Kwa sasa, kuna changamoto kubwa katika sekta ya afya, hasa kwenye suala la uchunguzi wa awali kwa njia ya maelezo ya mgonjwa (oral diagnosis).
Madaktari wengi waliopo kwenye hospitali na vituo vya afya wamekuwa wakishindwa kufanya uchunguzi huu kwa usahihi.
Wengi wao hujikuta wakitoa dawa kwa magonjwa ambayo mgonjwa hana, kwa sababu hawakufanikiwa kutafsiri kwa usahihi maelezo ya mgonjwa hadi kufikia kubaini tatizo halisi.
Hii inatokana na ukosefu wa muda wa kutosha, uzoefu mdogo, au mfumo wa haraka haraka (fast-track) unaowafanya madaktari wengi wa sasa kuwa wa “mwendo kasi.”
Matokeo yake ni wagonjwa kupewa dawa zisizolingana na matatizo yao, jambo linaloweza kusababisha madhara makubwa zaidi kiafya. Ushahidi wa hali hii upo mitaani.
Napendekeza serikali iwekeze zaidi kwenye ununuzi wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali – hasa kwenye vituo vya afya vya kata na wilaya ambako huduma za vipimo ni duni au havipo kabisa.
Vilevile, ni muhimu kuandaa wataalamu mahiri wa kuendesha mitambo hiyo ya uchunguzi, ili madaktari wasitegemee tu maelezo ya mgonjwa, bali vipimo viwe sehemu muhimu ya mchakato wa kutoa tiba.
Majibu ya vipimo ndiyo yawe msingi wa maamuzi ya kitaalamu kuhusu ugonjwa wa mgonjwa.