SERIKALI/CMM vs UMMA/CHADEMA na Ibara ya 20 ya katiba

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
serikali inapoteza muda wake kutishia UMMA/CHADEMA.
Wassira amesema

"Ibara ya 20 ya kifungu cha Katiba inampa nafasi na haki kila mtu kukutana na yeyote na kutoa mawazo lakini si kutumia nguvu kufikia malengo ya kisiasa"

"Sawa leo wanasema wanaizungumzia Dowans, kwanza iko Mahakamani,halafu watakuwa na kipi kipya? kama huyo Slaa siku zote, kampeni zote ameimba Dowans, ufisadi kasema sana lakini watu wakampa kura Kikwete".

"Tunachotaka ni amani na umoja. Hii ya kusema nguvu ya umma inotaka wapi? Kama nguvu ya umma basi iko

CCM kwa sababu wamepiga kura watu milioni tano, CCM wakapata milioni tatu wao (CHADEMA0 milioni mbili, sasa nguvu ya umma ni nani hapa"

"Kuna sheria ya usalama wa taif, kutangaza kutaka kuiondoa serikali madarakani ni kuvunja sheria ya Usalama wa taifa, hapo dola haitavumilia"

"Hali ngumu ya maisha inatokana na mtandao mrefu. Hivi sasa mafuta yako juu, pipa moja linafika dola 150, sasa wanataka Rais Kikwete aende Uarabuni kusimamia kupanda bei za mafuta?."


Mbowe akajibu:

Wassira "hana ubavu wa kuzuia maandamano yake".


Maoni:

Hiyo Ibara ya 20 anayo ongelea Wassira, inafafanua matumizi ya "nguvu" ni yapi?
Kuandamana kwa amani ili matatizo ya wananchi yasikilizwe ni "matumizi ya nguvu"?

Kama Serikali ina amini uchaguzi uliopita ulidhiirisha nguvu ya umma ipo upande wake kwanini wasiache vitisho dhidi ya CHADEMA na kuanza kuelimisha jamii pamoja na kuonyesha kazi nzuri walioifanya mapaka sasa?
 
Back
Top Bottom