Serikali achana na kujenga barabara za mwendokasi

Kwa uelewa wangu unazungumzia case moja inayowez kutokea mara chache sana. Tatzo la foleni sio njia nne Hatakam ukijenga njia nane Dar nzima bado factor za foleni ztabaki constant je traficlights, roundbout interaction znaruhusu flow of vehicle kwa haraka kwa muda mchache na katika direction zote so kutibu tatizo ndiposa Tanroads waje na mkakati madhubuti wa madaraja mfano Ubungo baada ya kujenga daraja foleni haipo tena je kuna njia nane pale?Hamna .
 
Sijui Kama umenielewa, hata taa zikiwepo acceleration ya Lori ni ya taratibu sana, fikiria una lane moja na foleni ya Malori 30, utavuka hiyo junction Kwa muda WA Zaidi ya nusu saa, angalia mifano yangu ni hai na hahitaji research Wala Nini ni uamuzi, unapofanyika mradi, wawe na future forecast WA operation na Sio narrow mindedness na kufikiria budget kama Hela ni za kwao, do once For ten years na Sio wanachojenga, Nalia na expertise ya Tanroads wanatuangusha big Time, tuwapigie kelele wazinduke
 
Ukianza kuclassify lorry ,suv,van ,buses nadhan Kuna kitu unamiss mfano gari la contena linaingia katikati ya mji kufanya Nini? Kwa kuanz classification ndiposa tunakuja na kitu kinaitwa Escape Route hizi ni zile barabara special kwa hizi long vehicle .tukisema kwamb tuweke njia nane na bado tuyaruhusu yaende mjin Hapan bado tatzo litakua ni lilelile.Nchi zilizoendelea xmeweka regulations na miundombinu wezeshi kuzuia folen ila sio kwa 100% kwa kuavoid hizi Long vehicles
 
Ndugu nime refer Changombe, their no any means to isolate the lories, Mikocheni Tipper trucks, people are still constructing, bila kusahau Lazy drivers, we always speaks the reality we don't need research for things which are vivid, WA Tanzania Sijui tukoje unabishia kitu kipo wazi, wewe unga Mkono Tanroads watatumia weledi wao
 
Tatizo tunajilinganisha na Watu waliokuwa focussed, sisi hata kupanga mitaa ni issue, unapata wapi uthubutu WA kulinganisha nchi zilizoendelea!? Think of your problem first, usijilinganishe na walioweza
 
miji yote bora duniani ina mwendo kasi hata kama ina barabara finyu. na ni usafiri unaosaidia sana kwa watu wa hali ya chini. acheni mawazo ya kizamani.
 
Sawa sawa mm nimeongea kiutafiti na reasoning nikatoa definition na solution ukaja na lorry nikakurekebisha kuhusu long vehicle ebu nambie lorry lipi la mchanga linaenda slow ,hivi lorry lenye gia mpak 8 lipo slow..nakurekebisha tu ungetetea hoja kuhusu two axial ,connected vehicle na Yale ya makontena Tanroads wako makini
 
Tatizo la stage za mwendokasi engineers walikosa ubunifu. Ni weird mtu kuvuka barabara akifate kituo. Pia kutuwekea matuta kwenye stage zao pia haijakaa poa. Engineers walikosa ubunifu hata wa kutengeneza njia za chini ili mtu apite akielekea kituoni kama vile tuna pita pale udsm coet?
Badala yake wamejenga ngazi ngazi baadhi ya vituo ambazo hata hazitumiki effectively.
 
Unaposema ubunifu ,zile sio underground Train station katika railway mkuu hoja yako haina mashiko kitu kutotumika effectively sio kwamba kisiwepo kabisa tunadesign kwa kuangalia miak 30 mbele
 
Dili za watu, hawatakusikia.
 
Mfano wako ni mbezi kibaha?
Je idadi ya magari kwa siku ni sawa na Dar es salaam?

Unajua Dar ina wakazi kiasi gani na wanaoingia kila siku ni kiasi gani?

BRT ni usafiri wa uma haijawekwa kwa ajili ya kupunguza foleni. Imewekwakwa ajili ya kurahisisha usafiri wa uma uwe standard.
 
Ukijua lengo la mwendokasi basi utakuja kuedit uzi wako....

1. Barabara hata ujenge njia 20 itafikia kipindi kutakua na foleni.
2. Foleni nyingi hutokea kwenye intersections. Mfano foleni ya ubungo imetatuliwa na just overpass mbili.
3.
Nadhani mtoa mada ameongelea vizuri tu kuwa kutokana na hali ilivyo. mimi nilikuwa na kadi na ilikuwa uhakika 15 Ubungo Posta asubuhi na jioni Posta Ubungo 15. Niliacha sababu alizozielezea mdau ,sasa barabara za magari ya binafsi zimekuwa nyemmbamba mfano sokoine drive kiasi magari yanapita mstari mmoja. Watu wa kimara unakuta kama ni daladala inaweza fika mjininkabla ya abiria anayengojea mwendo kasi sababu gari linakuja la mwendo kasi moja abiria ni wengi..nchi za wenzetu njia ingefaa ijengwe juu na ziwe treni ingesaidia sana maana inakuja na mabehewa mengi inauwezo wa kubeba abiria wengi
 
yani mtu na akili zako kabisa ukapande hayo mamwendokasi? tena umevaa na kasuti kako na kipafyumu umepaka loh, utatoka unanuka kinyesi kwa jinsi utakavyobanwa yaani kimsingi huo mradi umeshawashinda heri hata daladala za mbagala zina afadhali.
 
Wanasema Walijenga Dart Kwa Ajili ya kuomarisha usafiri wa Umma na hivyo ku encourage watu kutumia Mwendokasi badala ya magari binafsi.

Ila lomradi limefeli ,mambo ya kuiga.kwa Wazungu na mbaya zaidi ni mkopo
 
Barabara za kuja katikati ya Jiji ndio ziwe na BRT na light train

Pili Zijengwe Barabara nyingi Nje ya Jiji kiasi kwamba kusiwe na ulazima wa kutumia Barabara chache

Tatu kuanzishwe business centers zingine Nje ya Mji kiasi kwamba kusiwe na ulazima wa kwenda city centre.
 
Barabara za kuja katikati ya Jiji ndio ziwe na BRT na light train
In the end kwa kuhakikisha shida zinaondoka kabisa any City worth its Salt lazima iwe na Tube System lakini cost na umuhimu wake kulingana na uzalishaji sidhani kama tumefika huko (ila miaka elfu kadhaa ijayo huenda hii ndio dawa)
Pili Zijengwe Barabara nyingi Nje ya Jiji kiasi kwamba kusiwe na ulazima wa kutumia Barabara chache
Kwamba zikijengwa nje ya mji nyingi watu wakitaka kuja katikatika ya mji watatumia mazingaombwe (kwa zijengwe kwanza nyingi pasipo na uhitaji kuliko kwenye uhitaji
Tatu kuanzishwe business centers zingine Nje ya Mji kiasi kwamba kusiwe na ulazima wa kwenda city centre.
Ofcourse hilo nalo ni jawabo Satellite cities na nadhani sio kwamba hilo halifanyiki sasa na vilevile uwapo wa moja sio jawabu la kutokuwepo kwa lingine...., In short efficient and Convenient Mass Public Transport ni jambo la muhimu katika jamii yoyote ya wastaarabu...
 
Wanasema Walijenga Dart Kwa Ajili ya kuomarisha usafiri wa Umma na hivyo ku encourage watu kutumia Mwendokasi badala ya magari binafsi.

Ila lomradi limefeli ,mambo ya kuiga.kwa Wazungu na mbaya zaidi ni mkopo
Wao wenyewe waendeshaji ndiyo wanafeli...
Abiria wengi,wanaingiza magari machache

Mwisho,serikali hii chini ya ccm haiwezagi kufanya biashara

Ova
 
Tatizo la Tanzania tumeacha kujenga barabara za njia nane tumekomaa kujenga njia nne na mwendokasi tukidhani ndio suluhu ya foleni.
Miji mikubwa kama Dubai hakuna mwendokasi ila wamejenga barabara kubwa sana huku ukitaka uharaka unapanda treni/metro.
Mwendokasi wa Tanzania umeongeza foleni badala ya kupunguza foleni sababu ya kufinya barabara ya magari binafsi.
 
You are right! Naona wewe tunasaifiri wote kimtazamo. Nilikuwa najiuliza sana kwamba hvi hakukuwa na njia nyingine mbadala ya watu kuvifikia vituo vya kupandia mabasi ya mwendokasi? Maana naona hizi ngazi wanazojenga kwanza ni very complicated (umbali mrefu kufikia kituo) lakini pia zinachukua nafasi kubwa sana na mwisho zinaharibu tu taswira/sura ya eneo husika mfano mzuri ni pale Kimara yanapoishia mabasi ya mwendo kazi. Taswira ya lile eneo imeharibiwa na hilo daraja la waenda kwa miguu!

Likaja wazo kwa nini hawakujenga tunnels (au tunnels ni expensive sana?) nikaamua kuliacha kama lilivyo lakini kwa kweli mimi siyo mpenzi wa mangazi/madaraja ya juu ya waenda kwa miguu ya ajabu ajabu kama yale ya ubungo, Kimara au Mbezi kwa Magufuli terminal. Mimi siyo injinia bali ni mtazamo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…