Serikali, fanyeni hivi kwenye sukari

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
7,266
9,964
Badala ya kulalamika na kukejeli tunatakiwa kusaidia kimawazo kusaidia viwanda vyetu lakini vilevile kukuza uchumi na biashara ya nchi yetu. Haya ni mambo ambayo serikali inatakiwa kufanya kwenye hili la sukari

1. Ruhusu uingizaji wa sukari kwa kipendi cha mwaka mmoja wakati mikakati ma maandalizi ya viwanda vyetu na uzalishaji vinaendelea

2. Saidia viwanda kuongeza uzalishaji hadi kuhakikisha wana uwezo wa kuzalisha sukari kwa mahitaji ya nchi nzima kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja

3. Jenga magodauni/shehena ya nafaka pamoja na sukari kwenye sehemu ambazo zilitengwa kwa viwanda mfano Bagamoyo

4. Fungua soko la jumla la Nafaka kwa kipindi hiki na bei ikiwa kubwa serikali inauza nafaka sio sukari pekee lakini bei ikiwa chini serikali inanunua. Hii inapunguza ufichaji wa nafaka maana hawatajua bei kama itapanda au itashuka

5. Serikali ihakikishe inasaidia uzalishaji wa kutosha wa malighafi miwa ya sukari ikiwa ni pamoja na kusaidia kwenye kilimo cha kisasa.
 
Serikali ni lazima ielewe huwezi kuzuia ufichaji wa nafaka kwasababu biashara ya nafaka ni biashara ya ufichaji au utabiriaji "speculation" na hata nchi za kibepari kuna kitu kinaitwa "Hedge" na inafanyika kwenye biashara ya dhahabu, mafuta na baidhaa zote ambazo sio "services" hivyo huwezi kuzuia hii biashara
 
Tatizo la sukari ni kubwa sana na sijui kama magufuli ataweza hili jipu sababu hii biashara imeshikwa na matycoon wakubwa wakiwemo wanasiasa wastaafu wa serikali iliyopita,viongozi walijimilikisha viwanda vya sukari kama kilombero ni vigumu kuwatumbua,if magufuli ana jeuri akamtumbue mstaafu wa kilombero sugar tuone.
 
Jana nilieleza vizuri kuna matatizo makuu mawili kwenye biashara ya sukari (1) gharama ya utengenezaji iko juu (2) Hakuna "commodity market". Na solution kwenye ufichaji ni Serikali kuwa na strategic storage za nafaka zote kubwa sukari, mahindi, mchele na maharage. Bei ikipanda sana serikali ina ongeza supply kwa kuuza kwa jumla kwenye soko na bei ikiwa chini serikali inajaza mashehena. Hii itaongeza risk kwa wafanyabiashara wanao vizia. Mashena wagenge kwenye hizo sehemu zilizotengwa kwa viwanda mfano kule bagamoyo ambako walitoa watu. Kwenye gharama za uzalishaji viwandani goverment ni lazima ihakikishe cost iko chini hasa ya umeme kwa kufunga mitambo ya gas kwenye hivyo viwanda.SerikMagufuli anasema serikali ina uwezo lakini tatizo ya pesa ya serikali sio uwezo bali ni matumizi ambayo yana make sense opportunity costali ijitoe kwenye biashara ya imports kwasababu hakuna strategic benefit kwa kutumia pesa kununua sukari ni unnecessary. Vilevile hiyo pesa ingeweza kufanya shughuli nyingine za maendeleo
 
Tatizo la sukari ni kubwa sana na sijui kama magufuli ataweza hili jipu sababu hii biashara imeshikwa na matycoon wakubwa wakiwemo wanasiasa wastaafu wa serikali iliyopita,viongozi walijimilikisha viwanda vya sukari kama kilombero ni vigumu kuwatumbua,if magufuli ana jeuri akamtumbue mstaafu wa kilombero sugar tuone.
Dawa zipo nyingi tu, ambayo inaongozwa na kanuni ya "demand and supply" basi, mambo mengine ni story tu, mzigo mwingi ukiingizwa hao akina Zakaria na Gulamali watanyoosha mikono juu.
 
Tatizo hamuelewi kuwa Serikali imezamilia kuwaokoa wenye viwanda na wakulima wa miwa. Cha msingi tuwasihi wanaoificha waitoe.. na wazo dogo la kijinga tupunguze matumiz ya sukari yasiyo ya lazima hadi mambo yatakavyo kaa vizuri.

Back
Top Bottom