Serikali inachezea pesa zetu walipa kodi

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,863
5,694
Serikali hii ya awamu ya tano imekuja na kauli mbiu ya kulipa kodi na kubana matumizi yake. Lakini matumizi ya serikali hii ni mabaya kabisa na yanakatisha tamaa sisi walipa kodi.

Hebu fikiri kulikuwa na haja gani kwa polisi kujaza mafuta magari yao kibao na kuzurula tuu mitaani kuzuia mahafali ya Amani ya wanachadema vyuoni, huku mahospilini hakuna dawa, madawati hakuna huko mashuleni, barabara mbovu, huko Mbeya watu wanatumia kamba kuvuka mto.

Halafu watu wakishauri wafujaji wa pesa za umma washitakiwe mnasema ni wachochezi. Kwa hali hii hakuna maendeleo ya haraka tutayapata.
 
Bila kutupa maelezo ya LUGUMI, bila kutueleza hatima ya mchakato wa Katiba siwezi kuwaelewa kwamba hawatumii pesa zetu vibaya. Kivuko cha Bagamoyo kiko wapi? Barabara zinajengwa kiwango duni hazidumu wakati tunaendelea kulipia madeni ya barabara za gharama kubwa. Katiba imeteketeza mabilioni ya pesa kuanzia kwenye tume hadi bunge maalum la katiba, kwa kuendekeza siasa mufilisi, imeachwa hewani kana kwamba hakuna kilichotokea.
 
Back
Top Bottom