Serikali inasomesha wanafunzi vyuo vikuu ili wajiajiri?

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Jana kupitia ukurasa wa Naibu waziri wa afya,jinsia,wazee na watoto, ndugu HAMIS Kingwala alisema,(angalia Picha).
67197c52e791d082a06c6eea9792fbe3.jpg

ed0ae130317e29718a6704ffb2a408ae.jpg
.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter kama inavosomeka hapo juu. Naibu huyo wa waziri wa afya anataka au anawaomba wahitimu wa vyuo vikuu nchini waweze kujiajiri. Ikumbukwe serikali imewagharimia wanafunzi hawa kwa millions of shillings wakati wa masomo yao, vyuoni. Nitatoa mifano michache: Medical Doctor aliyesoma St. Francis university of health sciences automatically kima cha chini anachotakiwa kurejesha bodi ya mkopo(heslb) siyo chini ya 26millions,nursing officer(NO) aliyesoma Bugando anatakiwa kurejesha sio chini ya 23millions heslb,Mfamasia aliyesoma Bugando anatakiwa kurejesha sio chini ya 24millions(mkopo kutoka heslb),mwalimu wa masomo ya Sanaa sio chini ya 16 million.
Maswali yangu ni haya:
1. Kuna serikali yoyote ile hapa duniani inasomesha wanafunzi kwa gharama kubwa ili wajiajiri na waweze kurejesha mikopo waliyokopeshwa na serikali?
2. Kama serikali inasomesha wanafunzi wa vyuo vikuu kwa gharama kubwa,je hizi pesa wataweza kuzirejesha kama ambavyo wangekuwa wamejiriwa serikalini au kwenye mashirika binafsi?
3. Je serikali itapata wapi tena pesa za kusomesha wanafunzi wengine maana hakuna marejesho yatakayofanywa na mhitimu wa chuo kikuu ambaye kajiajiri na anapata japo 20000/ kwa siku?

4. Kwa hali hii ya kutowaajiri watu ambao muliwasomesha kwa gharama kubwa mnategemea baadae watakuwa wadaiwa wa namna gani maana hawatakuwa wadaiwa sugu tena Bali wadaiwa wenye magamba yaani ambao hawatalipa na haitatokea wapate uwezo wa kurejesha pesa hizo heslb?
NB: Walionufaika na mkopo wa elimu ya juu ni watoto wa masikini japo hata watoto wa mawaziri walinufaika.

Yapi maoni ya wahitimu baada ya serikali kusisitiza wajiajiri badala ya kutegemea ajira za serikali?!!!
1. "Tulipohitimu elimu ya juu tulitegemea kuajiriwa na serikali ili tuweze kurejesha kwa wakati pesa tulizokopeshwa na bodi ya mikopo(heslb) ila serikali ilisema itaajiri sio Leo au kesho,hii hali tumeizoea cha msingi sisi tumepata elimu mambo ya marejesho ya pesa za mkopo hazituhusu tena serikali itajua namna ya kuzipa pengo hilo ambalo lingetokana na marejesho ya pesa zetu za marejesho heslb,madam tunapata chochote kitu haina haja na ajira zao" alisema muhitimu mmoja ambaye ni mtoto wa fukara aliyezaliwa kwa makusudi ila akapata mkopo wa bodi ya mkopo na kuhitimu shahada yake ya biashara na hana mpango na ajira za serikal.
2. " Hakuna kitu ambacho nakifurahia kama serikali kutokutoa ajira zetu maana imenipunguzia stress za makato kwenye mishahara kama vike PAYE,BIMA,Mifuko ya jamii na makolokocho lundo" hii ilikuwa ni kauli ya mwalimu(mhitimu wa masomo ya sanaa)ambaye kwa sasa anafanya kazi ya u kondakta wa mabasi ya mikoani kuelekea dar. Kijana huyu alidai kila route Moja ya to and from anapata siyo ya 140000 na chenji kidogo hali inayomfanya aendeshe maisha yake bila shaka yoyote.
3. Naendelea na mahojiano na baadhi ya wahitimu wa elimu ya juu ili kupata mawazo au maoni yao juu ya ajira za serikali.(nitarejea).

Maoni yangu.!!!!!!
1. Serikali kama imedhamiria kutowaajiri vijana ambao walitumia pesa nyingi za walipa kodi kusomea fani zao na serikali haitaki kuwaajiri kwa kufanya zoezi la uhakiki wa vyeti lisiwe na mwisho. Basi HESLB mwafaaaaaa!!!!! Heslb mtatoa wapi pesa ambazo huwa zinatokana na marejesho kutoka kwa wanufaika mkopo?.
2. Serikali ijiandae kisaikolojia namna ya kupata pesa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu miaka mitatu au zaidi ijayo.

Mwisho kabisa nakaribisha maoni mbalimbali ya watimu wa stashahada,astashahada,shahada juu ya tatizo la ajira nchini.
Karibuni tujadili pamoja.

NB: "Hakuna taifa linasomesha wanafunzi wa elimu ya juu ili wakajiajiri".
Ni mimi Rais wenu
Rais wa mioyo ya watu
Rais atakayefanya muishi kama malaika 2020
 
Tatizo sio kumaliza chuo, mkuu..
Hii elimu tuliorithishwa na warithishwaji, ndio inayotufanya tuwe watumwa kifikra.

Elimu gani ya kipuuzi hii mtu anasoma tangu darasa la kwanza hadi anafaulu kidato cha nne (11 years), na almost miaka yote hiyo amekuwa akijifunza kiingereza kama somo la lazima, lakini bado hata kuandika barua ya kiingereza bila makosa ya kisafuri hawezi..!
Kukiongea ndio kabisa, hadi vyuoni ni shida, mbaya zaidi hadi mheshimiwa nae anazidiwa na Diamond Platnumz..(hapo nimecheka kidogo tu! ili nisionekane mchochezi sana).

Hii elimu huku kwetu imebeba mambo mengi ya kinadharia, lakini wenye hii elimu kwako ni halisi kabisa, na wao ndio wanaoifaidi zaidi. Huku kwetu soma sana, usipoajiriwa ndio basi tena.

(NB;I've told you this in majority)
 
Nakuwadhalilisha kuwaandika kwenye magazeti eti wadaiwa sugu wa bodi....hivi hata wanajua inachukua muda gani mtu kujiajiri mpaka kuanza kuingiza kipato? Wawaulize waliofanikiwa how long it took them to get there
 
Back
Top Bottom