bushland
JF-Expert Member
- Mar 6, 2015
- 7,015
- 4,984
Jamani kulingana na kichwa cha habari hapo juu,
Tafadhali serikali naomba mfanye mapinduzi ya kilimo kwani ya viwanda yametushinda kutokana na uhitaji mkubwa wa gharama za manunuzi ya machine, mitaji pamoja na changamoto nyingine lukuki.
Naomba tufanye kilimo kwani tukifanya mapinduzi ya kilimo ni rahisi pia kupata wawekezaji wa viwanda. Nguvu kazi ya vijana tunayo ya kutosha tena imezidi. Maeneo ya ardhi ya kilimo tunayo mengi tu.
Maji ya mabwawa, Mito maziwa vinatosheleza kuleta mapinduzi ya kilimo. Hatuwezi kufanya mapinduzi ya viwanda ilhali kilimo kimetushinda jamani. Mfano mzuri ni nchi ya America mapinduzi ya viwanda yalianza miaka ya 1820-1870 na yalileta mafanikio makubwa sana wakati huo na hadi sasa.
Serikali itoe maeneo, vifaa vya kilimo, madawa, mbegu kwa vijana kupitia serikali za mitaa waone nguvu ya vijana tulio nao.
Sasa basi naomba tuangalie faida za mapinduzi ya kilimo katika nchi yetu.
1.Ajira, idadi kubwa ya watu wasiokuwa na kazi watajiajiri katika kilimo, na hivo tukaondoa tatizo la ajira nchini.
2.tutakuwa na viwanda vingi ikiwemo vya nguo zitokanazo na kilimo tukifanyacho kama Vile nguo za Sufi, viatu vya ngozi, kutokana na ufugaji. Nk.
3.fedha za kigeni, nchi yetu inaweza pata fedha za kigeni kwa wingi kutokana na kuuza Mazao yetu nje.
4.Msimu WA mavuno Ni msimu mzuri kwa mwaka kwani watu wengi huwa nafuraha kutokana na kwamba mzunguko WA hela unakuwa.vizuri.
5.kilimo Ni chanzo kikubwa cha upatikanaji WA chakula cha kutosha katika nchi na katika familia kwa jumla
.
Hapo juu nimeeleza kwa uchache faida zitokanazo na mapinduzi ya kilimo
Sasa basi baada ya kilimo viwanda vitatokea Tu ,
Hatuwezi waza kujenga viwanda wakati hakuna uzalishaji WA kutosha,
Kuna vitu vya kufanya siasa lakini sio maisha.yetu wenyewe jamani,