Serikali ipo imara dhidi ya janga la COVID-19

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
137
179
Sikubaliani na baadhi ya makundi yanayojenga hoja kuwa Serikali yetu imeshindwa kupambana na janga la COVID-19 nadhani hoja hii ni dhaifu au inakusudio la kisiasa kwa maana ya kupotosha. Wanaojenga hoja hii wengi wapo mitandaoni, Binafsi naielewa nguvu ya mitandao kwa mantiki hiyo lazima tujibu tuhuma hizo dhidi ya serikali yetu.

Tuhuma zinazojengwa na wanaharakati na wapinzani wa serikali zinasimama katika mambo makuu mawili Mosi, Serikali imechukua hatua tofauti na mataifa mengine kama si ukanda wa Afrika mashariki na kati au ilivyo huko duniani. Ningepeda kuijibu hoja hii ambayo kwangu naiona inao udhaifu kwa njia moja au nyingine. Jibu: Serikali yenye mifumo yake dhabiti na weledi katika kusimamia shughuli zake za kiutendaji kwa wananchi si lazima kuiga na kuwa wafuasi wa kila kitu kinachofanywa na majirani zetu au na mataifa mengine.

Serikali kupitia kwa rais JPM baada ya COVID-19 kuingia nchini ilitangaza kutofunga mipaka wala kuingiza nchi kwenye utaratibu wa “lockdown” kama wengi walivyoshauri, Ushauri wao ulikuwa na tija lakini serikali kupitia kwa watendaji wake wakasimama na msimamo wa kuendelea na shughuli za uzalishaji mali kwa kigezo kikubwa cha kuchukua hatua muhimu za kiafya kama wataalamu wetu walivyoshauri, Uamuzi wa serikali kutoweka zuio lolote ni matokeo ya weledi wa serikali wa kuie;ewa vema jamii ya kitanzania ina maisha gani hasa katika eneo la uchumi na uzalishaji mali, Wapo walioona uamuzi huu ni wa ajabu na upuuzi Fulani, bahati mbaya kikundi kilichokuwa mstari wa mbele kuinanga serikali dhidi ya uamuzi huu ni kikundi cha SHIBE/ Wenye nacho ambao hata nchi ingeingia lockdown mwaka mzima kwao isingekuwa taabu isipokuwa kwa wanyonge tu ndo wangekipata cha moto. Aidha serikali haipaswi kuiga kila kitu kinachofanywa na mataifa mengine, natumia fursa hii kuipa serikali hatua na misimamo iliyoichukua kupambana na COVID-19 dhidi ya Watanzania.

Utumwa wa fikra ni mawazo ni mbaya sana Tanzania tusiwe sehemu ya utumwa huo, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi wamechukua hatua zinazofaa dhidi ya watu wake, Tanzania pia tumechukua pia kwa watu wetu zenye manufaa na tija kwa kwa maisha yao ya kila siku.

Pili, Wapo wanaojenga hoja kuwa Rais amejificha Chato, hoja hii ni mfu na haina mashiko nchi inaweza kuongozwa na rais akiwa eneo lolote lile la nchi, Pengine wanao jenga hoja wamesahau kuwa hata Mwl. Nyerere enzi za utawala wake aliwai kuongoza nchi akiwa nyumbani kwake Butihama, Fidel Castrol amefanya hivyo kwahiyo naomba hili lisiwe nongwa na isigeuzwe kuwa agenda ya kisiasa.

Tujenge hoja na kuleta mikakati ya kupambana na COVID-19 badala ya kuibua hoja zisizo na tija kwa watanzania, Wanasiasa tuache kutafuta umaarufu usio na tija kwa kipindi hiki bali tuonyeshe mshikamano wa dhati ili tuweze kuvuka salama salimini dhidi ya janga hili linalotukabiri.
 
1)walainza kulilia lock down wakashindwa.
2)wakaanza kusambaza uongo hali ni mbaya watu wanaanguka hovyo kwa corona wakashindwa.
3)wakaanza kulilia idadi ya ya takwimu za wagonjwa wakashindwa.
4)sasa hivi wanasambaza mipaka kufungwa watanzania haturuhusiwa kuvuka mipaka,mara tena watanzania wamekutwa na corona malawi,uganda,sijui kenya wanasahau wamesambaza habari za mipaka kufungwa.
5)washaacha ya corona wameanza mada zao za wabunge wao waliorudi bungeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Wapo wanaojenga hoja kuwa Rais amejificha Chato... wamesahau kuwa hata Mwl. Nyerere enzi za utawala wake aliwai kuongoza nchi akiwa nyumbani kwake Butihama
Duh, pamoja na kutofahamu hiyo Butihama iko sayari gani, hebu tutajie ni lini na katika mazingira gani Mwl Nyerere aliwahi kuongoza nchi akiwa Butihama! Pia tutajie ni shughuli gani hizo alizozifanya akiwa Butihama na kama aliwahi kuwaapisha mawaziri akiwa Butihama!
 
Hilo la kukaa Chato Wala lisikupe shida. Kuna kipindi JPM alikuwa ikulu mda mrefu wakasema anaogopa kuondoka atapinduliwa. Wabongo achana nao
 
Back
Top Bottom