SERIKALI inaipindua NCHI KIJESHI.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SERIKALI inaipindua NCHI KIJESHI..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eng. Y. Bihagaze, Jun 30, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  jesh 2.jpg jeshi1.jpg

  Wakati mzimu hatari wa mgongano wa ki- utu na maslahi kati ya serikali na madaktari ukiwa kwenye wakati wa joto kali ukifanyika kwenye shingo tepetevu ya raia asiye na hatia yoyote, mapambano yakiendelea kwa ari na kasi zaidi kiasi cha kutekana na kushambuliana kihasimu, kimaudhi na kiuzembe zaidi, Duru za wachunguzi wa kimtazamo zinavuja kwamba haya
  YANATOA TAFSIRI KWAMBA SERIKALI INAIPINDUA NCHI KIJESHI.

  Katika tafsiri nyepesi ya kawaida JESHI ni Kikundi cha watu waliojiunga ili kukamilisha kusudio maalum. Kwenye jamii ya watu wanaoikalia dunia wanatafsiri kwamba jeshi ni kikundi cha watu –wenye zana zinazoweza kuleta maangamizi kwa mwanadamu-waliojiunga kwa kusudio maalum. Na hapo ndipo tunayakuta majeshi mawilii ambayo yote yana lengo moja kumlinda au kumdhuru raia. Jeshi Lenye silaha za moto na Jeshi lenye silaha za madawa(madaktari na fani nzima ya uuguzi).

  Nachelea kuweka Petroli kwenye Moto unaowaka lakini pia sitaki kuwa mzembe wa kuweka mtazamo wa wazi wa hiki kinachoendelea. Kama raia wa kawaida Tunaamini Madaktari ni binaadam ambao wanabeba vichwa vinavyofikiri lakini pia serikali ina watu wanaofikiri on this basis hakuna mwenye hoja nyepesi hapa, kila mmoja ana hoja nzito na hoja yake lazima ifikie makamo stahilivu. Nataka niseme bila kulegeza semi, HILI NI JANGA LA KITAIFA..

  Unapotembelea baadhi ya Hospitali zetu, watoto wanavyoteketea kwa kukosa matibabu, wagonjwa wanavyohangaika kujipanga ili wajitibu, wananchi wanavyotafuta wataalam wa mitishamba kama tiba mbadala na huku wanapata madhara mengi zaidi, sasa hata wauza maduka ya dawa wamegeuka madaktari kwenye vitengo vyao ili wanufaike na sakata hili kwa kuwatibu wagonjwa kinyume na fani inavyotaka, na hapo haitoshi jibini la majadiliano linatiwa doa kwa kumshambulia kiini wa majadiliano Dr. Ulimboka, na hali kuwa tete zaidi kwetu wananchi maskini ya mungu sisi tusiojua lolote..Ni tafsiri gani ya maneno utayaweka hapa kama sio JANGA la kitaifa?


  Nirudi Duruni, Serikali inaipindua nchi kijeshi, serikali ikiwa ni kikundi kidogo sana cha watu waliokasmiwa dhamana ya uongozi wa nchi, na nchi ikiwa ndio umati wa raia wenyewe wenye nchi.
  Serikali ikiwa ni pamoja na Rais na vyombo vyote vya ulinzi na usalama, Bunge, Baraza la mawaziri, watumishi wa serikali wakiwemo na madaktari wenyewe, ambao wamekuwa kwenye mzozo, migongano na kero kwa Muda sasa. Huku Nchi, yaani sisi raia tukiwa watazamaji na waathirika wakuu wa kadhia hii. Kumekuwa na kero kati ya wabunge na posho zao, wizi wa wanyamapori, maandamano ya kupinga muungano, Vurugu za Zanzibar, Mauaji ya walemavu wa ngozi, ujambazi na ujangili uliokithiri, wizi wa waziwazi na ufisadi wa kutisha ambayo yote haya hayajapatiwa majibu toshelezi kwa raia, lakini mwananchi mtanzania ametulia tuli kama mjinga vile, sasa chokochoko hii imefikia hatua ambayo haiwezi KUVUMILIKA, inapogusa eneo la uhai wa raia..TIBA.

  Kuifatakua kadhia hii, tunajua wazi jeshi la kwanza yaani Vyombo vyote vya ulinzi na usalama ikiwemo Polisi, magereza, jeshi la wananchi nk, wana uwezo wa kuua kwa makusudi au bahati mbaya na jamii ikafichwa taarifa lakini vile vile Jeshi linalotumia madawa yani madaktari na Wauguzi nao pia wana uwezo huo huo wa kuua kwa bahati mbaya au makusudi na jamii sisi wananchi tukafichwa. Sasa inapofikia mishale jeshi mojawapo kati ya haya linapoanza kuua raia kwa makusudi, WAZIWAZI na Serikali Ikiwepo
  HAYA NI MAPINDUZI MAKUBWA.

  Madaktari wanapogoma kutoa tiba, ni tafsiri ya wazi kwamba wameamua kuua raia. Na kwa Kuwa Kuna Viongozi waliokasmiwa madaraka kuhakikisha hili lisitokee, ama kwa uzembe wao, ama kwa kushindwa kuongoza vema, ama kwa makusudi yao tu na chuki zao kwetu sisi raia maskini tusio na mtetezi wameamua kuruhusu janga hili litokee, hatuoni sababu ya ushawishi ya wao kuendelea kuhodhi madaraka hayo.
  WATOKE HARAKA SANA KABLA HALI HAIJAWA MBAYA ZAIDI.

  Wananchi hatuwajibiki kujua kiini cha tatizo –HAISAIDII, nani anaongoza vuguvugu hili-HAISAIDII, Ugomvi wa kimaslahi na kimapato hata kama serikali itatuelezea kiini cha ugonvi huu hadi mtondogoo haitasaidia lolote ilihali madhara ya kadhia hii yakiendelea kuwepo na kuleta balaa kila sekunde inayoondoka, tunachojua serikali ingekeketa mbivu na mbovu kwa uwezo ilionao na kuidhibiti hali hii isitokee.. kwa hiyo hatuzuiliki kabisa kuamini kwamba sasa
  VIONGOZI WETU UWEZO WAO WA UONGOZI NA KIFIKRA UMEKOMEA HAPO, TAFADHALI WAJIUZULU KUPISHA KADA NYINGINE YA SAFU YA WATUMISHI NAO WASHIKE USUKANI WA UONGOZI WA NCHI HII.

  Mweshimiwa Rais, Hivi kweli Unapata hamu ya Kula, Kulala, Na Kuburudika na Familia Yako Ilihali kuna watu ndani ya nchi yako Unayoiongoza wanateketea kwa kukosa Huduma muhimu kabisa ya kijamii ambayo ni TIBA!!.. unalala na Kuamka kabisaa.. Moyo wako Uko mweupe kabisaa. Aise haya kwanini yasiwe maajabu ya Nchi.. Mwenyezi Mungu amekupa Uwezo wa Kutamka neno kudhibiti hali hii lakini Umewaachia watoto huku wanavunjana mbavu na kutengeneza propaganda za kipumbavu kila mchao na kuzunguka kwenye vyombo vya habari kupika majungu, uchonganishi na Fitna na wewe upo kimya ukiangalia Mchezo huu unavyokwenda? Juzi Mganga mkuu wa Serikali na Timu ya watu watatu wamening'inia TBC wakisambaza umbea na chuki kwa watanzania. Unapoiambia jamii kwamba Daktari nayeanza ajira analipwa mshahara wa laki nane na nusu wakati MhandisiAnayeanza kazi analipwa laki nne, huu ni uchonganishi wa chuki. Kwamba sasa serikali inataka sisi wahandisi tuwachukie Madakrati kwa sababu kwanini wao wanapendelewa na serikali na bado hawatosheki wanataka serikali iwapendelee zaidi? Wakati shule yao ni Ngumu pia Shule ya Uhandisi ni Ngumu vilevile, Top brain Layers za Hesabu huenda Uhandisi na Top brain Layers za bailojia huenda kwenye fani ya matibabu, kwa hiyo mnataka wahandisi na kada nyingine waingie kwenye ugomvi na madaktari? Hii ni akili kweli au matope? Mtu ananing'inia kabisa kwenye TV ya kitaifa anamwaga Majungu haya.. na Bado yupo kwenye kiti anaendelea kula bata.. watu wanakufa huku.. huu si moyo wa uzalendo hata kidogo.. tumewakosea nini.. mtunyime matibabu na kutuchonganisha pia?

  Viongozi wengine wa serikali wako kukusaidia wewe kutuongoza sisi, sasa tunapoona viongozi hao uliowaweka wewe wakusaidie kutuongoza sisi leo wanagombana na madhara tunaathirika sisi, na wewe uko kimywa hutaki kumuwajibisha yeyote ni tafsiri gani sisi raia maskini ya Mungu Tunaipata? Tukisema Umewatuma Watutendee Hivi Utasema Tunakosea mweshimiwa?


  Ni baba gani asiye na uwezo wa kuadabisha familia yake mbele ya jamii??. Kwamba kuna mahakama ya Kazi, kwamba kuna kosa la kinidhamu mambo yote hayo hayasaidii baba Riz, Tunachotaka ni Huduma kwa jamii ziwepo na ziendelee.. Ila pia elewa kwamba sisi sote ni binaadam, tunatofautiana kifikra na kiuongozi, kama Mwenyezi Mungu hakukujaalia kipaji cha kuongoza matukio kama haya ya binaadam ni vema ama Ukakubali kizalendo kwamba Uongozi wa hili kibinaadam siuwezi, unang'atuka na mwingine anaendelea naye akishindwa vilevile anang'atuka. Au wajibisha uliowakasmia madaraka husika haraka ili kunusuru balaa zaidi ambalo sasa hasira ya mwananchi ikishaiva haitadhibitika.

  Kumwongoza binaadam ni Kazi Ngumu.


  Wanajeshi wana Umoja wa kitaifa ila madaktari wana umoja wa Kimataifa. Tunakoelekea sasa watu hawa kila mmoja kwa nafasi yake ataanza kutumia nafasi yake kumdhuru mwenzie kwa siri. Hata kama mtu atakimbilia Kutibiwa Nchi za nje, Madaktari watasema huyu ndiye yule kiongozi anayetoka kwenye nchi wanayodhalilisha fani yetu, watamtengeneza wanavyotaka kwa sababu uwezo huo wanao, watampeleka kwenye "Mabwepande" za kikwao..

  Amka kwenye kiti Mheshimiwa, wajibika kwenye Hili sakata sasa. INATOSHA.

   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  baba dhaifu hana maalaka na hata amri zake hazifuatwi kwa kuwa yeye ni dhaifu
   
 3. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,553
  Likes Received: 16,520
  Trophy Points: 280
  Maandiko yako yanatia simanzi!:A S cry:
   
 4. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  dah!...so sad!
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Serikali dhaifu, Liwalo na liwe. Tujielekeze zaidi 2015, wako watakaolimbikwa, wako watakao pona, elimu ya uraia hasa katika makanisa na misikiti ni muhimu. Huu ni wakati wa kukomesha mambo ya kinafiki. Serikali yetu ni legelege, na imeshindwa kuamua jambo kama hili. Hebu linganisha kipato cha Ana Makinda na Daktari. Leo bajeti ya Rwanda inalingana na bajeti ya Tanzania, tunachojua ni Ndiooooooo. Hovyo kabisa.

  Dhaifu
   
 6. m

  mamajack JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Baba ataanzia wapi???pote akigusa panamchoma.poleni watanzania.halafu kuna kitu kinaniuzi sana.kunamijitu haitumii akiri eti kila anyesimama na kukemea maovu anaonekana ni chadema.hapa sio itikadi za chama ni hali halisi ya taifa.
   
 7. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Liwalo na Liwe!
   
 8. y

  yaya JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tears on my eyes.
  Oh good Lord, please have mercy on this perishing nation.
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Sijui kama Baba Mwanaasha atakusikia umeeleza mambo ya msingi ya kulinusuru taifa letu lakini kwa sababu tuna Raisi Kiziwi tukubali kuangamia na kupotea kabisa kwenye uso wa dunia
   
 10. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 11. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumefika hapa kwa sababu ya UDHAIFU wa Rais wetu. Tujiandae kuwa wakimbizi ndani ya nchi yetu. Wanajeshi karibia wote wamebakia kuwa watii kwa Shimbo pekee yake ambaye ndiye anawalipa hela, lakini naye wanahasira naye maana anawakata fedha bila sababu. Then, kwa sasa jeshi liko tayari kuipindua serikali, haliko tayari kudhalilishwa. "Mimi nakwambia rafiki yangu, sisi tumesubiri hatua fulani ifikiwe, tunaiondoa madarakani nchi hii kwa nguvu za jeshi, huyu bwana (Rais) anakumbatia watu wachache tu, sisi huku tuko hoi kabisa na familia zetu, hafiki 2015 nakueleza mimi, Kambini kwetu alipata kura 2 tu, hana jeshi huyo, utii kwake mwisho" ni maneno ya Rafiki yangu, ambaye ni Askari jeshi.
   
 12. D

  DR. RICHARD Senior Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  No comments!! its the plain truth that any critical person can't deny
   
 13. D

  Determine JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  liwalo na liwe
   
 14. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Natoa machozi kwa huu uziii ni busara ambazo jk angezipata hata robo tusingekuwa hapa.
   
 15. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Utu wa mtu na wa Taifa ukifilisika, kinachobakia ni ombwe la uongozi!

  Kama hakuna Utu utatumia nini kuongoza na Kutatulia MATATIZO ya Jamii? Lazima itabidi kutumia INTIMIDATION and TOUCHERING!!

  Kwa mfano!

  1. Ili kufikia Utatuzi wa tatizo la mgomo wa Ma Dr na secta ya afya? Mkamate Dr mmoja mpeleke Mabwe pande Mtoe Meno mawili na kucha ishirini ... Hii itachukuliwa kama njia bora ya Utatuzi wa tatizo la afya. Lakini huu Si Unyama? Na huu si ushaidi kuwa Utu umefiklisika kwa serakali iliyoko madarakani kuchukua hatua kama hiyo?

  Vema tuendelee ... kwa kuwa kutoa meno mawili na kucha ishiri ...kumetatua tatizo la sector ya afya.. Tatizo la umeme lita tatuliwaje?

  2. Tatizo la umeme ... ongeza dozi ya kile kilichofanyika kwenye tatizo la afya. Sasa badala ya kutoa meno na kucha ongeza na kukata mkono mzima mtu akiwa hai ... Kwa kuwa Utu haupo tena ... hii itaonekana kufanya kazi na kutatua tatizo ... Na majibu mema yatapatikana ...Lakini huu ni Unyama si Utu tena. Lakini Tanzania imeasisiwa katika misngi ya UTU na sasa utu unatokomea na UNYAMA unashika hatamu... kama umeweza kuanza na mtu mmoja ... si lazima utaendela?

  3. Tatizo la waalimu kugoma. Hili Litatuliweje kwenye mfumo huu mpya? ...Ongeza dose ya Utatuzi namba 2. Sasa badala ya kumtumia mtu mmoja tumia watu kumi ...fanya kama namba 2. ..Jibu litapatikana...na Utu unapotea na unyama unashika hatamu. Tatizo la waalimu litauwa limepata Utatuzi kwa watu kumi kupelekwa Mbwe pande ... na kungolewa meno, macho, kucha na kukatwa mikono na miguu!! Kwani si UTU uepotea na Unyama umeshika hatamu?

  4. Tatizo la kupanada kwa bei ya BIDHAA MUHIMU litatauliwaje? Kwenye mfumo huu mpya ambao unaigia kwa kasi? JIBU... Ua waanchi 100 hadi 500... Kwa kuwa KU UA sasa ndio njia muafaka ya Kutatulia matatizo ya Mtanzania. Huu ni unyama kama Ule wa serengeti wa Mnyama kumua mnyama kwa ajili ya kutatulia tatizo la nja! Lakini Kwa Wanyama Kuua ni sahihi. Kwa mwanadamu kuuua kama njia ya kupatia utatuzi si sahihi.

  Kwa kuutupa Utu wa mtu katika kutatulia matatizo yake ... KIFO kinakuwa ndio jibu enedelevu la kutatulia matatizo ya jamii na kupata maendeleo ya taifa.

  ANGALIZO...

  Viongozi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wajue fika kuwa ..UTU.. Unauwezo wa Kuzima Mabomu yote ya Nuklia duniani yasifanye kazi.

  Watambue kuwa NGUVU YA UTU WA MTU ... si doli ..lakuchezea huko Mabwe pande ...

  Watambue kuwa Hawatakuwa na mahali pa kukimbilia ..Pale nguvu hiyo Itakapokuwa tayari IMEWIVA NA KUKOMAA NA KUVUNWA KWA MATUMIZI YA TAIFA LA TANZANIA.

  NINI CHA KUFANYA ...

  Utu wa mtu uheshimiwe na utumike kama Msingi wa utatuzi wa matatizo ya Mtanzania.

  Ole wake huyo atakaye leta na kuendeleza Mzaha juu ya Dhana hii ya UTU WA MTANZANIA ambao ndio UTANZANIA WENYEWE!!

  Bora ahame hii sayari akaishi sayari nyingine!!!!!!
   
 16. mutabilwa

  mutabilwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakika kaka umeandika uzii mzuri na kwa Mwelewa wala haiitaji tafsiri.....uzi uko wazi.
  MIMI NINA KITU WANA JF NIMEKIFIKILI KUWA KUNA USEMI USEMAO "IF YOU FIGHT WITH THE NATURE THE NATURE WILL KILLS YOU" Nina maana hii kuwa sasa taifa kama nature limeshabadilika na linatambua kila kitu kinachoendelea hivyo basi si wakati tena wa watawala kutumia mbinu zilezile za zamani kutawala make watakuwa wanashindana na taifa (nature) ambalo kwa sasa halitaki mbinu zilezile.please viongozi badilikeni make watu walishawachoka na mkiendelea hivi mtaishia kubaya!!!!!111
   
 17. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  ..

  Formula hizi nadhani zemebuniwa, zimejengwa Na sasa kuanza kutumika rasmi.. Kama maaskari wamefunga ndoa ya kidumu Na Majambazi, jambazi akiua mtanzania hapatikani ila jangili akiua faru faster keshatiwa sheriani. Sasa hapo tukisema majambazi ni Hao Hao maaskari Na maaskari ni Hao Hao majambazi nani atatuziba vinywa?

  Kama mahesabu yako hivi, Basi neno nchi ya Kidemokrasia liondolewe kwenye hizo Hansard za nchi Na litungwe neno jingine
   
 18. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Naamini akifanya ziara ya maksudi kutembelea hospital hizi atalia.. I am sure
   
 19. Xidian

  Xidian JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Nimesoma na kuumia sana, hivi kweli tz ina President?
  Nashindwa Kuamini kama kweli yupo au lah
   
 20. TAMKO

  TAMKO JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  ..
  ..
  Naskia Yupo.. Sasa sina uhakika kamili.. Naona tu kila kiongozi anajitendea anavyojiskia. Kuwa mtulivu ni jambo Jema sana Kwa Rais , ili kupima kila pepo kabla ya kung'oa conclusion.. Ila utulivu huku wananchi wanakufa sasa this is too much.. Akikurupuka kusema Ataongea Na maiti???!!!
   
Loading...