Sera ya Chadema ya "Utawala wa Majimbo"

Mtoa mada, naweza ipata wapi hiyo sera ili niisome kwanza niielewe ndio nije nitoe mchango.

Hata kama ni nzuri kiasi gani lazima wananchi tuelimishwe, isije kuwa another sera maslah.

Mikoa mimngine haina hata ulanga sijui itakuwaje.

Kila mkoa nchi hii una rasilimali za kutosha kwa namna yake.
Hebu taja mkoa m1 tu ambao ni maskini wa rasilimali?
 

JokaKuu, sio lazima tufuate Model ya USA, kuna nchi nyingi zinafuata mfumo huo na hakuna mwingiliano wa ki-maslahi kati ya Taifa na Majimbo. Mfano mzuri ni Ujerumani-maswala unayozungumzia ya kodi nk ni mambo ya ki-Taifa na yanamhusu kila raia bila kujali anaishi Jimbo Gani!!
Ndo maana naomba sana jamani viongozi wa Chadema mtuwekee bayana hili jambo hadharani ili tuweze kutembea pamoja!!!!!!
 
vyovyote vile itakavyokuwa, tunachotaka hata kama hakutakuwa na majimbo, basi wakuu wa mkoa wachaguliwe kwa kura, kama vile walivyo ma seneta au magavana wa majimbo. ambacho hatutaki hapa, ni uteuzi wa rais wa chama tawala kwa wakuu wa mkoa na wilaya. wakichaguliwa at least itakuwa bora kuliko. hiki cha mkuu wa wilaya ndo naomba Mungu kiondoke kabisa kwasababu hakina umuhimu zaidi ya kutumika chama badala ya nchi. mkuu wa mkoa akichaguliwa kwa kura, na kupewa mamlaka ya kusimamia vizuri mkoa wake, basi ata kuwa kwenye nafasi nzuri kuuendelea ule mkoa na atakuwa accountable sana kwa mkoa wake. tofauti na hapo anakuwa acountable kwa rais tu, akifanya mchezo anapigwa chini na rais kama hatakuwa ameendeleza interest za chama na rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…