Serikali itangaze kufuta ajira kwa viongozi wote wa Mashirika ya Umma na Halmashauri

Afyayaakili

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
923
1,255
Naona karibu taasisi zote za serikali wakuu wote walioudumu katika kipindi kilichopita wana harufu ya ukiukwaji wa maadili katika utendaji wao au kushindwa kuwasimamia wafanyakazi waliochini yao.

Sasa naona ni muda mwafaka kwa serikali kutangaza kufuta ajira zote za wakuu katika halmashauri na sekta zingine za umma, menegimenti ya ajira ipewe jukumu kwa kuangalia watu wanaostahili na wenye uzalendo kwa taifa.

Nasema hivi kwa sababu mfumo umeonekana kuwa ulikuwa umeoza kupita maelezo sasa ni wakati wa watu wenye nguvu na uzalendo kwa taifa kuingia kufanya kazi na kulikomboa taifa katika ombwe hili lenye uozo mzito maana ishakuwa sio majipu tena na kansa ambayo ni lazima kipande kichoasirika na hiyo kansa kitolewe kuliko kutishia kwa kupasua na kupaka dawa ya kuua bacteria wa juu wakati chini wapo kibao.

Kama hili litatokea kuna raia wa kitanzania wengi tuu wenye Elimu na weledi ndani na njee ya Tanzania wanaoweza kuongoza haya mashirika na halmashauri za serikali.
 
Siku zote tulisema tatizo mfumo watu wakatokwa na mapovu humu hongera kwa rais make amewasikiliza wapinzani sasa ameamua kujitoa mhanga kukabiliana na mfumo.
 
Kufuta wote? ni wazo zuri lakini itakuwa ni vigumu. Nafikiri waendelee kuwachomoa mmoja mmoja mpaka wote wabovu waishe. Lakini nakubaliana kabisa kwamba kwa mambo yalivyo, kila sekta imeoza. Watafukuzwa wengi sana.
 
Back
Top Bottom