Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 482
Leo asubuhi wafanyabiashara kwenye soko la Mbuyuni manispaa ya Moshi wameshikwa na butwaa baada ya kuja na kukuta vibanda vyao vimevunjwa na askari wa manispaa wakishirikiana na askari polisi. Vijana hao walipofika kwenye biashara zao hawakuamini kilichotokea. Wakiwa katika hali ya kutafakari polisi nao walifika na kuanza kurusha risasi hewani. Hii sio mara ya kwanza kwa wafanyabiashara wa Moshi kufanyiwa uhuni kama huu. Soku kuu la Moshi liliwahi kuungua na kusadikika kuwa lilichomwa makusudi na maafisa wa manispaa. Soko la juu nalo liliunguzwa na watu haohao. Wafanyabiashara wa eneo kwenye kiwanja cha CCM maarufu kama shimoni karibu na stendi kuu ya Moshi kilitokea kituko kama hicho pia. Stendi kuu ya mabasi ya Moshi pia iliwahi kuunguzwa ili manispaa waweze kujenga upya. Matukio yote haya yaliacha hasara kubwa kama sio watu kufa kwa shinikizo la damu.
Tukio la usiku wa kuamkia leo limetafsiriwa na wakaazi wa Moshi kama KULIPIZA KISASI kwa serekali iliyoko madarakani kwa kuwapa upinzani kura nyingi na kuinyima CCM. Wanahoji walikuwa wapi siku zote wksti wa kampeni wafanyabiashara walipanga biashara zao karibu kabisa na kituo cha polisi na hakuna aliyewauliza kitu! Je ruksa ya wakati huo ailikuwa HONGO ama ni nini? Hivi ndivyo serekali imeanza kazi?