comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,950
Wana jamii
Salaam
Ni muda muafaka sasa kwa serikali itoe tamko kali kwa wanasiasa wasiingilie maamuzi ya watendaji wataalamu , muingiliano wa siasa katika taaluma za watendaji kunasababisha wataalamu watendaji kushindwa kutumia utaalamu wao katika ngazi za maamuzi na utekelezaji, vilevile kusita kutoa ushirikiano wa maamuzi ya kitaalamu na kubakia na utaalamu wao kichwani, Aidha, kusita huko kutoa ushirikiano wa kitaalumu kunachangia shughuli nyingi zinazohusu utaalamu kulegalega, kuchelewa,au kutotekelezeka kabisa kwa kuhofia maamuzi ya siasa, maeneo ya kitaalamu yanayopaswa yasiingiliwe na siasa katika ngazi za mijadala hadi maamuzi ni Afya, Masuala ya taaluma ya fedha, uhasibu na uhandisi, Elimu, Ardhi- Wanyamapori na Utalii hususani Mipaka katika mapori ya Hifadhi, tafiti mbalimbali za kisayansi, Kilimo, Mifugo, Maji, Madini na Nishati, Aidha, kama siasa haitaingilia taaluma na utaalamu mambo yanaweza kuwa hivi-: upande wa migogoro ya mipaka kati ya wananchi na maeneo yaliotengwa kisheria migogoro haitatokea kabisa kwani wataalamu watakua wametekeleza wajibu kwa vitendo, ipasavyo, Elimu- sera ya elimu haitayumba au kubadilika badilika kila mara kwani wataalamu wasomi na wabobezi watakua wameweka sera zinazoendana na mazingira, urithi, utamaduni na mabadiliko ya sayansi duniani, Afya- wataalamu wetu wangewekeza zaidi katika tafiti na matokeo ya tafiti na tahadhari za mara kwa mara kama kuna viashiria vya magonjwa hatari kama wanavyofanya kituo cha utafiti wa magonjwa Marekani, Ardhi- matumizi bora na sahihi ya maeneo ya ardhi hivyo kuondoa migogoro vilevile siasa zisiingie katika kutoa maamuzi ya endapo mifugo itaingizwa katika Hifadhi hivyo wataaluma kutoa maamuzi yao katika kutekeleza kazi zao, Mifugo -wataalamu wa mifugo na ardhi wangeshauri na kutekeleza kwa vitendo ni jinsi gani ya kuondoa tatizo la migogoro kati ya wakulima na wafugaji, Madini-wataalamu wangeweza kabisa kutoa tathimini ya athari za uchimbaji na uchafuzi wa mazingira na matumizi sahihi ili kuepusha migogoro kati ya wawekezaji wachimbaji na wananchi, Uhandisi -wataalamu wangetekeleza wanayoona inafaa baada ya kufanya tathmini na makadirio ya kihandisi katika miradi yoyote.