Serikali isigawe bure ARV, inachochea uzinzi

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,833
Reaction score
140,900
Kwa kifupi
Kwa vigezo vilevile vilivyotumiwa kutokuruhusu watoto waliodungwa mimba mashuleni kwamba kurudishwa mashuleni kutachochea uzinzi. Kuna haja sasa ya serikali hii ya awamu ya tano kupiga marufuku ugawaji bure wa ARV kwa wagonjwa wa UKIMWI kwa kuwa inachochea uzinzi.

Magufuli atoe tamko kila mtu abaki na mkewe/mumewe, na hakuna kufanya ngono nje ya ndoa. Kwa kuwa vitabu vya dini zote vimekataza uzinzi, hivyo serikali itumie kigezo hicho kwa sababu hakina tofauti kabisa na kigezo ilichotumia kwa wanafunzi wa kike

Nadhani nimeeleweka
 
Mawazo mgando hayo,umeshasoma recent statistics toka ARV zianze kugawiwa!!?Maambukizi yameongezeka!!?

Je kipindi chote ambacho ARV zilikuwa hazitolewi,maambukizi yalikuwa chini kuliko kipindi ambacho ARV zimeanza kutolewa!!?

Unajua kiasi gani,ARV inapunguza maambukizi ya mama kwenda mtoto,Kati ya wanandoa!!?

Unafikiri kuacha kutoa kutapunguza maambukizi kwa study gani,uliuofanya!!?
 
Omba yasikukute.

Utakuwa hauwatendei haki wale waliozaliwa wakiwa tayali wamevipata na sasa hivi wako wengi kuliko walioambukizwa kwa ngono zembe.

Ni haki yao kupata dawa kama wapatavyo Wagonjwa wengine.

Pia dawa hizo ni za hisani kutoka Taasisi za nje.
 
Inabd ufaham kama mtu akianza arv hatakiwi kuacha maisha yake yote..utamdai sh ngap ??be human
 
Narrow Thinking!

Halafu shauri kama hizi pamoja na zile za Deo Kisandu ndizo ambayo Rais huwa anazichukua.Tatizo ni nini Lakini?.

Huwa hamtizami pande zote za shilingi.Hapa ndipo mzizi wa tatizo lilipo.
 
Good Thinking Mkuu!

Licha ya kuzaliwa nao (UKIMWI), pia zipo njia nyingi mno za maambukizi tofauti na Mleta mada alivyo base katika Njia moja tu (Ngono zembe).

Kwa uchache tu ni, kuwekewa damu yenye maambukizi ya UKIMWI katika taasisi za Afya, Ku-share zana zenye ncha kali pamoja na mwathirika nk.....(You can add).

Nadhani tatizo ni Uelewa mdogo juu ya Maambukizi ya Ugonjwa wenyewe na si vinginevyo.
 
Nimekuelewa mkuu mleta uzi ujumbe uliotaka kufikisha. Aisee!
 
Mleta mada ana maana kubwa kuliko mnachochangia hapo juu, ANYWAY SULEIMAN KANIITA KULA UBWABWA WA IDD
 
Nenda huko vijijini ukaone watu walivyo masikini halafu wana UKIMWI. Fikiri kabla ya kutoa post. Siyo wote tuna uwezo wa kula pilau leo!
 
Hizi ni pombe tu zimeandika hapa....
 
Ngoja uupate ndio utajua umuhimu wa hizi dawa....
Usidhani uzinzi pekee ndio utakufanya upate ukimwi..
Unajua PEP?
Sasa subiri dawa ziondolewe halafu kitoto chako cha miaka 3 kibakwe na muathirika...
Unajua wafanya kazi wa afya wanajichoma mara ngp na sindano wanapokuwa wanahudumia waathirika...??
Unajua wanatumia nini kujizuia virusi visianze kuzaliana muda ule alipojichoma.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…