MAGAMBA MATATU
JF-Expert Member
- Jul 2, 2011
- 646
- 1,187
Serikali ina vyanzo vingi vya mapato,,, baada ya Serikali za magharibi kutuondolea misaada Sasa njia sahihi ya kuongeza ukusanyaji kodi ni hii hapa
Kuna maduka mengi sana ya biashara kuanzia majiji makuu hadi miji ya kawaida,,
Serikali ifanyeje??
inatakiwa igawe mashine za EFD kwa kila mwenyekiti wa mtaa hadi kijiji ili kila anayepanga chumba ama nyumba ya kulala ama fremu ya biashara basi mwenye nyumba, chumba ama fremu ya biashara akatwe 10% ya bei iliyolipwa kama kodi ya mapato ya nyumba na hapo serikali itakusanya makusanyo kwa mwaka zaidi ya misaada tunayopewa,,,
Cha kufanya ni kutunga sheria yake ili mpangaji anapotaka kulipia pango lazima apewe risiti ya EFD ambapo pesa inaingia moja kwa moja serikalini,,,
Na inatakiwa kila baada ya miezi mitatu TRA inapitia nyumba mpaka nyumba kwa kukagua mikataba na risiti iliyolipwa kati ya mpangaji na mpangishaji na hapo hakuna mwenye nyumba atakayeshindwa kufanya hivyo.
Na sheria ielekeze kabla mpangaji hajaishi hapo alipopanga basi malipo yafanyike katika ofisi za serikali za mtaa na hapo ndo atapewa risiti Ila akikubali kupangishwa bila kupewa risiti ina maana atakua amevunja sheria na adhabu yake iainishwe maana amehusika kumlinda mwenye nyumba asilipe kodi ya upangishaji na hiyo risiti yake aitunze mpaka mkataba wake utakapoisha,,
Hivyo hivyo kwa mwenye nyumba apate kopi ya hiyo risiti ya mpangaji wake na yeye maafisa wa TRA wakibaini hajalipa kodi ya upangishaji nyumba yake basi atakua amevunja sheria na adhabu yake iainishwe.
Kiujumla tunakuomba Mh Rais wetu kuna vyanzo vingi vya mapato kama hivi na ukiamua basi miaka mitano ijayo tutaanza kutoa misaada.
Mfano. Nyumba inapangishwa 50,000 na 10% ya kodi ya upangishaji ni 5,000 mtu anakua ana nyumba vyumba vitano kwa mwezi 25,000 mara nyumba 500000=12.5b kwa mkoa mmoja kama Dar.
12.5b mara wastani wa mikoa 25 =312. 5b kwa mwezi
312.5*12=3.7Tilions kwa mwaka
Hii ni hesabu ya bei ya kawaida ya chumba na siyo kwa nyumba kubwa maana kuna nyumba na fremu zinapangishwa 200,000-1,000,000 kwa mwezi.
So naomba Rais wangu tujipange na hatimaye tutajenga Taifa huru na Dunia itatuheshimu