Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,982
- 45,891
Wengi wetu tuliona kuwa hiki chama hakifai, na bado tunaimani kwamba tulikuwa sahihi.
CHADEMA walikuja kupata umaarufu kwa kupinga kila jambo ambalo walikuwa wanaliona ni ovu katika jamii yetu.
CHADEMA walikuwa wanapinga utendaji mbovu kwenye ofisi za umma, walikuwa wakipinga matumizi mabaya ya fedha za umma, walikuwa wakipinga ufisadi na wizi uliokithiri, walikuwa wakituaminisha kwamba wanachukia sana vitu vyote hivyo. Baadhi waliamini lakini sisi hatukuamini kama ni kweli walimaanisha wanachotaka tuamini kuwa wakanisimamia.
Baada ya kuingia awamu ya tano, Magufuli alihakikisha kuna nidhamu katika ofisi za uma, jambo ambalo ni dhahiri sana, watakaopinga watakuwa wachache, kwani ukienda sasa katika ofisi za umma yale mambo ya kuambiwa njoo kesho au subiri, yamepungua au kwisha kabisa yote hayo yamewezekana baada ya utumbuaji kushika hatamu.
Ufisadi mkubwa na wawazi hakuna tena, kwakweli Mahakama ya mafisadi ni kama Onyo kuwa sheria itachukuliwa kwa yeyote atayejihusisha nao.
Serikali kwa kiasi kikubwa imepunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa kupunguza safari za ndani na nje ya nchi kwa watumishi wake, jambo hili limeokoa fedha nyingi sana za walipa kodi.
Kwa kiasi kikubwa swala la uzembe, ufisadi na wizi wa wazi wazi umepungua.
Ukiachana na yote hayo bado wapinzani wanasema kuwa Magufuli hafanyi lolote, ni dikteta , wengi tunajiuliza huo udikteta unaosemekana upo ni upi, je ni huu huu, wa kukataza wizi , ubadhirifu na ufisadi wa fedha za uma? je udikteta huu ni wa kuhakikisha kuwa nidhamu ya kazi na usimamizi wa miradi unakuwepo?
Kama CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vinapinga juhudi hizi za wazi, juhudi ambazo wao walisema na ajenda zao na bado mpaka sasa wanaendelea kusema kwamba Magufuli anatekeleza sera zao? Huu ni mkanganyiko mkubwa sana na kiashirio cha siasa za kitapeli.
Kama kinachofanyika sasa ndio kile kile Walichokuwa wakitaka kutuaminisha kuwa watakifanya wakiingia madarakani, kukipinga ni sawa na kusema kwamba sera zao hazikuwa sahihi. Sera za chadema ni mbovu kwakuwa wanazipinga sasa.
CHADEMA hawastahili kupewa nchi kwakuwa wanasera mbovu ambazo hazitekelezeki, na mfano mzuri ni huu wa sasa kutokana na namna wanavyompinga Magufuli anayetekeleza sera zao.