dumesuruali
JF-Expert Member
- Dec 2, 2016
- 287
- 621
Ni takribani mwaka wa nne sasa nipo kikazi Kasulu,,mkoani kigoma..
kimsingi hali ya barabara kutoka nyakanazi(njiapanda ya biharamulo na kigoma) mpaka kufika kasulu mjini barabara ni mbovu mno kiwango cha vumbi na mashimo ya kutosha..
Hali hii inasababisha usumbufu mno hususani kipindi hichi cha mvua...wanachofaya manispaa ni kupitisha greda na kukwangua barabara bila kuweka vifusi au hata changarawe tu...
Pichani hapo ni jana kilometa saba toka kasulu mjini mvua kubwa ilinyesha kiasi cha kusababisha tope na magari kukwama nami nikiwa muhanga wa adha hiyo kwani nililazimika kulala mjini na kuondoka asubuhi ya leo kurudi kazini..
Naipongeza wilaya ya buhigwe kwa kutengeneza barabara yao kwa kiwango cha changarawe na hali ipo vizuri kuelekea manyovu mpaka kigoma mjini...
viongozi wa halmashauri ya wilaya ya kasulu tizameni hili kwa jicho lingine...hali ni mbaya...