Serikali ifanye haya kutokomeza mimba za utotoni. Kuwafunga watu miaka 30 siyo suluhisho

Mi nimeipenda sana iko poa njia hii maana hata akifungwa miaka 30bado atapewa mimba tena na mtu mwingne,mi ningeshauli ulieleta huu uzi moja kw moja 2020 chukua form ugombeee ubunge kwenye jimbo lako ss wanajf tutakueezesha baba.
Asante Kwa ushauri mkuu nitaufanyia kazi Tuombe Fadhila za Mungu.
 
Hongera sana .
 
sasa unashauri selikali ifanye nn maana wanagawa kondomu bure na uwasherati unaanza school
 
Vitoto vingine havina bikra toka vikiwa na miaka 10,sasa kama hana bikra aulizwe alidondoshea wapi? - weakness ya sheria.
Kuwafunga miaka 30 sio sawa kabisa na kuwaacha sio haki. nimpe mwanaomimba alafu unifunge sikuiyoiyo naiomba mahakama imlee mtoto kwa kipindi chote ntachokua gerezani. -
bunge likipitisha sheria hii muingie mahakamani mkiwa na bia mbili mbili
 
kwenye madhara ya watia mimba kufungwa miaka 30 jela,naunga mkono 100% lakin kwenye suluhisho,kuna hoja zina ukakasi,hasa namba 3 & 4,hizo haziwezekani,inasemekana mtoto wa kike anaweza kupoteza bikra kwa njia nyingi ukiacha sexual intercourse hlo litaleta utata sana,pregnant test haitosaidia;hzo mimba watazitoa kabla ya muda wa test yenyewe na hii nchi kama unavyojua ni ya magumashi,magumashi yatafanyika mara uhaba wa vifaa mara ufisadi wa fedha nk itaishia pasipojulikana kama zoezi la katiba mpya au zoezi la vitambulisho vya taifa.
 
kiu yangu kubwa ilikuwa kutaka kujua nini wafanywe wanaume waliowatia mimba wanafunzi,ila hujagusia na kulipa uzito kama heading yako inavyosomeka,je waachwe tuu? au kuna chochote unaweza suggest? mwisho mkuu acha nikuswalike,nini maana ya bikira? is it physical or psychological?
 
na wengine msaidie,bikra ni ngozi nyepes iliyopo kwenye uke?(still unaambiwa wengine huzaliwa hawana ),je ni hali ya kuwa hujashawahi kushiriki tendo la kujamiiana? hizi mimi zinanichanganya na zitaleta ugumu kuitafsiri endapo mswada wa mleta uzi utataka kupitishwa.haha bikra z phenomenon.
 
Kipengele cha 3 hakina ulazima kabisa maana kinakiuka haki za binadamu.Kupima bikra ni uzalilishaji,upimaji unatokea pale inapotokea kuna ulazima kwamba binti amebakwa.So hakiwezi tekelezeka. Bikra huweza kuondoka bila kujamiana na mwanaume. Asante mtoa uzi!
 
Kwa mazingira ya sasa hata sheria iwe kali vipi, lazima mimba zitapiga hodi tu.
Kuwabana wanaume si kazi rahisi maana hata kuwekwa sheria ya kufungwa miaka 30 kwa kubaka, iligonga mwamba.

Wazazi na walezi kulea vyema na kuwakumbusha watoto mambo haya ya uzazi na madhara yake ndio njia imara iliyobaki.
 
Mtoto kazaliwa halafu mnamfunga baba yake miaka 30? Mnakuwa na huruma kwa binti aliyebeba mimba lakini hakuna huruma kwa mtoto anayezaliwa ambaye kimsingi hana kosa lolote. Miaka 30 mnaifahamu au mlikurupuka? Nani atamlea mtoto huyo? Pili kama binti anarudi masomoni baada ya kujifungua, kosa la aliyempa mimba linakuwaje, yaani na uzito gani? Leo mnifahamishe, hivi kumbe kubeba mimba si kosa, kosa ni kuweka mimba? Je, wakipeana mimba watoto wa umri mdogo, wa kike na kiume inakuwaje????
 

Kati ya yote uliyopendekeza namba 2 ndio suluhisho. Halafu kupima bikra aiendani na issue ya kupewa mimba. Halafu under 18 bado ni watoto. Unaonaje ukapima bikra ya wa kwako kama unaye badala ya kuipa mzigo serikali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…