BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,126
Wabunge CCM wapigwa ‘stop’ mijadala utekaji
www.ippmedia.com/sw/habari/wabunge-ccm-wapigwa-%E2%80%98stop%E2%80%99-mijadala-utekaji
Tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti Aprili 4 wabunge wamekuwa wakiwasilisha hoja nzito zikiwamo za kuwapo kwa kikundi kinachoendesha utekaji wa watu, madai ambayo yamekuwa yakiibua mijadala mikali bungeni na wakati mwingine 'kutafuna' muda wa shughuli zingine za Bunge.
Hali haikuwa nzuri zaidi bungeni katika vikao vya Jumatatu na juzi baada ya wabunge wa CCM, Hussein Bashe (Nzega Mjini) na Aeshi Hilaly (Sumbawanga Mjini) kudai kutishiwa kutekwa na kuuawa na kikundi hicho huku Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) akidai kikundi hicho kinaratibiwa na idara nyeti ya serikali.
Muda mfupi baada ya Zitto kutoa madai hayo bungeni juzi, Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu, aliyekuwa anaongoza kikao, alitangaza kuwa wabunge wote wa CCM walikuwa wanaombwa kuhudhuria kikao cha chama kilichofanyika mjini hapa kuanzia saa 2:00 usiku.
Chanzo kutoka ndani ya kikao hicho kiliiambia Nipashe jana kuwa katika kikao hicho, yalizungumzwa mambo mengi yakiwamo ya utekelezaji wa bajeti ya serikali na hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wabunge, ikiwemo baadhi kuhofia maisha yao kutokana na kudai kupewa taarifa kuwa muda wowote watatekwa au kuuawa barabarani.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, wabunge wa chama hicho walizuiwa kujadili bungeni na kuwasilisha hoja ambazo zinatoa taswira hasi kwa chama na serikali iliyoko madarakani.
"Tulizungumza mengi, lakini kubwa lilikuwa bajeti ya serikali. Yaliibuka mambo kadhaa.
Wapo wabunge wanaohofia usalama wao, walihakikishiwa suala hilo litafanyiwa kazi," chanzo chetu kilieleza.
Chanzo hicho kilidai kuwa baadhi ya wabunge walionywa kutokana na kuwashambulia baadhi ya mawaziri na huku kukitolewa onyo kwa wanaodaiwa kutoa siri za mkutano uliotangulia ambao wabunge wa CCM walikutana na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kwenye jengo jipya la makao makuu ya chama hicho mjini hapa.
Hata hivyo, chanzo chetu kilieleza kuwa licha ya onyo hilo kutolewa, uongozi haukutaja majina ya wabunge waliotoa siri za mkutano huo kwa vyombo vya habari.
MOJA TU
Alipotafutwa na Nipashe kwenye viwanja vya Bunge jana mchana, Katibu Msaidizi wa Wabunge wa CCM, Abdallah Ulega, alisema ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa bajeti ya serikali.
Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga, alisema katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wabunge wa CCM walielekezwa mambo mbalimbali yanayohusu bajeti ya serikali na jinsi ya kuchangia mijadala bungeni.
"Ajenda yetu ilikuwa moja tu, bajeti ya Waziri Mkuu. Tulijadiliana na tukafika mahali tukakubaliana kwa pamoja.
Kwa hiyo, tulikuwa tunajadiliana namna ya kuhitimisha, wapi panaonekana kuwa na kasoro turekebishe, wapi pamekaa vizuri tuboreshe zaidi," alisema Ulega.
"Sisi ni chama kinachotawala na hii tuliofanya jana (juzi) ni kawaida ya mabunge yote ya nchi za 'Commonwealth' (Jumuiya ya Madola). Lazima mkutane, mpeane pale unapoona hapa pana tatizo, mnawekana sawa. Pale panapoonekana sawa, mnaboresha zaidi 'then' (kisha) mnakwenda kwa pamoja."
Alipoulizwa kuhusu madai ya kujadiliwa katika kikao hicho hoja zilizokuwa zimewasilishwa zikiwamo za matukio ya utekaji na hofu ya usalama wa wabunge, Ulega alisema: "Kila mtu ana haki yake, usalama wa mtu ni usalama wake mwenyewe.
"Lakini yapo mengine ambayo mimi kama Katibu Msaidizi, nasema huwa tunaitana katika vikao vyetu vya kichama kwa sababu serikali yenyewe yote ipo katika kikao hicho cha chama.
Mkuu wa serikali ndiyo mwenyekiti wa hicho kikao kwa maana ya Waziri Mkuu.
"Kwa hiyo, katika mkutano wa wabunge, yeye (Waziri Mkuu) ndiye mwenyekiti, Spika anakuwapo pale na wengine wote. Kwa hiyo, unaweza ukayasema kwa mapana zaidi, ndiyo utamaduni wetu.
"Haikatazwi kuyasema bungeni kama mbunge lakini tunazungumzia kanuni za kiuendeshaji za mabunge ya Jumuiya ya Madola.
Masuala ya chama yanazungumzwa ndani, mnatoka mkiwa pamoja na kama kuna wingu lolote, linasafishwa pale ili mkienda mnakuwa sawa.
"Na kuna namna ya 'approach' vilevile. Wewe ukiwa mbunge wa chama kinachotawala na mbunge wa chama cha upinzani, 'approach' yenu katika kuyaendea mambo haiwezi kuwa inafanana.
"Kwa kifupi kikao kilikuwa kinazungumzia namna tunavyokwenda kuhitimisha hoja ya bajeti ya Waziri Mkuu.
Hii ndiyo ilikuwa ajenda kuu, hayo mengine yawezekana yalizungumzwa kama unavyofahamu hiyo ilikuwa ajenda nyinginezo tu."