Naja naja
JF-Expert Member
- Sep 13, 2016
- 747
- 1,452
Sera ya elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne imechangia kwa kiasi kikubwa kwa wanavyuo kukosa mkopo
Pesa ambazo zingetumika kugawa mikopo ndo hizo hizo zimegharamia elimu bure ,we jaribu kufikiria mwenyewe Magu ameingia madarakani mwezi November halafu January elimu bure ikaanza rasmi jiulize hizo pesa zimepatikana wapi kama sio hizi hizi za wanavyuo vikuu
Yani ni bora turudi kulekule tulipotoka ambapo elimu ya msingi na sekondari tulikuwa tunalipia lakini wakati huohuo wanafunzi wa vyuo wanapata mkopo kuliko kuwanyima mkopo wanafunzi wa chuo na kuifanya elimu ya msingi na sekondari bure
Gharama za kulipia elimu ya msingi na sekondari ni ndogo kulinganisha na gharama ya chuo
Kutokana na watu kutomudu gharama za chuo wengi wao wanakimbilia kozi za bei rahisi na zenye vipaumbele ya mikopo
Kwa hiyo basi wengi wao wanalazimisha kusoma vitu wasivyoviweza mwisho wa siku wanakuwa watu wa kukariri sana kuliko kuelewa madhara yake inapelekea kuzalisha watalamu feki
Ombi/ushauri:naiomba serikali mara moja waliangalie suala hili kwa jicho la tatu nikimaanisha wafute sera yao ya elimu bure ili ile pesa ambayo ingetumika kugharamia elimu bure wapewe wanafunzi wa vyuo vikuu
Nasema haya kwa kuwa wanafunzi wa vyuo wengi wao hawapati muda wa kukisoma kitu kwa undani kwa kuwa wengi wao wanajigawa nikimaanisha wanasoma wakati huo huo wanatafuta pesa kwa hiyo kwa kuwasaidia kupata pesa inayotosheleza ,itasaidia kuokoa ule muda ambao wangetumia kutafuta pesa kutulia darasani na kusoma
Wengi chuo wanadisco kwa sababu ya mahudhurio afifu yanayosababishwa na utafutaji wa pesa ambao kwa kiasi kikubwa unachangia mtu kukwepa vipindi ili aelekeze nguvu zake kwenye kutafuta pesa