Serikali achaneni na Tabibu Mwaka kwani anazidi tu kuwaumbueni!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
60,421
120,743
Kusema kweli leo nalia na Serikali na hasa Mamlaka zake hasa katika hili suala la huyu Tabibu Mwaka kwani sasa inaonekana dhahiri kuwa huyu Tabibu ni " Genius " kuliko hao wanaomfungia mara kwa mara.

Mlianza kumfuata fuata huyu Tabibu muda tu lakini kama kawaida yenu ya KUKURUPUKA bila kujipanga nyie mkija hivi yeye anawapelekeni kule na kiukweli anawashinda na mnaumbuka mno na leo najitokeza hapa kuwapeni " makavu " yenu.

Kiukweli mnatuchanganya sana kwani huku mnasema mmefungia kutoa huduma zake lakini wakati huo huo MWANAMUME Tabibu Mwaka anasikika tu " akitiririka " katika Vituo mbalimbali vya redio na hata tv tena akijipamba kabisa huku body language yake ikionyesha Jamaa ANAVYOWADHARAU na Mimi GENTAMYCINE leo nasema kwa aina hii ya UKURUPUKAJI wenu ambao sasa nauhisi kuwa ni CHUKI BINAFSI ZILIZOCHANGANYIKA NA WIVU DHIDI YAKE nasema Tabibu Mwaka ANASTAHILI KUWADHARAU na KUWAPELEKESHA.

Haya MATAMKO yenu yasiyo na KICHWA wala MIGUU yanatuchanganya na hata muda mwingine kutufanya TUMCHUKIE bure Baba wa Watu kumbe wakati mwingine inawezekana yeye ndiyo akawa yupo sahihi na labda nyie ( Mamlaka ) mliyomfungia ndiyo MNAUMWA!

Hata Mimi naomba nikiri kuwa NILIAMBUKIZWA chuki dhidi yake kwa haya MATAMKO yenu ambayo nayaita ya KIPUUZI na kiukweli nikawa namchukia Baba wa Watu Tabibu Mwaka lakini kwa aina ya UCHUNGUZI wangu nilioufanya natamka rasmi kuwa sasa nipo au naungana nae Tabibu Mwaka bega kwa bega na kuanzia sasa NITAMTETEA kwa nguvu zangu zote hadi muache KUMUONEA na kupitia bandiko langu hili hili nichukue nafasi hii kumuomba radhi Tabibu Mwaka kwa yale yote niliyokuwa nikimtakia humu kwani NILILEWESHWA CHUKI DHIDI YAKE na hizo MAMLAKA zenye CHUKI, WIVU na HASIRA dhidi yake na naamini hata Mwenyezi Mungu atakuwa amenisamehe pia.

Haingii AKILINI Mtu mnafungia asubuhi tena kwa kumpiga MIKWARA halafu baada tu ya Saa kadhaa anawazidi KIFIKRA na KIMAARIFA na kutoka kivingine. Mlikuwa MNAMDHARAU kuwa hana Elimu na ni " mjanja mjanja " ila sasa ninachokiona ni kwamba Tabibu Mwaka ndiyo " Kipanga " na nyie MAMLAKA mliyemfungia juzi ndiyo MAPOPOMA MLIOTUKUKA.

Huu OUNEVU wa aina hii hatutauruhusu hivyo basi kuanzia sasa TUTAUNGANA na Tabibu Mwaka na kumpigania hadi apate HAKI zake na kama kweli mnajua ana MAKOSA basi ni vyema mkayaweka na yawe na MANTIKI mbele yetu zaidi ya hapo TUNACHOKIONA ni kwamba SERIKALI hasa kupitia MAMLAKA zake zinazomfungia mara kwa mara ndiyo MNAMUONEA Tabibu Mwaka.

Hivi mnamfungiaje Mtu ambaye Watu wengi walioenda kupata TIBA kwake wamesema kuwa WAMEFANIKIWA na dawa zake na hakuna hata mmoja ambaye ameshajitokeza kusema kuwa AMEATHIRIKA na dawa zake sana sana ni Watu tu wenye JICHO LA HUSUDA dhidi yake ndiyo wanampakazia na kumchukia.

Principle yangu siku zote ni kuwa huwa SIPENDI UNAFIKI na NINAPOKUWA na DONGE MOYONI huwa SILIBAKISHI hata kama litamuhusu Mtu wangu wa karibu hivyo basi tunaomba nyie SERIKALI hasa kupitia MAMLAKA zenu huko Wizara ya AFYA hii nguvu mnayoitumia kumfuata fuata huyu Tabibu Mwaka basi mngeihamishia katika TAASISI au Hospitali nyingi za SERIKALI ambazo nadhani huko ndiko kuna UOZO na UMAGUMASHI ya kila aina ambao hupelekea Wagonjwa wengi kupoteza maisha huku wengine wakidhulumiwa na kunyanyaswa na Watendaji wenu wengi.

Nimemaliza!
 
Dr. Mwaka pamoja na kituo chake cha Foreplan wamefungiwa kutoa huduma yeyote ya dawa asili, lakini cha ajabu bado anaendelea kujitangaza kuwa anaendelea kutoa huduma ile ile na sehemu ile ile ya Ilala Bungoni.

Mwaka anajifanya eti anatangaza kampuni yake mpya ya Foreplan Limited wakati anatangaza kutoa huduma zile zile zilizofungiwa.

Na hivi vituo vya redio vinavyoendelea kumtangaza havijasikia tamko la serikali?

Najiuliza tu, Mwaka anatoa wapi kiburi cha kushindana na serikali hii ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli.

Kama anadhani kaonewa kwa nini asifuate utaratibu wa kukata rufaa kuliko kuendelea kuvimbiana na serikali?
Hivi akipewa adhabu kali zaidi atamlaumu nani?

Asifikiri serikali haijui ujanja anaotumia, hata hiyo kampuni anayoifanya kama cover-up imesajiliwa na serikali hii hii hivyo nayo inaweza kufungiwa, ni ushauri tu.
 
Dr. Mwaka pamoja na kituo chake cha Foreplan wamefungiwa kutoa huduma yeyote ya dawa asili, lakini cha ajabu bado anaendelea kujitangaza kuwa anaendelea kutoa huduma ile ile na sehemu ile ile Ilala Bungoni.

Mwaka anajifanya eti anatangaza kampuni yake mpya ya Foreplan Limited wakati anatangaza kutoa huduma zile zilizofungiwa.

Na hivi vituo vya redio vinavyoendelea kumtangaza havijasikia tamko la serikali?

Najiuliza tu, Mwaka anatoa wapi kiburi cha kushindana na serikali hii ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli.

Kama anadhani kaonewa kwa nini asifuate utaratibu wa kukata rufaa kuliko kuendelea kuvimbiana na serikali?

Hivi akipewa adhabu kali zaidi atamlaumu nani?
Kafungiwa yeye au Kampuni yake?

Pili hujui kuwa kazi ni uhai, na unapozuiliwa kufanya kazi ina maana huyo mtu anataka kusitisha uhai wako!
 
Dr. Mwaka pamoja na kituo chake cha Foreplan wamefungiwa kutoa huduma yeyote ya dawa asili, lakini cha ajabu bado anaendelea kujitangaza kuwa anaendelea kutoa huduma ile ile na sehemu ile ile Ilala Bungoni.

Mwaka anajifanya eti anatangaza kampuni yake mpya ya Foreplan Limited wakati anatangaza kutoa huduma zile zilizofungiwa.

Na hivi vituo vya redio vinavyoendelea kumtangaza havijasikia tamko la serikali?

Najiuliza tu, Mwaka anatoa wapi kiburi cha kushindana na serikali hii ya awamu ya tano chini ya rais Magufuli.

Kama anadhani kaonewa kwa nini asifuate utaratibu wa kukata rufaa kuliko kuendelea kuvimbiana na serikali?

Hivi akipewa adhabu kali zaidi atamlaumu nani?

Siku zote ukiwa unafuatiliwa na Watu lazima tu utawashinda na hatimaye watakupa jeuri na kuzidi kukupaisha.
 
Mwaka hawezi kuizidi Akili Serikali.Naona mnaona ndondo Cup itakosa ufadhili ndo mmeamua mmtetee

Hivi kama Mtu jana mnamfungia tena kwa " mikogo " yote halafu leo tunamuona akiendelea kupiga mzigo tena akiwa na " bashasha " na " dharau " zote huko siyo kuwa na JEURI na SERIKALI? Mkuu unatumia " Kiungo " gani cha mwili KUFIKIRI? Jambo dogo tu hili la Tabibu Mwaka linakushinda kulifanyia tu intellectual assessment kisha " ukajiongeza? ". Ndondo Cup hapa imeingiaje? Naomba niishie hapa nisizidi KUKUDHARAU kwani najijua mwenyewe.
 
Kaja kwa jina la Mkurugenzi wa Foreplan ltd. Ye katoa neno clinic na anaendelea kupiga hela. Inaonekana washauri wake wako vizuri sana

Ukishakuwa na HELA / PESA / FEDHA lazima tu pia utazungukwa na TECHNOCRATS hivyo utakuwa " unateleza " tu dhidi ya " wapuuzi ".
 
Kusema kweli leo nalia na Serikali na hasa Mamlaka zake hasa katika hili suala la huyu Tabibu Mwaka kwani sasa inaonekana dhahiri kuwa huyu Tabibu ni " Genius " kuliko hao wanaomfungia mara kwa mara.

Mlianza kumfuata fuata huyu Tabibu muda tu lakini kama kawaida yenu ya KUKURUPUKA bila kujipanga nyie mkija hivi yeye anawapelekeni kule na kiukweli anawashinda na mnaumbuka mno na leo najitokeza hapa kuwapeni " makavu " yenu.

Kiukweli mnatuchanganya sana kwani huku mnasema mmefungia kutoa huduma zake lakini wakati huo huo MWANAMUME Tabibu Mwaka anasikika tu " akitiririka " katika Vituo mbalimbali vya redio na hata tv tena akijipamba kabisa huku body language yake ikionyesha Jamaa ANAVYOWADHARAU na Mimi GENTAMYCINE leo nasema kwa aina hii ya UKURUPUKAJI wenu ambao sasa nauhisi kuwa ni CHUKI BINAFSI ZILIZOCHANGANYIKA NA WIVU DHIDI YAKE nasema Tabibu Mwaka ANASTAHILI KUWADHARAU na KUWAPELEKESHA.

Haya MATAMKO yenu yasiyo na KICHWA wala MIGUU yanatuchanganya na hata muda mwingine kutufanya TUMCHUKIE bure Baba wa Watu kumbe wakati mwingine inawezekana yeye ndiyo akawa yupo sahihi na labda nyie ( Mamlaka ) mliyomfungia ndiyo MNAUMWA!

Hata Mimi naomba nikiri kuwa NILIAMBUKIZWA chuki dhidi yake kwa haya MATAMKO yenu ambayo nayaita ya KIPUUZI na kiukweli nikawa namchukia Baba wa Watu Tabibu Mwaka lakini kwa aina ya UCHUNGUZI wangu nilioufanya natamka rasmi kuwa sasa nipo au naungana nae Tabibu Mwaka bega kwa bega na kuanzia sasa NITAMTETEA kwa nguvu zangu zote hadi muache KUMUONEA na kupitia bandiko langu hili hili nichukue nafasi hii kumuomba radhi Tabibu Mwaka kwa yale yote niliyokuwa nikimtakia humu kwani NILILEWESHWA CHUKI DHIDI YAKE na hizo MAMLAKA zenye CHUKI, WIVU na HASIRA dhidi yake na naamini hata Mwenyezi Mungu atakuwa amenisamehe pia.

Haingii AKILINI Mtu mnafungia asubuhi tena kwa kumpiga MIKWARA halafu baada tu ya Saa kadhaa anawazidi KIFIKRA na KIMAARIFA na kutoka kivingine. Mlikuwa MNAMDHARAU kuwa hana Elimu na ni " mjanja mjanja " ila sasa ninachokiona ni kwamba Tabibu Mwaka ndiyo " Kipanga " na nyie MAMLAKA mliyemfungia juzi ndiyo MAPOPOMA MLIOTUKUKA.

Huu OUNEVU wa aina hii hatutauruhusu hivyo basi kuanzia sasa TUTAUNGANA na Tabibu Mwaka na kumpigania hadi apate HAKI zake na kama kweli mnajua ana MAKOSA basi ni vyema mkayaweka na yawe na MANTIKI mbele yetu zaidi ya hapo TUNACHOKIONA ni kwamba SERIKALI hasa kupitia MAMLAKA zake zinazomfungia mara kwa mara ndiyo MNAMUONEA Tabibu Mwaka.

Hivi mnamfungiaje Mtu ambaye Watu wengi walioenda kupata TIBA kwake wamesema kuwa WAMEFANIKIWA na dawa zake na hakuna hata mmoja ambaye ameshajitokeza kusema kuwa AMEATHIRIKA na dawa zake sana sana ni Watu tu wenye JICHO LA HUSUDA dhidi yake ndiyo wanampakazia na kumchukia.

Principle yangu siku zote ni kuwa huwa SIPENDI UNAFIKI na NINAPOKUWA na DONGE MOYONI huwa SILIBAKISHI hata kama litamuhusu Mtu wangu wa karibu hivyo basi tunaomba nyie SERIKALI hasa kupitia MAMLAKA zenu huko Wizara ya AFYA hii nguvu mnayoitumia kumfuata fuata huyu Tabibu Mwaka basi mngeihamishia katika TAASISI au Hospitali nyingi za SERIKALI ambazo nadhani huko ndiko kuna UOZO na UMAGUMASHI ya kila aina ambao hupelekea Wagonjwa wengi kupoteza maisha huku wengine wakidhulumiwa na kunyanyaswa na Watendaji wenu wengi.

Nimemaliza!
Vp Shemeji Bado Anaendelea Kutumia Dawa Zake, Basi Na Mm Naungana Na Ww Kuhakikisha Hafungiwi, Lakini Fikiria Haya Ndg, Kuna Kitu Kinaitwa Medical Ethics Huyu Bwana Hafuati Hata Kidogo, Yeye Anafanya Kazi Kama Hospital Tena Ya Rufaa, Anavua Chupi Za Dada Na Wake Zetu Eti Anatibu Infertility Kwa Elimu Ipi?? Ndio Maana Hata Babu Wa Loliondo Alituteka Akili Na Phd Zetu Kichwani
 
kwani hiyo serikali ni ya malaika???? maana inaonekana unaiogopa sana ndugu...
 
Back
Top Bottom