Serikali imepanua wigo wa uwezeshaji

Serikali imepanua wigo wa uwezeshaji

jaba jumah

Senior Member
Joined
Sep 24, 2015
Posts
150
Reaction score
50
Maeneo Maalumu ya Uwekezaji:

(i) Mikoa 20 imetenga Maeneo Maalumu ya Uwekezaji ili yawekewe miundombinu ya msingi itakayovutia Sekta Binafsi kujenga viwanda na kufanya biashara katika maeneo hayo; na

(ii) Sheria za Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZ) na Maeneo Maalumu ya Uchumi (SEZ) zimepitiwa ambapo vivutio mbalimbali ikiwa ni pamoja na nafuu ya kodi vimebainishwa ili kuhamasisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika uwekezaji.

(h) Benki ya Rasilimali imeanzisha Dirisha Maalumu kwa ajili ya kuwezesha wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kupata mikopo kwa riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa viwanda;

(i) Jumla ya makampuni 130 yamewekeza mitaji yenye thamani ya Shilingi bilioni 2,041.6 mwaka 2014 ukilinganisha na Shilingi bilioni 126.6 mwaka 2010 na kutengeneza ajira za moja kwa moja zilizotokana na uwekezaji huo kufikia 31,923; na

(j) Ekari 107 zimepimwa katika Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuanzisha Vijiji vya Viwanda (Industrial Villages) na kupata hati miliki (Title Deeds) ili kuanzisha viwanda vya kusindika na kutengeneza bidhaa za ngozi.

(k) Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI): Katika kipindi cha mwaka 2010-2013, jumla ya mikopo 56,517 yenye thamani ya Shilingi bilioni 30.6 imetolewa na kuwezesha upatikanaji wa ajira zipatazo 113,876 kupitia Mfuko wa Kuendeleza Wafanyabiashara Wadogo (NEDF).

#KijanaWakatiNiWako
#HapaKaziTu
 
Back
Top Bottom