Serikali iache kubebana

Serikali iache kubebana

Wilderness Voice

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
921
Reaction score
1,651
Ati kumefanyika uteuzi wa baraza la mawaziri. Ningekuwa Rais. Waziri kashindwa kuleta tija katika muda alokaa katika wizara ni kumuondoa na kuweka mtu mwingine. Tanzania ina wabunge 300 na kitu lakini bado kuna Watanzania millioni 60.

Ndo kusema hao mawaziri wenu ndo watu wenye uwezo pekee.

Mfano Jafo alioneshwa kushindwa mudaTamisemi Leo kapewa wizara nyingine. Huyu alopewa Tamisemi alishawahi kuwa Afya, kule kulimshinda. Watu wanaiba madawa, fedha zikaliwa. Wasiwasi wangu ataiweza Tamisemi? Shetani lililowashinda wengi. Ukisikia ufisadi wa hii nchi umejaa Tamisemi.

Kule kuna vurugu kila namna hata migogoro ya ardhi ni huko. Ok huyu waziri wa Fedha. Alisha kuwa hapo enzi za Kikwete, akiwa naibu, je kuna tija alofanya? Tuleteeni sura mpya zisizo na mazoea. Huenda wa kafanya makubwa.

Rais inafika sehemu anaongea kwa kuwaonea huruma mawaziri ati msiwe na wasiwasi nimewachukueni wote. Mhe Rais, usiwe na huruma ya mama. Upo kwa ajili ya watanzania. Waziri hawezi piga nje chukua mtu anae faa. Watanzania ni wengi.

Mwisho kwa style hii sijui. Matatizo ya Tanzania yataendelea kubaki yalivyo.
 
Bahati mbaya huyo Rais amepewa mamlaka na Katiba ya kumteua ampendaye! Hivyo kubali tu matokeo. Hakuna namna nyingine ya kufanya.
 
Andiko lako lina hoja ya msingi sana. Ila kwa sasa hatuna budi kukubali na kutii baraza lililoteuliwa na kiongozi wetu mkuu.

Jaffo kaonywa mara kibao, inamaanisha hafai kupewa wizara nyingine...Ummy hakuna chochote alichofanya kwenye afya zaid ya sifa walizompa kwenye corona ambazo inabidi moja kwa moja ziende kwa wataalamu wa afya by professional....
 
Mwanamke ni mwanamke tu.
Na mwanaume ni mwanaume tu.

Ngoja niishie hapo niendelee kuomboleza kifo Cha hayati jiwe.
 
Back
Top Bottom