SERIKALI HII IJIKITE KWNY MIRADI YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

kluger

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,071
2,000
Salamu na Heri ya sikukuu za Christmas na Mwaka mpya, 2017.

Naipongeza serikali chini ya uongozi wa mheshimiwa Rais wangu Bw. J.P.Magufuli kwa hatua mbali mbali za haraka na maendeleo, kwa kweli nampongeza sana Rais kwa hilo.

Binafsi nina mapendekezo huru kwa serikali hii ambayo ni sikivu na yenye nia njema kwa watu wa hali za chini kuhusu suala zima la KILIMO ambacho ndiyo UTI WA MGONGO kwa taifa hili. Mbali ya madini, misitu, gas, bahari na raslimali zote za nchi lakini bado kilimo, ndiyo chanzo kikuu cha mapato kwa asilimia kubwa ni kimaanisha kinagusa idadi kubwa ya watu wa vipato vya chini tena hasa huko vijijini.

Awamu iliyopita ilifanya jitihada zake kupitia mkakati mpango wa KILIMO KWANZA. Mambo mbali mbali hapa na sera ziliwekwa kuhusu kilimo.
Naishauri Awamu hii kuendeleza hatua zilizofikiwa hadi sasa.
Kwa mapendekezo yangu, paanzishwe MIRADI YA UMWAGILIAJI nchi nzima. Kilimo hapa nchini kwetu kimekuwa kikitegemea mvua ambazo hazitabiriki kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Hivyo basi ili kuwa na uhakika wa kilimo ambacho kinagusa walio wengi ni vyema serikali hii ikaelekeza matumizi mengi na hata makubwa kwny MIRADI ya UMWAGILIAJI /IRRIGATION SCHEMES nchi nzima.
Serikali igharimike kuchimba mabwawa makubwa kabisa WATER DAMS Kwa ajili ya kuvuna na kukusanya maji mengi. kipindi cha mvua.
Wabwawa haya yatatusaidia kufanya kilimo cha UMWAGILIAJI vile vile ufugaji wa samaki, jamani hili linawezekana kabisa, sina utaalamu katika mambo haya pengine niruhusu hoja mbadala katika hili kama kuna shida katika utekelezaji wake, mabonde ya mtu Rufiji, Ruvu na mingine mingi Kwa nini tusijenge mabwawa makubwa kabisa ambayo yatavuna maji ya mvua na kupunguza mafuriko ambayo yanawaua watu kila mwaka.

Nchi kama Sudan, tumesoma na kusikia Irrigation scheme huko Khartoum, hv kweli nchi hii akipata MIRADI ya namna hii Kwa kila mikoa minne mradi mmoja, bila shaka tutapunguza njaa na kuzalisha ajira Kwa watu wa chini Kwa kiasi kikubwa, sijawahi sikia mawaziri wasomi wa kilimo wakiongelea hili, kupitia uzi huu naomba nielimishwe kama mpango huu Kwa nini haujawahi fanyika au hata fikiriwa Kwa nchi yetu, je tatizo ni nni??

Ahsante,

Kwa kutambua hili
 

Mnyirani

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
886
500
Acha ujinga huko, magufuli anaamini wanyonge wanahitaji ndege kuliko matrekta au kusambaza maji,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom