Serikali italipa malimbikizo ya mishahara?

Kazimzubwee

Member
Nov 7, 2016
51
57
Je uhakiki utapoisha serikali itawalipa watumishi wake mishahara mipya pamoja na malimbikizo tangu mwezi wa saba?

Au uhakiki ni wa kudumu? Maana bunge lilipitisha bajeti tangu mwezi wa saba lakini wanyakazi wanataabika hadi leo maisha yamekuwa tight na hakuna wa kuwafariji,kisa uhakiki hewa unaoendelea au hazina hamna fedha?

Au ndo mwendo kasi. Maana laki tatu kwa mwalimu na millioni 35 kwa baba,hapa ni parefu sana huyu wa chini anaishije?au ni kweli msemo alieshiba hamkumbuki mwenye njaa?

Maana viongozi wetu mishahara yao ni minono wanakula wanasaza hawamjali wa chini maana kwao Tanzania zipo Mbili.
 
Hii ipo kisheria nyongeza ya mshahara ni tarehe 1 july, leo mwezi 11 hakuna chochote. Kuna watu wakupanda madaraja na wanastahili hadi leo kimya, kuna watu tunastahili kulipwa malimbikizo yetu hadi leo kimyaaaaaa unahakiki unaendelea non stop......
 
Da! Kama halmashauri ya MVOMERO inaongoza kwa mkoa Wa MOROGORO kwa malimbikizo badi wapo watumishi pale wanadai zaidi ya miaka 5
 
Hili la kusema 'au hazina haina fedha' halikubaliki. Kwa sababu serikali ingetoa tamko rasmi la malipo hayo kufanyika kuanzia muda flani flani wakaeleweka, kuliko ilivyosasa imani ya watumishi wa serikali inazidi kupotezwa na ukimya huu wa kitapeli unaofanywa na serikali hii.

Kwani kama bado wanajipanga kitu gani kinachowazuia kutoa tamko? kuna raia atabishana nao? Kama wanajinasibu kuwa ni wakweli na wapenda haki, je kuzungusha haki za watu kimyakimya hiyo ni haki kweli?

Ni nani kwa jina tumjue anayewajibika kutuliza sintofahamu hii na kurejesha ari ya wafanyakazi, aliyekaa kimya bila sababu?

Lakini nadhani kuna kampeni kubwa sana imeandaliwa ya kumharibia mheshimiwa kwa kupitia ushauri mbovu, ili mwisho wa siku raia wauchoke utawala huu kabisa.

Chakushangaza waziri mwenye dhamana hiyo yupo na anapiga mshahara bila wasiwasi wowote, hapo inamaanisha nini? kuna kitu nyuma ya pazia kinaandaliwa kisayansi na mamluki waliopo serikalini, lazima kipo tu. Ninasema hivyo kwa sababu tangu utawala wa Nyerere kuja Mwinyi,enzi hizo kulikuwa na hali mbaya sana ya uchumi, lakini sijawahi kusikia ama kuona haki za wafanyakazi zinachezewa kama inavyofanyika hivi sasa, sijawahi kuona, yaani bado.
 
Kiukwel mpaka sasa dhamira ya serikali naona ni kutesa na kuongeza ugumu wa maisha kwa watumishi na wananchi wote, uhakiki miez6? Hii sasa hakuna! Na sizani kama malimbikizo yatalipwa kwan imani sasa na SERIKALI hii ni 0,

Kuna baadhi watumish waliositishiwa ajira zao June,wamerdshwa wachache na wameenda kusain mipya sio ile walosaini kabla kusitishiwa, mkataba umesoneka wameanza Nov 1,2016 na hakna Malipo ya MUDA ulopita wala hela kujikimu!

Hii ni ishara mbaya sana, bado wengine hawajaitwa mpaka sasa! Watumishi umma wamekuwa kama wakosaji yaani hii tz ni shda!

Wakati wao huko juu wanakula na kunywa na kukalisha matako yao ofsin tu, huku chini vumbi sio vumbi Bali ni hatari,

Watu wakiongea inakuwa wanachochea! Too much! Kila mtu anahaki kuishi tena vizr nasio kuwa kama mkosaji!

Bajet imetengwa,Malipo hafifu, AJIRA mpya hakna sasa hawa wanafanya nn?

Tumechoka kusoma namba tunataka tusome herufi sasa!
 
Hii ipo kisheria nyongeza ya mshahara ni tarehe 1 july, leo mwezi 11 hakuna chochote. Kuna watu wakupanda madaraja na wanastahili hadi leo kimya, kuna watu tunastahili kulipwa malimbikizo yetu hadi leo kimyaaaaaa unahakiki unaendelea non stop......
Wakati mwingine hizi trade unions au vyama vya wafanyakazi kazi ni nini hasa?
Kula posho kwenye vikao au kuna lingine?
Kama vyama haviwezi kupiga kelele kuhusu haya ya msingi kabisa, wataweza lipi?
Aliyeviroga vyama vya wafanyakazi alishakufa kitambo!
 
Malimbikizo lazima yalipwe.Ukisikia madeni ya Serikali ndio kama hayo.
Ninachopendekeza hapa ni kwamba ipo haja ya Bunge kutunga sheria ili pawe na riba maana wakati mwingine deni linakaa hata miaka mitano halafu unalipwa kiwango kilekile wakati kiuhalisia thamani ya pesa inakuwa imeshuka.
 
walisema serikali yao haitakuwa ya michakato, sasa sijui hii michakato ya vyeti mara uhakiki mara picha mara vitambulisho vya taifa mara vyeti vya ndoa nk inatoka wapi, ".......politicians are hypocrits..... Me against the world" Tupac Omar Shakur
 
Wakati mwingine hizi trade unions au vyama vya wafanyakazi kazi ni nini hasa?
Kula posho kwenye vikao au kuna lingine?
Kama vyama haviwezi kupiga kelele kuhusu haya ya msingi kabisa, wataweza lipi?
Aliyeviroga vyama vya wafanyakazi alishakufa kitambo!
TUCTA imechagua viongozi wapya ngoja tuwaone
 
Malimbikizo lazima yalipwe.Ukisikia madeni ya Serikali ndio kama hayo.
Ninachopendekeza hapa ni kwamba ipo haja ya Bunge kutunga sheria ili pawe na riba maana wakati mwingine deni linakaa hata miaka mitano halafu unalipwa kiwango kilekile wakati kiuhalisia thamani ya pesa inakuwa imeshuka.
Kisha kodi wanakata kwa viwango vya wakati uliopo
 
Fedha zipo FIXED ACCOUNTS Wanapata FAIDA kwanza. """"tumejipangaaaaa Mwakaaa huu Wataisomaa""
 
Hizo pesa naona zikajenge Ubungo interchange, maana hadi sasa tuna vibilioni 67 tu, havitoshi kwa kweli, ujenzi wa hii flyover ni gharama sana
 
...serikali hii ni bomu ambalo litawapasukia 2020...we waache waendelee kuwatesa watumishi wa umma....itakula kwao mwisho wa siku...jana nmemsikia waziri wa utumishi akiwasema watumishi wanaodaiwa....sasa kama hamlipi stahiki za watumishi kwanini wasidaiwe???...nyie serikali mnawadai watumishi kwa nguvu....lipeni haki na stahiki zao kwanza...ili waweze kulipa madeni yao.....
 
Tucta wanafiki hawana lolote malalamiko kuhusu madai ya watumishi yanaongezeka Kila kukicha hakuna wanachokifanya Kazi kupiga mbeta tu pia hawana technics mpya za kuifanya serikali ilazimike kulipa madai hayo
 
Back
Top Bottom