo katika maeneo yote yaliohifadhiwa, hayo yalisemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alipofanya ziara katika wilaya ya Longido na kujionea uharibifu mkubwa wa mazingira uliosababishwa na mifugo, Aidha ameagiza maeneo yote ya mipaka ya Hifadhi na wananchi yahakikiwe, zoezi hilo linaendelea kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya makazi, Wizara ya maendeleo ya Mifugo, Wizara Nishati na Madini na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuainisha mipaka sahihi na kuondoa migogoro
Chanzo: ITV
Chanzo: ITV