Sera ya majimbo ya CHADEMA inatekeleza Katiba ya nchi

Sera ya majimbo ya CHADEMA inatekeleza Katiba ya nchi

Stabilaiza

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Posts
1,843
Reaction score
1,143
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka wazi kuwa mamlaka yote katika nchi yanatoka kwa wananchi. Hivyo sera ya majimbo ya CHADEMA inatekeleza kwa vitendo ushiriki wa wananchi katika utawala.

Kwa kupitia sera ya majimbo ambayo lengo lake ni kuongeza madaraka kwa wananchi katika kusimamia wawakilishi wao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika eneo husika. Ni vigumu kuona matatizo kwa ukaribu kwa kuongoza kutokea Dar es Slaam. Usimamizi wa raslimali na shughuli za maendelo utakuwa rahisi na hivyo kuimarisha katika yetu ya nchi.

Sera hii ya majimbo pia itaimarisha local governments kwa vile usimamizi wake utakuwa karibu zaidi kuliko kutokea Dar es Salaam. Taasisi mbalimbali katika nchi hii zimegawanya katika maeneo madogo ili kuleta ufanisi na kufanya utekelezaji kuwa rahisi. Mfano wa Taasisi hizi ni Radio Tanzania. Radio Tanzania wana kanda ya mashariki, kanda ya kati, kanda ya kusini, kanda ya magharibi ili kuleta huduma wanazotoa ziwe karibu zaidi na wananchi.

Pia TANESCO imegawanywa katika kanda mbalimbali ziitazo mikoa, ambayo ni tofauti na mikoa ya nchi. Hivyo sera ya majimbo ya CHADEMA inatekeleza kikamilifu matakwa ya katiba ya Tanzania inayohimiza madaraka ya nchi kuwa mikononi mwa umma.
 
ndg,stablize,hii imekaa vizuri mno,waelimishe mambumbu wasio jua kwamba katiba inasema mamlaka yote ya serikali itatoka kwa wananchi,lakini ccm imewapora mamlaka yao, na kuwa yenyewe sasa ni serikali tukufu kutoka mbinguni,aitakiku hojiwa na wenye nchi ambao ni sisi kikatiba,tukiihoji tunaitwa wachochezi tunataka kuvuruga amani,mifano ni mingi sana,kule mtwara gesi ilileta kasheshe,wenye nchi hawataki gesi iende dar,serikali inawaita wachochezi,na hii imekua ndio ngonjera ya serikali ya ccm,ikiguswa na maswali ya msingi ya wananchi,hooo hawa ni wachochezi,sasa uhu mpango wa cdm kuleta serikali za majimbo ni yakuungwa mkono na watanzania wote,sasa madarakaka yatarudi kwa wenye nchi,badala ya kuoziwa na kakundi cha wapiga dili mafisadi,mambo ya uzauza yatakua mwisho wananchi watakua na sauti na maamuzi juu ya rasilimali zao,
 
Ndio maana nimeleta uzi huu ili pamoja tuwaeleze wananchi kuwa sera ya majimbo imekaa sawa, inashabihiana na matakwa ya Katiba na nchi yetu
 
Hospitali ziko za kanda,kuna mahakama za kanda,kuna kanda maalumu za kipolisi,na mvua hua zinanyesha kufuata ukanda hainyeshi nchi nzima kwa wakati mmoja,nahata kunamazao ya kikanda mpaka udongo hutofautiana kikanda,kiswahili chenyewe nichakikanda mfano mama kuna kanda zinaita mamaa,au babaa, kakaa nk.ukanda ulikuwepo na utaendelea kuwepo,kwani hata madini yanapatikana kikanda siamini kama kanda yaziwa wanaweza kuvuna tanzanait?ndio maana hua unasikia mikoa ya kanda ya kusini hua kuna baridi sana nk.nch hii nikubwa bila kugawa ngwe huto imaliza nandio maana mpaka sasa kunawatu bado wanajua nyerere ni rais.CHADEMA ahsanteni kwa kutimiza haja zetu tunajua 2015 mkichukua nchi mtacheza viwanja vyote kwa wakati nasio ccm zao ni dar tu kila waziri dar hata kama kazaliwa singida hahahaha maccm polisi!! Mweee
 
Taaratibu wataelewa tu,Nikiombe chama tu kiunde jopo la watu wakuwaelimisha wananchi hata kwa njia za matoleo ya magazeti na cds kufikia 2015 walau watz wawe wanajua nini maana ya mamlaka kurejeshwa mikononi mwao!
 
Hospitali ziko za kanda,kuna mahakama za kanda,kuna kanda maalumu za kipolisi,na mvua hua zinanyesha kufuata ukanda hainyeshi nchi nzima kwa wakati mmoja,nahata kunamazao ya kikanda mpaka udongo hutofautiana kikanda,kiswahili chenyewe nichakikanda mfano mama kuna kanda zinaita mamaa,au babaa, kakaa nk.ukanda ulikuwepo na utaendelea kuwepo,kwani hata madini yanapatikana kikanda siamini kama kanda yaziwa wanaweza kuvuna tanzanait?ndio maana hua unasikia mikoa ya kanda ya kusini hua kuna baridi sana nk.nch hii nikubwa bila kugawa ngwe huto imaliza nandio maana mpaka sasa kunawatu bado wanajua nyerere ni rais.CHADEMA ahsanteni kwa kutimiza haja zetu tunajua 2015 mkichukua nchi mtacheza viwanja vyote kwa wakati nasio ccm zao ni dar tu kila waziri dar hata kama kazaliwa singida hahahaha maccm polisi!! Mweee

:yo:isaluti,u,baaria,
 
Mkuu, hii nimeipenda saana! Elimu hii tamu kweli. Hebu tafuta jukwaa la kutuelimisha wengi zaidi!.... Hata mvua hufuata kanda, polisi nao kanda!!!!!!!.... Safi!
 
Nadhani ipo siku ccm watamkaririsha mbunge wao ataikopi na kuipesti na kuiwasilisha kama hoja binafsi.
 
Hii iko poa, Sera ya Kanda imewashika pabaya Magamba kwa sasa wanaweweseka.
 
kama wasomi wenyewe wanaoielewa katiba ndo nyie basi tumekwisha. au unaongelea katiba ya kenya? sio wengine hatuna ufahamu wa kutosha na hiyo ya kenya kama ndo unayomaanisha,
 
ungesema chadema ingetokea wakaingia madarani ndo wangebadilisha, hapo ungeeleka na hasa unapojadili na waelewa. hiyo jadili na mazezeta wenzako tu.
 
Ndg makamanda;

Kutokana na minong'ono ya baadhi ya watu humu jf kama vile mzee mwanakijiji na wengine,nimeamua kuweka wazi kuwa sera majimbo ya chadema iko kikatiba kwa ufafanuzi ufuatao;

mosi:inawezekana tatizo linalowachanganya watu ni tofauti ya neno kanda na jimbo,napenda kuweka wazi kuwa tumeamua kutangaza kanda/majimbo zetu/yetu kwa kutumia katiba ya chama chetu,kwa mujibu wa katiba ya chama chetu ktk 7:6 inaonesha wazi mfumo wa uongozi wa kanda/jimbo utakuwa hivi;7.6.1 kutakuwa na baraza la uongozi wa jimbo na litaundwa na mabaraza ya uongozi wa mikoa inayounda jimbo husika kwa mfano jimbo/kanda ya kati litaundwa na mabaraza ya uongozi ya mikoa ya singida,dodoma na morogoro,

pili:KATIKA 7.6.2 majimbo au kanda hizo zitakuwa na kazi ya kukishauri chama juu ya mambo mbalimbali ya kisera yanayohusu jimbo husika,pia kuchagua wajumbe wa kuwakilisha jimbo kwenye baraza kuu.

Pia ktk 7.6.3 inaelezea jinsi vitakavyofanyika na jinsi ya kuviitisha,

NAAMINI KUWA KUNAITAJIKA MAREKEBISHO KADHAA KATIKA MFUMO HUU WA MAJIMBO ILI UWEZE KUENDANA MOJA KWA MOJA NA KATIBA YA CHAMA COZ KUNA BAADHI YA VITU VICHACHE VINAHITAJIKA NA MKUTANO MKUU NDIO WENYE MAMLAKA YA KUBADILISHA KATIBA AU VIPENGELE VYA KWENYE KATIBA.

By kimboka sawere.
 
wanaofiki semen ndio, ndiooooooooo! ?wasioafiki waseme hapana,hapanaaaaaaa! Walioafiki wameshnda,jukwaa linaendelea na shguhul zake
 
Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka wazi kuwa mamlaka yote katika nchi yanatoka kwa wananchi. Hivyo sera ya majimbo ya CHADEMA inatekeleza kwa vitendo ushiriki wa wananchi katika utawala. Kwa kupitia sera ya majimbo ambayo lengo lake ni kuongeza madaraka kwa wananchi katika kusimamia wawakilishi wao na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika eneo husika. Ni vigumu kuona matatizo kwa ukaribu kwa kuongoza kutokea Dar es Slaam. Usimamizi wa raslimali na shughuli za maendelo utakuwa rahisi na hivyo kuimarisha katika yetu ya nchi.

Sera hii ya majimbo pia itaimarisha local governments kwa vile usimamizi wake utakuwa karibu zaidi kuliko kutokea Dar es Salaam. Taasisi mbalimbali katika nchi hii zimegawanya katika maeneo madogo ili kuleta ufanisi na kufanya utekelezaji kuwa rahisi. Mfano wa Taasisi hizi ni Radio Tanzania. Radio Tanzania wana kanda ya mashariki, kanda ya kati, kanda ya kusini, kanda ya magharibi ili kuleta huduma wanazotoa ziwe karibu zaidi na wananchi. Pia TANESCO imegawanywa katika kanda mbalimbali ziitazo mikoa, ambayo ni tofauti na mikoa ya nchi. Hivyo sera ya majimbo ya CHADEMA inatekeleza kikamilifu matakwa ya katiba ya Tanzania inayohimiza madaraka ya nchi kuwa mikononi mwa umma.

mkuu, hujui ulisemalo na mjadala wako hauna mashiko
 
kumbuka TANESCO haiongozi kimajimbo. ina Mkurugenzi Mtendaji mmoja ambaye ambaye ndiye huratibu utendaji wa ofisi zote za kanda. si kila kanda hutumia mapato yake kuendeleza kanda husika. na huo utaratibu wa kanda hutumika tu hapa Dar es Salaam na si mikoa yote. na hapo hoja inayotumika ni kanda na si majimbo.

kuhusu RTD ni kuwa walifanya hivyo kutokana na uwezo mdogo wa shirika hilo kutoa huduma mikoa yote. ndiyo maana wakawa na RTD kanda ya kusini kuhudumia mikoa ya lindi, mtwara na ruvuma. walipoimarisha mitambo katika mikoa yote, RTD kanda ya kusini ikawa haipo tena. kumbuka serikali iliyo karibu na wananchi haiongozwi kimajimbo. ni serikali ya kijiji na mtaa ndiyo iliyo karibu zaidi.

serikali ya watu inayoelezwa hapo si ya majimbo. ni serikali ya kidemokrasia ambayo hutokana na watu, the government of the people by the people and for the people. hiyo ni tofauti na utawala wa kiimla (udicteta) ambao hautokani na watu
 
Back
Top Bottom