Barakaeli174
Senior Member
- Aug 2, 2015
- 171
- 142
Wana jf sikatai serikali kuhamasisha wananchi kuchangia maendeleo yao katika sekta tajwa, ila naona kama habari inayohusu ukusanyaji mapato na kupita kiwango si sahihi maana serikali ni kama inahitaji wananchi kuchangia kwa sehem kubwa, au kutategeshewa ajali ili zipatikane pesa za rambirambi zitakazo saidia au zitakazo pelekwa kwenye secta hizo kwa ajili ya maendeleo, sasa pamoja na kuingiza siasa kwenye maswala ya kijamii je iyo siasa imekuwa msaada kwa wananchi, na je iyo siasa baada ya kuonekana kuwasumbua wengine na kuwafanyia visivyo mnafikiri wananchi wengi walio athirika na siasa chafu watakuwa na muitikio wa kuchangia. Makamu wa rais amewasili zanzibar na imekuwa hivi
"' Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Unguja – Zanzibar akitokea mkoani Dodoma ambapo hapo kesho anatarajiwa kuzindua ya kampeni maalum inayojulikana kama Mimi na Wewe mjini Unguja.
Lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha jamii kuchangia kwa hali na mali katika uboreshaji wa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, afya, mazingira na kusaidia watu wasiojiweza katika Mkoa wa Mjini Magharibu, Unguja.
Katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Serikali na wa Vyama vya siasa.
Source: Habari leo