Serikali Bado inaongozwa na Rostam, Lowassa na JK

Asilia

Member
Feb 18, 2008
24
4
Fukuto la fukuta, moshi wafoka, mapovu yanamwagika, CCM imefika njia panda! Ama isuke au inyoe!

Hili vurugu la Richmond, likizingirwa na BOT EPA, BOT CIS, BOT Minara, Rada, Kiwira, Buzwagi, TICS na moto kutoka Upinzani, unafanya mambo kadhaa tujiandee kutokea.

1. Wabunge ambao si mtandao, wenye uchungu wa kweli wa CCM, kuendelea kusulubisha viongozi wao na Serikali yao iwe wazi. Hawa wabunge, mwokozi wao na nguzo yao ni Wastaafu Malecela, Kawawa, Mwinyi, Salim na Msuya. Huku wako hawa walioshupalia RDC;-Mwakyembe, Kilango-Malecela, Seleli, Kimaro, n.k.

2. Team Mkapa; huku ni wale wajanja wa Che-Nkapa ambao bado wanatibu majeruhi ya mchakato wa kugombea Urais 2005 na kunyang'anywa tonge la Hatamu za Chama. Hapa kuna Mang'ula, Ngwilizi, Kigoda, Kinana, Warioba na Ruhinda. Katika kundi hili, pia wapo wale waliotajirika na mradi wa Ujasirimali Ikulu; Yona, Mramba, Mgonja, Mkono n.k.

3. Mtandao; Kundi hili lina majeruhi wengi kutokana na kuvunjwa kwa baraza la mwazirina mwegemeo wa kashfa za ufisadi kuwa kwenye shingo zao. Kundi hili, limegawanyika katika sura mbili;
1. Team Kikwete ambayo wamebakia Makamba, Chiligati, Membe, Migiro, Karume

2. Team Rostwassa(Rostam/Lowassa); Karamagi, Msabaha, Nchimbi, Apson, Meghji, Kamala, Masha Diallo, Chenge,
4. Wasiofungamana lakini wana nguvu na ni tishio; Pinda, Mwandosya, Sumaye, Balali, Salmin, Magufuli, Msekwa na Sitta.

Serikali mpya na baraza lake la mawaziri bado ni ya Kikwete Lowasa na Rostam.

Masha-Mambo ya ndani, bila Lowasa Bw. Mdogo Masha asingekuwa hapo alipo, ni lowasa aliyemshika mkono na kumwingiza kwenye siasa, kwani yeye Masha na Business partner wake Magai walikuwa private lawyers wa mamvi, na hata Magai aliwahi kupatiwa ujumbe wa bodi ndani ya city water wakati huo Lowasa ni waziri wa maji. Je unategemea Masha atasahau alikotoka kama JK asivyomtupa Hussein Mwinyi???? Hao polisi, Manumba na Magereza vyote viko chini ya Masha. Sasa je, nani atamkoma Nyani giradi????

Ngeleja-Nishati na Madini- Huyu alikuwa mwanasheria mkuu wa Vodacom Tanzania LTD ambako Rostam na lowasa wana hisa japo mamvi ni silent share holder. Ni Rostam aliyemshika mkono Ngeleja akagombee Sengerema na kumpatia fungu la kutosha ashinde. Na ndio maana ameachwa madini ili aendelee kulinda migodi ya Rostam. Hivyo tusitarajie mabadiliko makubwa.

Mkullo-fedha- Huyu akiwa mkurugenzi wa NPF sasa NSSF alichota mapesa kibao kumuunga mkono JK mwaka 1995, hivyo ni senior mwanamtandao. Na ndio maana Mkapa alipoingia madarakani akamtema NSSF.

Chenge- Miundombinu, JK hana namna, hampendi Chenge lakini anakuwa forced na Lowasa na Rostam. Mikataba yote kuanzia IPTL n.k imesainiwa wakati wa Chenge na yeye anaelewa nani ni nani katika hayo makampuni yanayozidi kuutafuna utajri wa taifa hili na kutuacha watanzania tukilalia chips kavu. Eti JK atamtosa Chenge! THUBUTU! Atasema kila kitu ! Na ndio maana wakamuwahi Salome mbatia wakamuua ili asiendelee kutoa siri kwa wapinzani kuhusiana na pesa za BOT, kwani yeye ndo alikuwa Mweka hazina mkuu wa chama wakati wa uchaguzi

Kutokana na kuwepo makundi haya makubwa na utata unaotambaa angani hasa baada ya Lowassa kuangushwa na minong'ono kuwa naye Lowassa ana ushahidi wa kujikosha, linalobakia kwetu watazamaji ni kupima upepo na kuomba dua wapigane na wagawanyike ili tujue nani ni kwa manufaa ya Taifa na nani ni mnyonyaji.

CCM si salama, na hata kama wakitoka nje ya ukumbi wakiwa wamekumbatiana, tusiwaamini.
 
Mkuu hii network ilivyo ina kujustfy heading yako. In maana tuko kule kule? Tuseme JK anatufix left right kiasi hiki huku akijua wazi anafanya nini? Tuendelee kuangalia nini kitatokea .
 
Hongera sana kwa anlysis nzuri!
Mimi nilisema mara baada ya cabinet mpya kutangazwa kwamba hakuna jipya. Kilichobaki ni kutetea haki zetu sis watanzania na kuzidi kuwaanika hawa mafisadi. Hivi sasa kuna juhudi za makusdi za kuzima ukweli wa EPA kufichuka!
Aluta continua..
 
Tunailaumu serikali kwa SPIN huku na sisi tunaandika headings ambazo zina dramatize issue huku ukweli ni tofautio kabisa?

Toa analysis yako na waachie wananchi tuamue wenyewe.
 
Tunailaumu serikali kwa SPIN huku na sisi tunaandika headings ambazo zina dramatize issue huku ukweli ni tofautio kabisa?

Toa analysis yako na waachie wananchi tuamue wenyewe.

Mtanzania, r u refering to me? Maana sijakuelewa. Maana the analysis I was refering to ni ya hapo juu na Asilia which I think includes some very good facts. Sasa unataka nini zaidi, there's no spinning hapa! Labda ulete wewe hoja!
 
Tumsaidie Jk nini cha kufanya,Nijuavyo mimi Barza la Mawaziri linapangwa na Kamati kuu na Rais huwa anenda pale na majina liyoshauriwa na CC.Rais lazima aweke watu anawajua na sio kuweka watu tu wasio na mawazo kama yeye.

tujenge Tanzania iliyo Moja,EL alishaachia ngazi.wamebaki watendaji kama kina Mgonja na Mrindoko ..na wengine wengi

suala lingine ambalo ni la msingi ni kwa wasomi wa chuo kwa kushupalia mambo huku ya kwao yamewashinda.Kuna tatizo la madarasa na vyumba vya malazi ni vichahce ila hatgujasikia wameandamana kwa ajili ya hayo.waache unafiki kwa kuanza kudeal na ishu za BUSH sababu they cant touch him coz ni utouchables.
 
Hata kama kivuli cha Lowasa na Rostam bado kipo ktk utawala uliopo madarakani lakini ule uhusika wao moja kwa moja katika mambo yaliyo na maslahi kwao umeondoshwa.

Hata kama aliwaazima akina Masha,Ngereja vyeo n.k walinde dili zake,kinachotazamwa sasa hivi ni utendaji wa kazi.

CCM Wagawanyike wasigawanyike shauri lao,tunahitaji kuona Taifa linaongozwa kwa mujibu wa katiba yetu ya Jamhuri wa Muungano,Wadanganyika wanapata haki zao za msingi.
 
Tumsaidie Jk nini cha kufanya,Nijuavyo mimi Barza la Mawaziri linapangwa na Kamati kuu na Rais huwa anenda pale na majina liyoshauriwa na CC.Rais lazima aweke watu anawajua na sio kuweka watu tu wasio na mawazo kama yeye.

tujenge Tanzania iliyo Moja,EL alishaachia ngazi.wamebaki watendaji kama kina Mgonja na Mrindoko ..na wengine wengi

suala lingine ambalo ni la msingi ni kwa wasomi wa chuo kwa kushupalia mambo huku ya kwao yamewashinda.Kuna tatizo la madarasa na vyumba vya malazi ni vichahce ila hatgujasikia wameandamana kwa ajili ya hayo.waache unafiki kwa kuanza kudeal na ishu za BUSH sababu they cant touch him coz ni utouchables.

Gembe, Baraza la Mawaziri la sasa halikupangwa na CC ya chama, I can reassure you of that! Hata Shein mwenyewe hakuhusishwa! EL kuachia ngazi ni just a facade, ni active sana in the background na ndiye aliyebariki uteuzi wa PInda - check the speech given by lowassa alipotangazwa Pinda also PInda aliconfirm kwamba ali'komazwa' na Lowassa, na kila kitu kajifundishwa na Lowassa.
Mfano wa Masha ni mzuri sana kwa sababu alikuwa kila wakati anadai kwamba yeye ni mshikaji wake EL and he will do anything to protect his buddy hata baada ya yeye (EL) kujiuzulu. Mara tunasikia kawa waziri!
Other sources pia wameconfirm kwamba Rostawassa wako very active hivi sasa wanapanga itakuwaje.
Shein amesaidia katika kupunguza wizara tu, lakini siyo majina.
Ushauri hamna haja ya kumpa JK kwa sababu hashauriki, kama kweli ameweza kumrudisha Chenge despite kusoma kelele zote kwenye magazeti dhidi yake huyu fisadi (wait a minute! Maybe JK doesn't read newspapers!) basi ni kwamba hataki ushauri.
Ilichobaki ni impeachment yake, au 2010 we make sure harudi tena na genge lake la mafisadi and we bid farewell to CCM as we know it!
 
Mini nadhani tuache kucheza mpira usiokuwa na magoli, kilichobaki tuanze kuchoma mali za mafisadi pindi tuu tutakapokutana nazo
 
Mini nadhani tuache kucheza mpira usiokuwa na magoli, kilichobaki tuanze kuchoma mali za mafisadi pindi tuu tutakapokutana nazo

Hiyo itakuwa ni anarchy na sisi tunataka civil disobedience. Ukitaka kujua tofauti jaribu kuangalia na kusoma kazi za Martin Luther King Jr na Mahatma gandhi kama mifano mizuri ya civil disobedience. Hii ya kuchoma moto siwezi kuunga mkono na nina uhakika wan JF walio wengi watakataa kuhusika katika anarchy!
 
Hiyo analysis yako inaonyesha kuwa Lowassa Rostam Kikwete si mtandao tena? duhh, unatuchanginyi.
 
Kwa nini tuchome mali ambazo zinaweza kulisaidia Taifa hili?

Nchi hii haijafikia kuwa KOSOVO ya kuharibu kila mali ya Fisadi.Kuna kanuni,taratibu na sheria za kuwafilisi mafisadi,na ndo maana ya Bunge ktk nchi.

Kwa mtindo huu tutachoma hadi makazi ya Mkapa kule kijijini kwake Lushoto.Sauti ya umma ina uwezo wa kuwanyang'anya kila walichokwiba.Voksi populi voksi dei
 
Mtanzania, r u refering to me? Maana sijakuelewa. Maana the analysis I was refering to ni ya hapo juu na Asilia which I think includes some very good facts. Sasa unataka nini zaidi, there's no spinning hapa! Labda ulete wewe hoja!

Susuviri,

Ungesoma kwa makini kidogo tu ungegundua namwongelea nani. Analysis na heading vimeandikwa na Asilia na wala sio wewe na ndio vitu viwili nilivyoongelea mimi.

Heading yake na analysis havifanani, hakuna fact mahali popote kuonyesha Lowassa au Rostam ndio wanaongoza nchi. Kama hana uhakika basi kwenye heading yake angeweka question mark na sio kama alivyoandika.
 
Gembe heshima yako for a good observation. Katika nchi yeyote ile duniani,jumuia ya wasomi ndiyo ambayo huleta mabadiliko makubwa ya kisiasa na uchumi mfano Iran. Hapa kwetu wasomi wa UDSM ndiyo wamekuwa wakituangusha na wanaunafiki wa kifisadi. Wakati wa uchaguzi,John Mnyika aligombea pale ubungo,tukategemea kura toka kwa wasomi wa UDSM wangembeba kijana huyu pengine leo angeleta changamoto kule bungeni akisaidiana na Zitto,UDSM wakamtosa, then wanakuja hapa JF na bwebwe za kulaumu serikali ya CCM na kuandaa makungamano yasiyoleta maendeleo yeyote,si ndiyo unafiki huu wa kifisadi. Kama unataka mabadiliko,lazima wapinzani wawe wengi bungeni hili tuweze kuibana serikali na ndiyo hapo tutapata majibu sahihi ya kashfa zote.
 
Gembe heshima yako for a good observation. Katika nchi yeyote ile duniani,jumuia ya wasomi ndiyo ambayo huleta mabadiliko makubwa ya kisiasa na uchumi mfano Iran. Hapa kwetu wasomi wa UDSM ndiyo wamekuwa wakituangusha na wanaunafiki wa kifisadi. Wakati wa uchaguzi,John Mnyika aligombea pale ubungo,tukategemea kura toka kwa wasomi wa UDSM wangembeba kijana huyu pengine leo angeleta changamoto kule bungeni akisaidiana na Zitto,UDSM wakamtosa, then wanakuja hapa JF na bwebwe za kulaumu serikali ya CCM na kuandaa makungamano yasiyoleta maendeleo yeyote,si ndiyo unafiki huu wa kifisadi. Kama unataka mabadiliko,lazima wapinzani wawe wengi bungeni hili tuweze kuibana serikali na ndiyo hapo tutapata majibu sahihi ya kashfa zote.

Je unakubali pia kuwa Mnyika alivyogombea Ubungo alikuwa na nia hii ya kuongeza namba ya wapinzani bungeni?
 
Nimeifurahia analysis hii ingawa sina uhakika kama ni ya kweli. Nilichofurahia hapa ni jinsi ilivyoonyesha namna gani serikali ya JK ilivyoundwa kwa kujuana zaidi kuliko sifa na uwezo wa mtu. Inaonyesha kuwa mawaziri wengi wako pale kutokana na kujuana na fulani kwa namna fulani tena ya kifisadi zaidi.

Sikupendelea heading iliyotumika kwa sababu inaonyesha kama vile ROSTAM na LOWASA wanashirikiana na JK kwa pamoja kutoa maamuzi ya serikali, jambo ambalo sidhani kama ni kweli.


On the other Note, je mama Migiro naye bado ni active kwenye politics za CCM au umempakazia tu?
 
Marekebisho,


1.
Serikali Bado inaongozwa na Rostam, Lowassa na JK

Serikali inaongozwa na rais na pinda, wakishinikizwa na wazee wa ccm, baada ya kikwete kukubali kushindwa, majina ya braza jipya la mawaziri kikwete huweka wake, na wazee wa ccm humpa yao, angekuwa anachagua yote peke yake, Nagu, Magufuli, Mkuchika, Pinda wasingekuwemo,

Chenge, anawekwa kwa dhana moja tu ya kumuogopa Shibuda, maana kufuatilia usawa wa mawaziri kwa mikoa, either achaguliwe Shibuda, au Chenge, shetani anyejulikana ni Chenge, Shibuda ni moto wa kuotea mbali!

2.[
B] Fukuto la fukuta, moshi wafoka, mapovu yanamwagika, CCM imefika njia panda! Ama isuke au inyoe![/B]

CCM is just fine, ni kikwete, lowassa, na rostam ndio hawajui hilo, but they will learn very soon what Mrema learned in a ver hard way kuwa hawana ubavu wa kushindana na serikali, na hasa wazee wa CCM.

3.
Wabunge ambao si mtandao, wenye uchungu wa kweli wa CCM, kuendelea kusulubisha viongozi wao na Serikali yao iwe wazi.

Watakaojisulubu ni mafisadi wenyewe kwa kuto taka kuelewa kuwa our political times as a nation has changed, na kwamba bunge halitakuwa the same tena kama zamani lwa wabunge waliolala!

4.
Hawa wabunge, mwokozi wao na nguzo yao ni Wastaafu Malecela, Kawawa, Mwinyi, Salim na Msuya.

Salim hayumo humo aliapa kuwa hataki tena siasa za bongo, lakini pia mwokozi wao ni sisi wananchi, Mkapa anaingia hapo sasa maana hana kundi na hajawahi kuwa nalo zaidi tu ya kushiirikiana na viongozi wezi, angekuwa na kundi angewaachia uongozi.

5.
Team Mkapa; huku ni wale wajanja wa Che-Nkapa ambao bado wanatibu majeruhi ya mchakato wa kugombea Urais 2005 na kunyang'anywa tonge la Hatamu za Chama. Hapa kuna Mang'ula, Ngwilizi, Kigoda, Kinana, Warioba na Ruhinda.

Kinana, hana kundi ni neutral, Warioba hana kundi alitemwa na mkapa baada ya ripoti yake long time ago, Ruhinda ni mtandao na ni director wa bodi Vodacom ya rostam,

6.
Team Kikwete ambayo wamebakia Makamba, Chiligati, Membe, Migiro, Karume 2. Team Rostwassa(Rostam/Lowassa); Karamagi, Msabaha, Nchimbi, Apson, Meghji, Kamala, Masha Diallo, Chenge,

Mtandao originally ulianzishwa kikwete mwenyewe kutokana na ku3wasiliana sana kwa text message na wenziwe, members wa kwanza walikuwa rostam, six, nchimbi, luhanjo, membe, mkalla, nyami, david mathayo, wengine wote waliingia baadaye kwa tamaa baada ya kuangalia upepo kwanza, kati ya hao mwenye matatizo ni rostam peke yake, wengine wote wako safi.

7.
Wasiofungamana lakini wana nguvu na ni tishio; Pinda, Mwandosya, Sumaye, Balali, Salmin, Magufuli, Msekwa na Sitta.

Pinda ni nguvu ya wazee wa ccm, sumaye iliisha pale tu mkapa alipomtema kwenye urais hana mfuasi hata mmoja, Salmin ni kundi la jm, sitta ni mtandao, msekwa hana kundi.

8.
Serikali mpya na baraza lake la mawaziri bado ni ya Kikwete Lowasa na Rostam.

Serikali inaongozwa na kiwkete kwa mashinikizo toka wazee wa ccm, ambao wako samba samba na bunge, na ndio the power behind kamati ya Mwakyembe.

9.
Masha-Mambo ya ndani, bila Lowasa Bw. Mdogo Masha asingekuwa hapo alipo, ni lowasa aliyemshika mkono na kumwingiza kwenye siasa,

masha na john mongela waaliingizwa kwa pamoja na Nchimbi,kuanzia kwenye ujumbe wa baraza la vijana wa mkoa Mwanza, shirika la sheria la masha na magai, walimuajiri ridhiwani na kujiweka sawa na kikwete, at this point masha is on his own baada ya kukwepa deal la Richimonduli.
 
Naona tumakaa sana bila kumkumbuka mtanzania mwenzetu ndugu yetu rafiki yetu kipenzi mh rostam aziz;kwa kweli katika mapito anayopitia kelele zote hizi na wizi wote alioufanya kwenye kagoda kufikia kuwafumba hata macho waziri mkuu na raisi wake na kumchanganya pinda kukimbilia kwenye deci;kwa kweli ushauri wangu mganga unayemtumia usimwache;na nina uhakika katika zile pikipiki pale bagamoyo zinazopeleka watu kwa waganga mganga wako hayumo...lazima utakuwa mwenyewe na kama kweli mstaarabu jaribu kwasaidia ndugu zako wakina mramba na yona na nduguyo mgonja wajikwamue kwa hili;mahakimu wahindwe hata kufukiria kesi zao;
watanzania tuendelee kusali hawa wanaootumia nguvu za giza ipo siku zitashindwa na uchafu utazidi kujulikana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom