Sera za Tanzania kwa Congo zitaathiriwa vipi na ushindi wa Felix Tshisekedi, mgombea kutoka upinzani?

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,240
9,527
Mwaka 2014 nilikuwa Congo ila sikuzurura sana kwasababu ya hali ya usalama wakati huo. Nilijikalia Goma nikatulia tuli!!

Tanzania inapendwa sana Congo, ukitaka bia za offer kwenye baa za Congo basi itamke Tanzania.
Kwanini?

Kuna wanajeshi wengi sana Congo wanaosubiri mwisho wa mwezi kuchukua mishahara minono bila kazi kubwa. Kazi yao mara nyingi ni kubeba 1.5kg ya smg na kupiga saluti.
Hao ni wanajeshi kutoka umoja wa mataifa ila sio watanzania.
Watanzania wanapigana sana, wana ari na kushinda vita.
Kila mwanajeshi wa kitanzania anayeingia Congo anaomba kupelekwa mstari wa mbele wa mapambano!

Hilo sidhani kama litaendelea maana Kabila hayupo tena. Si yeye tu, hata chama chake hakipo. Yupo bwana Felix kwa sasa ambaye bado hajaapishwa.

Sera yetu kwa Congo haiko wazi, na ndio maana rais wetu wa nchi ana urafiki na Kagame ambaye kimsingi ndio tunaepigana nae Congo!

Cobalt!!!
Hii ndio sababu inayonifanya niseme kuwa Kagame ndio adui wetu mkubwa Congo (angalau kwa level zetu maana mwisho wa siku sisi wote ni vibaraka).
Kagame ni muuzaji mkubwa wa Cobalt kwa huu ukanda wa maziwa makuu ilihali hana mgodi wa maana wa Cobalt.

Cobalt sio kitu cha mchezo!!!!!

Angalia smartphone unayotumia - iko powered na Cobalt.
Mradi mkubwa duniani wa magari ya kuendeshwa kwa battery tu za umeme unategemea Cobalt. Hivyo Cobalt sio kitu kidogo!

Power behind the throne!
France vs Belgium
Hili nitaliongelea kwenye thread nyingine.
Nitasema sisi tunalipwa na nani kukaa Congo, kwanini vijana wetu wapoteze maisha kwa maslahi ya matajiri, na mengine mengi!

Je, sera yetu kama taifa kwa Congo itabadilika?

Sent using Jamii Forums mobile app
》》》》》》》》》》》》》》》》》

TUENDELEE

SERA YA TANZANIA KWA CONGO!
Nimejaribu kuangalia 'sera ya Tanzania kwa nchi za nje/ mambo ya nje' - Tanzania foreign policy 2015 na hakuna sera specific kwaajili ya Congo.
Jambo hili naliona kama sio la afya kwetu kwasababu ya ukubwa na upana wa ushiriki wetu kwa mambo ya Congo!
Tukiweka sera specific kwaajili ya Congo itatupa fursa ya kuangalia mwenendo wa vikosi vyetu kwa ukaribu zaidi, maslahi yao na maslahi yetu kama taifa.
Tutaweza pia kufanya foresight ya ushiriki wetu kwa siku zijazo Congo maana kama nitakavyoeleza baadae, vita ya Congo sio vita ya kuisha leo au kesho!!

POWER BEHIND THE THRONE
Kiukweli kabisa hakuna kiongozi wa Congo aliyewahi kuwa na mamlaka na nguvu za kweli za kiuongozi tokea Congo imepata uhuru.
Kila unapoangalia historia ya Congo lazima kuna majina yatajitokeza, always!
Lazima USA awepo na Belgium na France.
Kuna wengine wengine lakini hao ni wadau wadogo tu, washika dau haswa ni hao hapo juu!

Congo inateswa na uzuri wake, ukubwa wake na rasilimali zake!

copper, gold, diamonds, cobalt, uranium, coltan na mafuta ni baadhi tu ya rasilimali zinazopatikana kwa wingi Congo. Ukijumlisha na ardhi kubwa, ya pili kwa ukubwa Africa, nyuma ya Algeria yenye rutuba na mto unaosadikika kuwa na kina kirefu kuliko yote duniani, mto Congo (maarufu kama -the Congo) vinafanya wale tunaopenda kuwaita mabeberu wakose usingizi wakiiwaza Congo.

Belgium kwa mfano 1/6 ya pato lake la ndani inatokana na sekta ya manufacturing inayobebwa sana na malighafi zinazotoka Congo, hasa Cobalt!

Umicore kwa mfano ni kampuni kubwa sana Belgium yenye wafanyakazi 9,700 na turnover ya euro 12.3 billion kwa mwaka.
Hii ni kampuni moja tu ambayo uhai wake unategemea malighafi kutoka Congo.Kwao hawa yeyote atakaewawezesha kuzipata hizi malighafi watakuwa nae bega kwa bega.

Cobalt inatumika zaidi kutengenezea lithium-ion batteries. Hizi ni betri tunazotumia kwenye smartphone zetu na zile rechargeables za magari ya kisasa yanayoendeshwa kwa system ya umeme.

Ila impact yake kwa uchumi wa Belgium haiishii hapo, kuna sekta ya utafiti ambayo inaweza kufanya kazi kubwa kwasababu ya hizi malighafi na mapato yanayotokana na export ya hizo end-product zake.

USA yeye ni mdau mkubwa sana wa maendeleo Congo na kama ilivyo kawaida yake, yeye ananyonya mafuta.
Sawa anarudisha fadhila kwa kutoa misaada ya kibinadamu kwenye maafa na vita ila pia anauza silaha MONUSCO ambalo ni jeshi la kulinda amani la UN.
Ukimuangalia vizuri USA utagundua kwamba amani ikipatikana Congo umuhimu wake utapungua.
Labda kutakuwa na sababu ya kiangalia upya terms za kibiashara na kufikiria wadau wengine pia. Unafikiri USA anapenda kujikuta kwenye nafasi hiyo?
Well hapendi!! Na ndio maana amehakikisha silaha ndogondogo zinajaa mtaani kama karanga!
Congo kama umekosana na jamaa, ukilipa elfu 10 tu kwa thamani ya hela ya kitanzania basi jamaa analimwa risasi.

Kufikia 29 May 2017 MONUSCO ilikuwa na takrinani jumla watu elfu 23 kwenye payroll yake. Kuanzia wanajeshi mpaka wafanyakazi wa kawaida.
Hawa amani ikipatikana Congo unadhani watakwenda wapi?
Unafikiri wanatamaani amani ipatikane Congo?

☆Twende kwenye mapumziko mafupi, tukirudi tumuangalie France, njaa ya Kagame na Museveni Congo. Tujiangalie na sisi watanzania tunaonyofolewa roho kila kukicha na kama uwepo wetu kule una maslahi yoyote ya maana kwetu☆.
 
Hamna mabadiliko makubwa kwasababu kwanza kuna sehemu kubwa ya wacongo walioshindwa kupiga kura kwasababu ya kukosekana kwa miundombinu yakupigia kura.

Pili huyu Tshisekedi amepata 38% ya kura.
Maana yake ni kuwa 62% ya waliopiga kura hawamwamini!
Hivyo mziki bado upo.
Naiona kongo ijayo ipo kama china. Hakika congo itabadilika haswaa. Walioshikilia kidedea kumuondoa kabila ni kanisa katoliki.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naiona kongo ijayo ipo kama china. Hakika congo itabadilika haswaa. Walioshikilia kidedea kumuondoa kabila ni kanisa katoliki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Congo haitakuja kuwasalama kwani mabeberu ndo walipochomeka mirija yao, China, USA, EU, Rwanda, SA, Angola, Uganda nk Hata hyo Tshekedi akicheza wanamuondoa.
Congo itatengemaa tu pale matajiri wao watakapoacha kuwa vibaraka wa wakubwa
 
Congo ina ukubwa wa Ulaya Magharibi, ni ngumu sana kuitawala kwa mfumo uliopo.
Kutoka Goma mpaka Kinshasa kwa basi unatumia nauli ya milioni na sehemu kwa fedha za kitanzania.

I was very surprised ati usafiri wa ndege ndani ya Drc ni Common kuliko mabasi kutokana na miundombinu hafifu ya barabara na mauaji ya.misituni..ile nchi ni pasua kichwa!
 
Nasubiri kuona namna ambavyo serikali mpya itakavyopambana na hao waasi wa mashariki.

Ile nchi ni tajiri sana, makontena ya coltan yanasafirishwa mwaka mzima, january mpaka disemba mzigo unapanda meli.

Wazungu nyoko haswa, wamehakikisha jamaa wanatwangana wakati wao kiupolee wanachukua mzigo.
 
Mwaka 2014 nilikuwa Congo ila sikuzurura sana kwasababu ya hali ya usalama wakati huo. Nilijikalia Goma nikatulia tuli!!

Tanzania inapendwa sana Congo, ukitaka bia za offer kwenye baa za Congo basi itamke Tanzania.
Kwanini?

Kuna wanajeshi wengi sana Congo wanaosubiri mwisho wa mwezi kuchukua mishahara minono bila kazi kubwa. Kazi yao mara nyingi ni kubeba 1.5kg ya smg na kupiga saluti.
Hao ni wanajeshi kutoka umoja wa mataifa ila sio watanzania.
Watanzania wanapigana sana, wana ari na kushinda vita.
Kila mwanajeshi wa kitanzania anayeingia Congo anaomba kupelekwa mstari wa mbele wa mapambano!

Hilo sidhani kama litaendelea maana Kabila hayupo tena. Si yeye tu, hata chama chake hakipo. Yupo bwana Felix kwa sasa ambaye bado hajaapishwa.

Sera yetu kwa Congo haiko wazi, na ndio maana rais wetu wa nchi ana urafiki na Kagame ambaye kimsingi ndio tunaepigana nae Congo!

Cobalt!!!
Hii ndio sababu inayonifanya niseme kuwa Kagame ndio adui wetu mkubwa Congo (angalau kwa level zetu maana mwisho wa siku sisi wote ni vibaraka).
Kagame ni muuzaji mkubwa wa Cobalt kwa huu ukanda wa maziwa makuu ilihali hana mgodi wa maana wa Cobalt.

Cobalt sio kitu cha mchezo!!!!!

Angalia smartphone unayotumia - iko powered na Cobalt.
Mradi mkubwa duniani wa magari ya kuendeshwa kwa battery tu za umeme unategemea Cobalt. Hivyo Cobalt sio kitu kidogo!

Power behind the throne!
France vs Belgium
Hili nitaliongelea kwenye thread nyingine.
Nitasema sisi tunalipwa na nani kukaa Congo, kwanini vijana wetu wapoteze maisha kwa maslahi ya matajiri, na mengine mengi!

Je, sera yetu kama taifa kwa Congo itabadilika?

Sent using Jamii Forums mobile app
Na wasiwasi Bwana Felix ameingia kwenye makubalino na wakina Kabila ilikuonesha wapinzani wameshinda kwasababu kwa mujibu wa redio mbao mshindi wa kweli siyo yeye. Napata wasiwasi hii style huko mbeleni CCM wataitumia.
Kiukweli hii akili Waafrika tungetumia kwenye maendeleo tungekuwa mbali sana.
 
Back
Top Bottom