Serikali Bado inaongozwa na Rostam, Lowassa na JK

Wenzake wameroga weeeeeeeee sasa wanatajana uko, hana cha mganga wala nini subiri tu,dawa yake iko jikoni. Tanzanians are not stupids....this blood sucker ROSTAM wil see their wraths.
 
Hakuna cha mganga wala mjomba wake mganga, hela za Kagoda walizitumia wakuu wa CCM kurudisha nchi mikononi mwao na nyingine kujengea ma-kasri. Pinda hawezi chchote, kutokana naye kupewa u-PM ambao nao ni ulaji kwa hiyo atabakia anababaisha babaisha tu kuhusu Kagoda.

DECI aliingilia kwa sababu wafadhili walitaka hivyo kwani walikuwa wanashangaa vipi hawa wanaiachia kitu hiyo wakati kule kwao Marekani walimkamata mmoja hivi karibuni aliyekuwa anafanya kitu kama hicho na wakamtia pingu?

Deci yake ilianguka na kuchangia kuporomoka kwa masoko ya fedha kule, hivyo itakuwa haielweki JK anatembeza bakuli kule kwao huku kwake kuna Deci anayoikodolea macho!
 
Za mwizi ni arobaini hkuna cha mganga wala mganguzi. Wapo watu wanaiba na hirizi mdomoni hawakamatwi lakini siku zao zikifika huwa wanapigwa mpaka wanazitapika hizo hirizi zao. Arobaini za RA ziko njiani.
 
Si jambo la kushangaza kuwa wengine karibu wote wameguswa - kuanzia Mramba hadi Liyumba (angalau wamefika mahakamani) lakini Rostam Azizi ambaye ametajwa kwenye EPA, Kagoda, Dowans, na kwingine kote bado anadunda tu mtaani.

Ukichukulia mashitaka yaliyofunguliwa dhidi ya kina Mramba na kile ambacho serikali imekuwa inasema au kusita kusema kuhusu EPA, Kagoda na Dowans. Na pia ukichukulia PR inayoendeshwa sasa hivi kwa niaba ya Rostam Azizi kwa kutumia ofisi muhimu za serikali na CCM, si jambo la kushangaza kuwa Kikwete na Rostam bado wana nguvu yote ya kujaribu kudaganya uma wa watanzania kuwa serikali ya CCM inajisafisha (inapigana) na ufisadi.

Sio kwa sababu ya udini kama ambavyo baadhi ya watu hapa wamekuwa kwa muda sasa wakidai (kuwa ubaguzi wa kidini ulichangia sana kwa kilichotokea dhidi ya Mramba, Mgonja na Yona huku Rostam Azizi akipeta), Kikwete na Rostam ni marafiki wakubwa na ufisadi wote wa Rostam unamnufaisha Raisi Kikwete moja kwa moja.

Katika hili, wanaosubiria kumuona Rostam akichukuliwa sheria kwa uhusika wa moja kwa moja kwenye EPA, Kagoda na Dowans nk, wana muda mrefu sana wa kufanya hili.

Kikwete na Rostam Azizi ni pete na chanda - ufisadi wa Rostam Azizi ulimweka Kikwete ikulu na utaendelea kumweka madarakani huku pia ukimnufaisha Kikwete na familia yake binafsi kwa miaka mingi sana ijayo.

habari ndiyo hiyo.
 
Mhh ... Haikuchukua muda kwa hii kuunganishwa na nyingine. Kazi kweli kweli hapa JF.
 

Hapo nidpo huwa naona kumbe alkaeda si vichaa!
 

Mimi kwa jinsi ninavyomjua Rostam (kidogo) kwa kupima moves zake na matamshi yake naona ni mtu mwenye akili sanaa (evil genius). Akili zake zinaweza kulinganishwa na watu kama baba wa taifa (JKN) ila tu zake ni 'evil intelligence' au werevu wa kufanya maovu. He is the master power broker Africa or Tz has ever seen. Hata huko kuwa karibu na JK au Lowassa na kuwakamata sawasawa ni kwa sbb ya u-evil genius wake. Wanaodhani JK na Lowassa au CCM for that matter wanamtumia au wamekuwa wanamtumia kufanya ufisadi wanakosea. Yeye ndio anaowatumia wote hao bila wenyewe kujua. Mimi kama baadhi ya waafrika nina tendency za kishirikina (I believe there is witchcraft) na kwa hiyo I remain open to the fact that yule jamaa anaweza kuwa mshirikina wa kutupa, tena yeye mwenyewe anaweza kuwa ni sangoma (mchawi). Wairani na waarabu, hata wahindi ni washirikina kwelikweli, kwa hiyo sio ajabu kuwa jamaa alirithi matunguli.
 

This simple analysis, is somehow good and convincing. However, some variables' causality is elusive.
 

Kikwete ni fisadi, tena mkubwa kwa sasa kuliko wote. Ufisadi wake mkubwa ulianza katika mkataba wa Buzwagi, alioubariki usainiwe hotelini ng'ambo akiwa hukohuko. Rostam amekuwa akishusha makontena ya 'zawadi' nyumbani kwa kikwete Oystebay. Kikwete ni hatari kwa mustakabali wa CCM na nchi yetu. Asulibishwe mapema kabla hajaharibu zaidi. Yeye ndiye mzizi.
 
CCM na njaa Tanzania

CHEKI! Kufuatia kilio cha njaa kama kilivyoanza kuanguliwa na Bw. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bakuli la msaada litaanza kupitishwa ndani na nje ya nchi.

Kitakachotokea ni kwamba tutapewa chakula bure. CCM itafanya chake. Tenda ya ugawaji na uuzaji wake atapewa baniani au bulushi mmoja. Bilioni zitakazopatikana nyingi zitaliwa na jamaa hao na mabwana au watwana wao na bilioni chache ndio chama kitazichukua ili kujifaragua na uchaguzi mkuu wa 2010. Je, Slaa na kina Zitto mpo hapo. Mpo?
 

Hata kama ni kweli kuwa Rostam Aziz anatumia matunguli basi kumbuka kila bomu lina anti yake. Ni kiasi cha kujua timing tu.

Mawazo yangu yananiambia Anti-Rostam ni Dr. Slaa. Kama RA anatumia majini, basi Slaa anatumia nchi kavu. Tatizo ni kuwa:

1. Je Dr. Slaa atakubali kwenda kupambana na Matunguli ya RA na uchawi wa Bagamoyo?

2. Je Wananchi wa Tanzania tutakuwa tayari kumpa hiyo kazi ili akasafishe Ikulu na sehemu kibao kama Tanesco, Bandari, utalii nk?

3. Je mataifa ya nje yanayofaidikia na uzembe huu wa sasa wa Tanzania, watakuwa tayari kumuachia Slaa aendelee kuwanyanganya kitumbua mkononi?
 
Eti JK atamtosa Chenge! THUBUTU! Atasema kila kitu ! Na ndio maana wakamuwahi Salome mbatia wakamuua ili asiendelee kutoa siri kwa wapinzani kuhusiana na pesa za BOT, kwani yeye ndo alikuwa Mweka hazina mkuu wa chama wakati wa uchaguzi


Ehhh, hebu subiri Kidogo.

Asilia, Mtanzania, MJKK, FMes, mtu anaweza kunisaidia hiyo sehemu nimeweka BOLD? Eti walimuuwa ili asitoe siri? Nimekuwa nafuatilia hii topic ila nimekuwa naachwa Solemba. Nilisikia sereva wa roli lililomgonga kapotea. Sasa kumbe mambo yenyewe ni haya? Ufafanuzi zaidi naomba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…