IZENGOB
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 323
- 317
Nikiwa natafakari juu ya mambo mbalimbali yanayotokea katika nchi yangu,ninaona wingu zito lililogubikwa na sauti za wanyonge walio na vilio vya kila aina huku wakiwa na tumaini tupu la Nchi ya viwanda yenye kuwajali wanyonge na walio kata tamaa.Hakika walikufurahia sana pengine waliwaza na kujiaminisha kuwa wewe ndio mkombozi wa maisha yao kwa kuwa ulikuwa na sera zilizotukuka na zilizojaa manukato ya nchi mpya ambayo ni ya kujali wanyonge na kujinadi kuwa wewe ni "mpenda haki,mtetezi wao,mwenye hamu na ashiki ya kuwafunga walafi na mafisadi waliofuja mali za umma,wezi wa kutumia kalamu na wengine walianza kukukimbia ndani ya Chama chako.
Wengi walitegemea kusikia waliohusika na lada akina chenga,waliowatorosha wanyama pori akina ....,waliokusanya mabilioni kwenye mgao wa Nshomile wa Bukoba,na yule jamaa maarufu mwenye mvi mliokuwa mkimuimba na kumtukana jukwaaani wakikamatwa na kufungwa.
Inasikitisha kuona wale wanaothubutu kupaza sauti zao kutumia akili na maarifa yao kuelimisha,kukosoa na kuikanya serikali,pengine hata kufichua maovu,wanaosimamia ukweli na hoja zenye mashiko,wanaowalilia watanzania, wanakanyagwa na kupotea kama punje ya haradani kwenye mguu wa tembo.
Kila nilalapo niamkapo nawaona vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa hili wakiwa wamefungwa pingu najiuliza swali "Je mafisadi ndio hawa naowaona wakisindikizwa na polisi wenye mitutu na silaha kali za kivita?"Jibu ni la hasha hawa ni vijana wapenda haki,wanaolilia uhuru wa kutoa maoni wanaolilia utawala wa kufuata sheria na katiba tuliyoitunga wenyewe,na iliyokuweka hapo ulipo pia ulioapa kuilinda na kuifuata kama ilivyo pasipo kuondoa hata nucta ya yaliyomo.
Mjomba kwa kuwa cheo chako ni kukuu tena kikuu sana naandika haya nikiwa na woga wa kumfuata ndugu yangu 8 ambaye mpaka sasa hajulikani alipo harufu wala tetesi zake ya kuwa amepita hapa au kule zimepotea gafla.Samahani mjomba nimeghafrika ila najua hayo yote nayoyaoona yakifanyika kwa nguvu zote,akili zote na ujuzi uliotukuka katika miili ya wapenda haki hayakuwa sera ya chama chetu mjomba.
Mjomba nasema haya kwa uchungu kwani sipendi kuona nchi yangu ikiwa imegubikwa na wingu la uoga,hofu na uonevu usiokuwa na msingi wala faida yoyote katika taifa letu.
[HASHTAG]#KAMWE[/HASHTAG] SITAOGOPA#