Serikali iangalie mfumo wa upangaji kodi wa TRA kunusuru biashara

kenethedmund

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
347
89
Naomba kabla ya yote nimpongeze Mh. rais kwa kazi kubwa yakuhakikisha serikali inakusanya kodi ili kuweza kuleta maendeleo katika taifa. Na ni wajibu kwa mwananchi yeyote kulipa kodi hili linaumuhimu mkubwa sana katika taifa. Nikirejea kwenye kauli ya rais aliyoitoa hivi karibuni kwamba ni bora kuwa na meli moja inayoingia bandarini kuliko kuwa na meli 60 ambazo hazilipi kodi zinashusha mizigo bure, kwenye hili hata mimi nakubaliane nae.

swali linakuja je kodi wanazotoza TRA na mamlaka zingine za serikali ni rafiki kwa uchumi wa taifa letu ?,

Tusisubiri mpaka ufike wakati inakuja meli moja, lazima tuangalie kodi wanazotozwa wafanyabiashara zinalipika na je ni wezeshi yani ukiweka gharama ya kodi pamoja na gharama zingine huyu mfanyabiashara ataweza kumudu kupata faida na kukuza mtaji wa biashara hasa ukizingatia idadi kubwa ya wananchi bado wanategemea kuajiriwa na serikali pamoja na sekta binafsi.

Mwisho wa siku bidhaa ikimfikia mtumiaji ataweza nunua?

Kwanini nasema haya, tunataka wananchi waondokane na tabia yakutaka kusubiri ajira kutoka serikalini na sekta binafsi, yani wafikirie kujiajiri lakini bado hapo hapo kuna vikwazo vimewekwa ambavyo vinamyima huyu mwananchi kufikia hayo malengo.

Mfano mtu anapotaka kuanza biashara analazimika kufika TRA ambapo kule atakadiriwa, alafu baada ya kukadiriwa ni lazima alipe kwanza kodi ya kota ya kwanza ndio aweze kwenda jiji/halmashauri nakupatiwa leseni ya biashara.

Mfano wa pili ni ule wa mfanyabiashara ambaye alikadiriwa kodi ya kiasi cha 320,000/=Tsh kwa biashara ya stationery kwa mwaka jana, mwaka huu wa 2017 huyu huyu mfanyabiashara anaenda TRA anaambiwa malipo ya eneo biashara yake ilipo anapotaka kufungua ni kiasi cha 800,000/=Tsh kwa mwaka.

Hili ni ongezeko la kodi la zaidi ya 100%, sasa huyu mfanyabiashara atawezaje kukuza mtaji na hapo hapo kuendelea kuwa mlipa kodi mzuri wa taifa.

Mfano wa tatu ni ule wa EFD, ambapo mfanyabiashara analazimika kununua kifaa hicho, kwa gharama zake huku waliopewa mamlaka yakuuza mashine hizo wanataka walipwe fedha zao cash pasipo kutoa kwa mkopo.

Kwa yote haya mfanyabiashara huyu ataweza kweli kufikiria kujiajiri au atabaki na zana yakusubiri kuajiriwa. Ndio maana nasisitiza kuna umuhimu mkubwa wa mamlaka za mapato Tanzania kufanya tathmini mpya ya viwango vya kodi vilivyopo na utaratibu mpya ili viwe rafiki, vikiwa hivyo ninahakika tutakuwa na taifa ambalo litakuwa na walipa kodi wengi zaidi na pia itasaidia kutatua tatizo la ajira. Ni vyema mashine kama za EFD wakawa tra wanasambaza wao na sio kutumia wafanyabiashara wafanye hili zoezi. Hili litasaidia kwa kila mfanyabiashara kuwa na hii mashine.

Nawakilisha
 
Msilalamike sana. Kaeni kimya. Kodi zikikata akili zitawarudi.

Ukikombizana na kichaa aliyechukua nguo zako ukiwa bafuni, wanaowatazama hushindwa tenganisha nani sio kichaa.
 
Nakubaliana na wewe mkuu, mfumo wa kodi uko hovyo kabisa kwa sababu hawaangalii gharama nyingine kwa mfano kodi ya chumba cha biashara na gharama za umeme , Wao wanatamka tu unatakiwa ulipe kiasi fulani
 
Back
Top Bottom