Serikali haijafurahishwa na tukio hilo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali haijafurahishwa na tukio hilo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, May 9, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Written by Stonetown (Kiongozi) // 09/05/2011 // Habari // No comments

  [​IMG]
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeviagiza vyombo vya usalama Zanzibar kulishuhulikia ipasavyo suala la kuchomwa moto vibanda vya biashara katika fukwe za Pwani Mchangani na Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Agizo hilo lilitolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika katika maeneo hayo kuangalia hasara iliyopatikana na kuwapa pole waliopatwa na mkasa huo wa kuchomewa moto madanda yao ya biashara.
  Makamu wa Pili wa Rais kwa niaba yake na Serikali kwa ujumla alieleza kusikitishwa kwake kuhusu vitendo hivyo na kuahidi kuchukua hatua zinazofaa kuvikomesha kabla ya kuathiri jamii.
  Aliwataka wamiliki wa mabanda ya maduka hayo kutolihusisha suala hilo na ubaguzi baina ya Watanzania Bara na Visiwani kwa dhana ya kuwa wengi wao wanaasili ya Bara kwa kuwa wapo walioathirika ambao ni wazanzibari. Bali wajione kuwa ni Watanzania na wana haki ya kufanya biasharakamawenzao wanavyofanya kwao kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi.
  Kuhusiana na ombi la wananchi hao kutaka kupatiwa hifadhi ya muda Balozi Seif aliwapa pole kwa hasara walioipata na kuhusu pahali pa kujistiri kwa wakati huu, na kuwaahidi kwamba Serikali ya Mkoa itawapatia sehemu ya kulala kwa muda wakati serikali ikilishughulikia suala hilo.
  Kabla ya hapo katika risala yao waathirika hao waliiomba Serikali kuchukuwa hatua zinazofaa dhidi ya wanaohusika badala ya kuwaona mitaani wakitamba na pia kuomba wapatiwe mahali maalum pa kujenga maduka yao ili waishi kwa amani na kuendelea na biashara zao kama kawaida.
  Halikadhalika, katika shukrani zao zilizowasilishwa na mmoja wao James Chales zilimpongeza Makamu huyo wa Pili wa Rais na Serikali kwa ujumla kwa kufika kuwafariji na hatua wanazochukuwa juu ya kadhia hio hasa kwa ahadi ya kwamba jeshi la polisi kuchukua hatua za kuwasaka wanaohusika na tukio hilo na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
  Naye Charles Pendael Tito alisema wamekuwa wakiishi kwa khofu wakati huu kutokana na kuwa bado watu waliohusika wanaweza kuendelea vitendo hivyo wakati wowote na kuiomba serikali kulichukulia suala hilo kwa umakini kwani linaweza kujirudia tena iwapo serikali itasita kuwachukulia hatua madhubuti za kuwadhibiti wahalifu hao.
  Tito aliiomba serikali katika kipindi hiki kuwapatia makaazi mazuri ambayo yatakatoweza kuwasitiri pamoja na watu wawili ambao wameathirika kupatiwa matibabu na wakaazi wengine kuomba kupatiwa magodoro kwa kuwa hivi sasa wanaishi katika maisha ya khofu na yasio na uhakika.
  Akizungumza kwa njia ya simu mzee wa miaka 70 wa kijiji cha Pwani Mchangani Ame Haji Ame ameilaumu serikali ya wilaya ya kutokana na kupuuza madai ya wananchi ya muda mrefu ambapo wanalalamikia suala zima la kuwepo vitendo viovu vinavyofanywa na wafanyabiashara hizo alizoziita za kikahaba ambapo alisema vitendo hivyo vimekuwa vikishamiri kila kukicha.
  Alisema mbali ya vitendo hivyo kumekuwepo na uhalifu mkubwa na uharibifu wa mazingira yanayofanywa katika maeneo hayo na fukwe kwa wafanyabiashara hao kufanya vitendo vya biashara ya ngono waziwazi jambo ambalo limekuwa likiathiri jamii ya wananchi wa kijiji hicho ikiwa pamoja na mipira ya kondom kuzagaa na kuchezewa na watoto wadogo ambapo serikali ilishauriwa kukomesha vitendo hivyo lakini imekuwa ikisitasita kuchukua hatua.
  “Ndio wananchi wamekasirika kwa sababu kumekuwa kukifanyika vitendo viovu vya biashara ya ngono na hili tumelitamka muda mrefu kuiomba serikali yetu ya wilaya kuichukua hatua lakini serikali imeshindwa kuchukua hatua madhubuti kukomesha vitendo hivi, sasa huwezi kuwalaumu wananchi kwa sababu ndio wanaothirika na madhila haya na jamii inaendelea kuharibika” alisema Mzee huyo.
  Kamanda wa polisi mkoa wa kaskaskazini Unguja, Masoud Msellem Mtulya aliwaambia waandishi wa habari kwamba hadi sasa jeshi la polisi limewashikilia watu saba kuhusiana na tukio hilo na wakati wowote watapandishwa mahakamani kujibu shutuma hizo.
  Alisema jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi kuwatafuta wengine wanaohusika na tukio hilo huku akiwaomba wananchi kutoa mashirikiano na jeshi lake ili kuwakamata watu wanaowatilia wasiwasi kuhusika na tukio hilo huku msako mkali ukiendelea ili kuhakikisha tukio kama hilo halitokei tena katika mkoa huo.
  Akizungumzia chanzo kinachozungumzwa na wananchi wa mkoa wa kaskazini Kamanda Mtulya alisema baadhi ya wananchi wanadai kulalamikia vitendo vinavyofanywa na wafanyabiashara hizo za vinyago na mama ntilie ukiwemo kuuza madawa ya kulevya, kuuza na uvuta bangi pamoja na biashara ya umalaya katika maeneo hayo ya fukwe na wanafanya biashara maeneo bila ya vibali vya kisheria katika maeneo hayo.
  Aidha alisema upande wa walalamikaji waliochomewa moto mabanda yao Kamanda Mtulya alisema wanadai kwamba wamechomewa biashara zao kwa kuwa wao ni watu kutoka Tanzania bara na wananchi wa hapo wamechoshwa na watu hao kuwavamia katika maeneo ya wananchi kwa kufuata biashara za kitalii.
  Kamanda Mtulya alisema madai yote hayo hayana ukweli kwa kuwa maeneo yanayoendesha uhalifu sio hayo pekee katika mkoa wa kaskazini lakini pia suala la kufukuzwa watu wa Tanzania bara halina ukweli kwa kuwa wapo walioathirika katika kuchomewa moto ambayo ni wazanzibari ingawa watu wa Tanzania bara ni wengi katika tukio hilo.
  Hata hivyo Kamanda Mtulya alisema suala hilo bado wanalichukulia kama ni la kihalifu na hawawezi kuliwacha likamalizika hivi hivi lakini jeshi la polisi litawakamata wale wote wanaohusika na kuwafikisha katika vyombo vya kisheria ili iwe funzo kwa wengine wenye kufanya vitendo kama hivyo.
  Kiasi cha watu 40 wamechomewa mabanda ya maduka yao juzi ambapo mabanda 43 yalichomwa katika ufukwe wa Pwani Mchangani karibu na Hoteli ya Waikiki na 30 yalichomwa Kiwengwa karibu na Hoteli ya Ocean Beach Resort.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CCM ndio wa kulaumiwa kwa kuashiria Ubaguzi wakati wa Uchaguzi 2010

  Sasa Wa Visiwani wanaona sio vibaya kuwashambulia wa bara walioko huko Visiwani

  Tusuburi Rais Wa Muungano atasemaje ???
   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Business as usual, atachekacheka tu!
   
 4. MAYOO

  MAYOO JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Poleni sana Wabara wenzangu, sijui itakuwaje siku kivumbi kikianza huku?! Wapemba watafanyaje, isije ikawa mkuki kwa nguruwe ....... Mungu ibariki Tz
   
 5. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Wapemba wanahusika vipi na tukio hili lililotokea Pwani Mchangani, Mkoa wa Kaskazini Unguja?

  Tena mmeshupalia sana ugomvi na kuuhusisha na mambo ya Muungano, mna hakika mnakisia tu?
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  May 9, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Kwa vyanzo vya habari kama (clip ITV), na hii iliyotoka mzalendo.net nashawishika kuamini tukio limetokea kama lilivyoripotiwa.
  Nawapa pole wote waliofikwa na janga hili lisilo la asili bali la kupangwa na wanadamu.

  Tukio hilo linahusishwa na watu wa Tanzania bara kutakiwa kuondoka visiwani ili muungano uvunjike. Viongozi wanasema hili ni tukio la kihalifu na lisihusishwe na ubaguzi(xenophobia)
  Ninapenda kuona watu wakiishi kwa utengamano licha ya tofuti za kijamii, imani au tamaduni. Naamini kuwa kwa watu walioishi pamoja kwa miaka 47 njia muafaka ya kutafuta suluhu ya tatizo ipo mezani. Siamini hata siku moja katika vurugu kwa kujua ni hatua dhaifu na ya kinyonge katika kufikia suluhisho la jambo lolote.

  Sipendi kuchukua upande katika sakata hili, hata hivyo nalazimika kuuweka ukweli kama unavyojulikana.
  Hapa JF wapo wazanzibar ambao siku zote wamekuwa wakitoa tuhuma kuwa uhalifu na umalaya visiwani umeletwa na wabara n.k.

  Tukio hili kama alivyoeleza huyo mwanakijiji linahusiana na tuhuma hizo na ni wazi kuwa jambo hili limechochewa na wznz na hao vijana wamefanya kazi kutimiza kile walichokidhamiria siku nyingi.
  Ukitembelea mzalendo.net jambo hili limeungwa mkono na hata kutaka wanasheria wawekwe ili kuwasaidia wahalifu kwa sababu walichokifanya ni kwa maslahi ya znz. Huko mzalendo wanahoji uhalali wa Mtanganyika kupata ardhi Znz!!

  Tuhuma zinasema watu hao wanafanya umalaya na uhalifu ndio sababu ya kuchukuliwa sheria mkononi. Wabara hao ni wachache mno na swali la kujiuliza wanafanya umalaya na nani? kama ni mabinti wa kizanzibar kwanini wasichukue hatua za kudhibiti watoto wao? Kama wanafanya uhalifu ni upi huo tukijua wamasai siku zote ni walinzi, na kwanini wasitoe taarifa kwa vyombo husika? Eti wanafanya mapenzi hadharani! idadi yao ni chache sana na sijui kama wangeweza kwenda znz kwa ajili ya ngono tu. Lakini mbona Waitaliano wanapofanya mapenzi ya wazi kule beach, je hiyo ni sawa na kwanini hoteli walizofikia zisichomwe moto. Kwamba kusambaa kwa kondom kunaletwa na wabara, sio waitaliano, Waganda, Wakenya n.k bali Wabara!!!!

  Wznz wanataka ulimwengu uamini kuwa wao hawatumii kondom na kila inayoonekana imeletwa na mbara. Wanataka tuamini wao hawana uhalifu na magereza yaliyopo ni kwa ajili ya watu wa bara. Takwimu zinaonyesha znz ina kiwango cha maambukizi ya maradhi ya ukimwi sawa na nchi nyingine. Haiingii akilini kuamini kuwa wao ni waumini wazuri kiasi cha kudhani tendo la ngono ni tukio geni katika maisha yao.
  Huko znz wapo watoto wasio na baba, na wapo wznz wanaozaa nje ya ndoa huku bara kama ilivyo sehemu yoyote duniani. Ni znz huko huko kuna mashoga waliobobea, hilo hawalioni wanaona malaya toka bara.
  Na wanatumia vigezo gani kujua malaya wa bara na si kutoka Lamu, mombasa au Comoro?
  Je si kweli kuwa hii ni 'prejudice' iliyojengwa dhidi ya Wabara.

  Pengine kwa kuogopa 'back lash' dhidi ya malaki ya wznz waishio bara ndio maana serikali inataka tuamini hili ni tukio la kihalifu na si ubaguzi kama ule wa South Africa(xenophobia). Ni mpaka atakapotokea wa kunishawishi vinginevyo ni ngumu kuamini hii si 'xenophobia'.
  Ni znz ambako wakazi wake wanajivumia chanzo cha ustaarabu 'civilization' hapa EA, sasa sijui huu ndio ustaraabu wanaojivunia !

  Zipo njia nyingi za wazi na zisizo na fujo za kuvunja muungano, tumependekeza mzitumie lakini inaonekana njia iliyo vichwani mwenu ambayo wana JF wznz wamekuwa wakiisema '' subirini mtaona, mambo yanaandaliwa' ni kuchoma moto. Mtakataa vipi kwamba hili si lenu wakati mumechoma waraka hadharani na badala ya kulaani mnajivumnia uhalifu, sasa hawa wanakijiji wafanye nini kama wasomi wameweza kuchoma nyaraka hadharani.
  Sijui na siombi wabara wakaamua kulipa kisasi, mungu pishilia mbali ! amin.

  Nawasihi ndugu zangu wa bara kufikiria ukaazi wao visiwani, na kuepuka kulipa kisasi kwasbabu ni lazima iwepo tofauti kati ya mstaarabu na asiye. Nanyi wznz manoshangilia uhalifu huu jitazameni, angalie leo na kesho na mjiulize je ni vema kurusha mawe ukiwa unaishi kwenye nyumba ya vioo!
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Tusiwape nguvu watu ambao wanafikiri matumizi ya vichwa ni kubebea vitu vizito na sio kufikiria.Tanzania ni ya watanzania wote...huku kubaguana ni matokeo ya kufikiri kudogo kwa baadhi ya watu ambao mara nyingi wanaamini matatizo yanayowazunguka yanaweza kumalizika kwa kuwafukizia mbali watu wasio wa eneo hilo....kama mambo yangekuwa marahisi hivyo mbona Dunia ingekuwa pouwa sana
   
 8. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Likitokea hilo sidhani kama ndugu zao wenye kuamini kile kitabu kitukufu kama watakuwa nanyi kwa hilo
   
Loading...