Serikali ibebe mzigo wa madeni yasiyolipika ya benki za biashara!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,793
Kubadilika kwa sera kwa ghafla kumesababisha benki nyingi kupata hasara na kuwa na bad debts kiasi cha kuzifanya taasisi hizo zipunguze uwezo wake wa kutoa mikopo au kupunguza shughuli hizo ili ku manage risks...
Kwa kuwa serikali imechangia kwa kiasi kikubwa kwa kuyumba kwa taasisi za fedha, serikali iwajibikke kuzikopesha fedha bila riba taasisi za fedha na deni hilo lilipwe ndani ya miaka kumi... Fedha hizo ziwe hadi asilimia hamsini ya bad debts za benki husika.
Hii itasaidia kusisimua uchumi na kuzikwamua benki zilizo katika kipindi kigumu...
 
Mabenki mengi yalikuwa hayafuati taratibu za kukopesha.

Tatizo la mikopo alijaanza kwenye utawala wa hawamu ya tano. Barclays Bank walipa tatizo utawala iliopita kwa sababu ya mikopo.

Watanzania wanachukulia mkopo kama ku-win lottery! Hatukopi kwa madhumuni ya kulipa.

Mfano, Europe mabenki mengi yanapenda kuwashawishi customers wake kuchukua mikopo midogo midogo ambayo ni unsecured. Mzungu hata ukimshawishi vipi kama ana plan nao hachukui lakini Mtanzania akienda Benki kwa shughuli zake nyingine halafu wakamshawishi hapo hapo kuchukua mkopo wala hatafikiri mara mbili. Anaona kama siku hiyo ameamka na bahati!
 
Kubadilika kwa sera kwa ghafla kumesababisha benki nyingi kupata hasara na kuwa na bad debts kiasi cha kuzifanya taasisi hizo zipunguze uwezo wake wa kutoa mikopo au kupunguza shughuli hizo ili ku manage risks...
Kwa kuwa serikali imechangia kwa kiasi kikubwa kwa kuyumba kwa taasisi za fedha, serikali iwajibikke kuzikopesha fedha bila riba taasisi za fedha na deni hilo lilipwe ndani ya miaka kumi... Fedha hizo ziwe hadi asilimia hamsini ya bad debts za benki husika.
Hii itasaidia kusisimua uchumi na kuzikwamua benki zilizo katika kipindi kigumu...
Acha hizo benki zife tu.Zingine zilikuwa zinatoa mikopo bila ya kufuata masharti halafu unataka pesa yetu ikawabebe
 
Back
Top Bottom