Serikali isimfunge mikono Mh Nyalandu

Serikali isimfunge mikono Mh Nyalandu

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,956
Reaction score
25,348
Natoa wito kwa serikali ya chama cha mapinduzi kama kweli wanapenda kushinda vita dhidi ya ujangili waache kumfunga mikono Mh Lazaro Nyalandu ili awanusuru tembo na wanyamapori wengine wanaoangamia kila siku kutoka na kasi ya ujangili. Nimesikitishwa sana na kitendo cha serikali kuwarejesha kazini watendaji wanaohujumu vita dhidi ya ujangili. Mh Nyalandu alikuwa akitekeleza maazimio ya ripoti ya bunge kuhusu operesheni ujangili, zoezi ambalo halikufanikiwa kufuatia kuingiliwa na kuvurugwa na wanufaika wa ujangili.

Utenguzi wa adhabu aliyotoa Nyalandu kwa watendaji wa wizara yake kama sehemu ya maagizo ya ripoti ya Tume ya Lembeli yanatupa wasiwasi kwamba huenda kuna viongozi ndani ya chama na serikali wanaonufika na ujangili huu wa wanyamapori.

*************************************************************************************
Sasa ni dhahiri kwamba kuna msuguano wa wazi kati ya mihimili miwili ya dola, Bunge na Serikali, kuhusiana na hatua ya Serikali kuchelewa kutekeleza maazimio ya Bunge.

Msuguano huo umeshika kasi wiki hii baada ya Serikali kuwarudisha kwenye nyadhifa zao vigogo wawili wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambao hivi karibuni waliondolewa na Waziri Lazaro Nyalandu, huku wabunge wakiapa kuibana Serikali kuwang'oa viongozi hao.

Vigogo hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa na Mkurugenzi Msaidizi, Jaffar Kidegesho kwa madai ya kutowajibika ipasavyo katika vita dhidi ya ujangili nchini.

Mbali na sababu hiyo, lakini Nyalandu alikaririwa akisema alichukua uamuzi huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mazimio 16 ya Bunge, yaliyotolewa baada ya taarifa ya Operesheni Tokomeza Ujangili.

Ikulu yatoa tamko

Wakati mvutano huo ukiendelea, Ikulu imeitaka wizara hiyo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kumfukuza mtu kazi.

Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema kuzingatiwa sheria, kanuni na taratibu za kumfukuza mtu kazi ndiyo suluhisho la msuguano unaoendelea kati ya Waziri Nyalandu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi juu ya hatima ya wakurugenzi hao ambao walitimuliwa kazi Februari mwaka huu.

Balozi Ombeni aliwataka viongozi hao kuhakikisha kuwa uamuzi wowote wanaoufanya kuhusu kuwaondoa kazini watumishi hao unazingatia sheria, taratibu na kanuni kwa kuwa zinaeleza wazi hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

"Siwezi kujua kwa nini wanaendelea kuvutana, hilo waulize wao, ninachojua wanatakiwa wazingatie sheria, kanuni na taratibu katika jambo hilo," alisema.

Alipoulizwa ni nani kati ya Nyalandu na Tarishi hafuati sheria za utumishi wa umma, alisema: "We mwenyewe nenda kazisome (sheria) utajua tu."

Kwa mujibu Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002, Kifungu cha IV (23) (2) inayozungumzia mamlaka ya Rais kumwondoa mtumishi aliyemteua kazini, amri ya kumfukuza mtumishi wa umma itatekelezwa iwapo

(a)hati ya mashtaka imeandikwa dhidi yake

(b)mtumishi wa umma amepewa nafasi ya kujibu mashtaka hayo

(c)Maombi yametolewa kwenye hati ya mashtaka kwa mujibu wa taratibu zilizo chini ya kifungu namba 34.

Ripoti ya uchunguzi wa matatizo katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, azimio namba saba lilimhusu Profesa Songorwa kwa jina lake na cheo chake likitaka Serikali kumwajibisha kwa kuudanganya umma kuhusu mazingira na kifo cha Emiliana Marrow wa Babati.

Uchunguzi wa madaktari huru na picha za mwili wa marehemu, zilionyesha alikufa kwa kuteswa na askari waliotekeleza Operesheni Tokomeza Ujangili, lakini taarifa ya Profesa Songorwa ikasema alikufa kwa Pressure (shinikizo).

"Bunge linaazimia Serikali ichukue hatua za kumwajibisha mkurugenzi wa wanyamapori kwa kuudanganya umma na kujaribu kuficha ukweli," linasomeka azimio hilo la Bunge la Desemba 20.

Hata hivyo, baada ya Nyalandu kumwajibisha Profesa Songorwa na mwenzake, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Maimuna Tarishi aliwarejesha kazini akidai kukiukwa kwa sheria za utumishi wa umma.

Wabunge mbalimbali waliohojiwa jana, walidai kinachoonekana kinatoa taswira kwamba Serikali inalitunishia misuli Bunge kila mara linapotoa maazimio ya kuwawajibisha watumishi wa umma.

Kwa mujibu wa Wabunge hao, siyo mara ya kwanza hali inayotokea sasa ndani ya Wizara ya Maliasili kutokea serikalini, kwani mazingira kama hayo yalitokea pia Wizara ya Nishati na Madini.

Mwaka 2011, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, David Jairo alirudishwa kazini baada ya kusimamishwa kazi kutokana na kutuhumiwa bungeni kuchangisha zaidi ya Sh50 milioni ili zisaidie kupitisha bajeti.

"Yanayotokea sasa Maliasili ni kama yaleyale yaliyotokea Nishati na Madini… Inaonekana kama ni sinema vile, tunapitisha (Bunge) maazimio lakini Serikali haitaki kuyatekeleza," alidai mbunge mmoja.

Waziri Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), David Silinde alisema kinachotokea Wizara ya Maliasili na Utalii ni mwendelezo wa Serikali kupuuza maazimio ya Bunge.

"Hata kwenye Hazina tulitaka TPDC (Shirika la Maendeleo ya Petroli) libakie na asilimia 100 ya makusanyo lakini mpaka sasa Serikali imepuuza na inalipa asilimia 50 tu,"alidai Silinde.

Silinde aliongeza kusema, " Hii ni tabia inayoanza kujengeka na sisi kama wabunge hatupaswi kuiacha izoeleke kwa hiyo mimi ni mmojawapo ambaye nitalihoji hili Bunge la bajeti wiki ijayo."

Kwa mujibu wa Silinde, mpango wake huo unaungwa mkono na wabunge wengine na kwamba watataka maazimio yote yaliyokwishaazimiwa na Bunge yawekewe kikomo cha utekelezaji.

Mbunge wa Bunda, Alphaxard Kangi Lugola ambaye alikuwa mwiba kwa Serikali na kuchangia mawaziri wanne kujiuzulu, alisema ameshtushwa na taarifa za kurudishwa kazini kwa vigogo hao.

"Mimi ndiyo kwanza niko uwanja wa ndege narejea sijasikia kama wamerejeshwa, lakini kama ni kweli basi kuna tatizo ila subiri nithibitishe hili ili nikisema niseme nikiwa na uhakika,"alisema Lugola.

Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya, alisema kilichofanywa na Serikali kuwarudisha vigogo hao kimejenga mazingira mabaya ya utendaji kazi kati ya Nyalandu, Tarishi na vigogo hao.

"Huku ni kumdhalilisha Nyalandu kwa sababu hata kama angekuja waziri mwingine yeyote ni lazima atekeleze maazimio hayo ya Bunge… kama kuna kasoro wazirekebishe lakini wawajibishwe,"alisema.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli alisema maazimio hayo hayakuwa yake kama Lembeli wala ya kamati bali yalikuwa ni ya Bunge zima.

"Hayo yanayotokea huko Maliasili nisingependa kuyazungumzia ila ninachoweza kusema maazimio ya kuwawajibisha watendaji hao yalikuwa ni ya Bunge zima na bado yanasimama kama yalivyo,"alisema.

SOURCE: Mwananchi

:yield:
 
Ndio maana TZ uandishi bado sana unatetea visivyopaswa kutetewa unaacha kutetea vinavyopaswa kutetewa...

safari bado ndefu.
 
Ndio maana TZ uandishi bado sana unatetea visivyopaswa kutetewa unaacha kutetea vinavyopaswa kutetewa...

safari bado ndefu.

Tuambie hivyo vinavyopaswa kutetewa ni vipi? Kama kutetea wanyamapori wanaotuingizia fedha za kigeni (zinazokulipa mshahara na kununulia gloves za kumzalisha mkeo) unaona ni upuuzi unataka tutetee nini? Sio kila post lazima uchangie. Yatosha ukasoma tu, ukaenda zako na utaelimika--kuliko kuandika ujinga usioweza kuujengea hoja! Haya ndio matatizo ya kushikiwa akili--siku zote huwezi kufikiri kwa kutumia akili zako binafsi. Pole sana.
 
Nyalandu ni fisadi na Mwizi.

Ukiona anapambana na akina Songorwa ujui anataka kujitengenezea himaya.

Kama ni utekelezaji wa maazimio Nyalandu naye ni victim.

Nimeshangaa Nyalandu kupewa uwaziri,NIMEIDHARAU CCM.
 
kama hao wakurugenzi wanapaswa kuwajibika na waziri Nyarandu pia anapaswa kuwajibika kwani wakati wa hiyo operation alikuwa naibu waziri cha ajabu amepewa promotion kuwa waziri kamili lakini pia rais ameteua tume ya kijaji kwanini wasisubiri ripoti ya hiyo tume mwisho wabunge waache unafiki kwani kuna maagizo mangapi hayajatekelezwa kuanzia richmond wamechukua hatua gani
 
Tuambie hivyo vinavyopaswa kutetewa ni vipi? Kama kutetea wanyamapori wanaotuingizia fedha za kigeni (zinazokulipa mshahara na kununulia gloves za kumzalisha mkeo) unaona ni upuuzi unataka tutetee nini? Sio kila post lazima uchangie. Yatosha ukasoma tu, ukaenda zako na utaelimika--kuliko kuandika ujinga usioweza kuujengea hoja! Haya ndio matatizo ya kushikiwa akili--siku zote huwezi kufikiri kwa kutumia akili zako binafsi. Pole sana.

Mkuu ungejua kilicho nyuma ya pazia anachofanya Nyalandu tangu enzi za u NW na jinsi ikulu ilivyomstukia usingetetea unachotetea...

That's why nikasema tunasafari ndefu...
 
Aanze kuwajibika Nyalandu kwa kushindwa kazi na asisingizie wakurugenzi. Aseme tu kuwa hao aliofukuza ni mabeki wanaozuia dili lake la ufisadi. Hivi alishaacha uhuni? nilishangaa sana alipopewa uwaziri kama donors walivyoshangaa Haji Mponda kupewa uwaziri hasa waswisi ambao walijua utendaji wake Mbovu Ifakara Health Institute (former Ifakara Health Research and Development Centre. Alikuwa amebebwa na former Director Hassan Mshinda kisa udini.
 
Nyalandu ni fisadi na Mwizi.

Ukiona anapambana na akina Songorwa ujui anataka kujitengenezea himaya.

Kama ni utekelezaji wa maazimio Nyalandu naye ni victim.

Nimeshangaa Nyalandu kupewa uwaziri,NIMEIDHARAU CCM.

Mkuu haya ndio yaleyale matatizo yetu baadhi ya watanzania kuishi na kutenda kwa groupthink...

Leo watu wanamwona Lembeli shujaa wakati huyo mtu anajitahidi sana kuivuruga wizara ya maliasili hasa viongozi ambao ni kizingiti kwao...

Kuna huyu mama Maimuna tarishi huyu anamsimamo mkali mno wa kiimani na kimaadili kama Hamisi Kagasheki lakini ndo wanaopigwa vita sana...

Juzi Nyalandu karudishwa Airport akisafiri kwenda SA kwa ajili ya mambo yao na lembeli Leo anaonekana msafi...

Ndio maana nasema tuna safari ndefu sana kuilewa siasa ya Tanzania yetu macho...
 
Ndio maana TZ uandishi bado sana unatetea visivyopaswa kutetewa unaacha kutetea vinavyopaswa kutetewa...

safari bado ndefu.

Ndo ulichokiona baada ya kusoma hyo habari? Kweli safari bado ni ndefu
 
Mkuu ungejua kilicho nyuma ya pazia anachofanya Nyalandu tangu enzi za u NW na jinsi ikulu ilivyomstukia usingetetea unachotetea...

That's why nikasema tunasafari ndefu...

Hapo sasa unaongelea udhaifu wa serikali na mtendaji mkuu kama kweli Nyalandu alishitukiwa mbona amepewa promotion kuwa waziri? Kwann mkurugenzi adanganye kuhusu riport ya kifo kama sio mnatuchezea mapicha
 
Mkuu haya ndio yaleyale matatizo yetu baadhi ya watanzania kuishi na kutenda kwa groupthink...

Leo watu wanamwona Lembeli shujaa wakati huyo mtu anajitahidi sana kuivuruga wizara ya maliasili hasa viongozi ambao ni kizingiti kwao...

Kuna huyu mama Maimuna tarishi huyu anamsimamo mkali mno wa kiimani na kimaadili kama Hamisi Kagasheki lakini ndo wanaopigwa vita sana...

Juzi Nyalandu karudishwa Airport akisafiri kwenda SA kwa ajili ya mambo yao na lembeli Leo anaonekana msafi...

Ndio maana nasema tuna safari ndefu sana kuilewa siasa ya Tanzania yetu macho...
Nyalandu hafai
 
Hapo sasa unaongelea udhaifu wa serikali na mtendaji mkuu kama kweli Nyalandu alishitukiwa mbona amepewa promotion kuwa waziri? Kwann mkurugenzi adanganye kuhusu riport ya kifo kama sio mnatuchezea mapicha

Aliyetoa promo sio mungu,ni yule yule anaepanga mara nyingi kikosi DHAIFU.
 
Jamaa amehamaki sana anahaha usiku na mchana Maimuna Tarishi aondoke wafanye yao jamaa anatamaa hatari
Nasikia kamweka Lembeli mfukoni.
Nilimkubali Lembeli ila sakata hili la Kagasheki amejimaliza.

But kama ni kuwajibishwa naye Nyalandu asteap aside kwani alikuwa hana cha kupotezewa.
HATA HIVYO namwona Nyalandu aking'olewa muda sio mrefu kutoka pale wizarani.
Nyalandu ni mmoja ya mawaziri wabovu kuwahi kutokea,wengine ni Kawambwa,Tibaijuka na akina Chikawe.
 
Jamaa alipika jungu zito akaja kustukiwa mwishoni...

Lembeli mtu mbaya sana wengi wameanza kumstukia..
Ile safari aliyozuiliwa na ikulu ilikuwa ya kifisadi...

Ikulu imecheza sana kumrudisha sorongwa pale idarani..

Nami naliona anguko lake
 
Tuambie hivyo vinavyopaswa kutetewa ni vipi? Kama kutetea wanyamapori wanaotuingizia fedha za kigeni (zinazokulipa mshahara na kununulia gloves za kumzalisha mkeo) unaona ni upuuzi unataka tutetee nini? Sio kila post lazima uchangie. Yatosha ukasoma tu, ukaenda zako na utaelimika--kuliko kuandika ujinga usioweza kuujengea hoja! Haya ndio matatizo ya kushikiwa akili--siku zote huwezi kufikiri kwa kutumia akili zako binafsi. Pole sana.

Kama ndugu/shemeji/rafiki yako Nyalandu anaona maamuzi ya Katibu Mkuu Kiongozi siyo sahihi ajiuzulu kama Mtangulizi wake Kagasheki. Toka lini amekua na uchungu na nchi hii? Njaa zake na kutumikia maslahi ya walio mpigia debe kupanda hapo juu ndiko kunasababisha uzalendo wa machozi ya mamba!!
 
Wakati mwingine huwa naangalia changizi za watu kama hawa then najiuliza wanajielewa? Kama ndio kwanini wanavaa uhusika usiowafaa?

Kama sivyo kwanini hawatafuti kujua ukweli?
 
Back
Top Bottom