Sera ya Chadema ya "Utawala wa Majimbo" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera ya Chadema ya "Utawala wa Majimbo"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kindafu, Apr 25, 2012.

 1. k

  kindafu JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Chadema ina uhakika mkubwa wa kushika Dola katika uchaguzi ujao kama utakuwa kweli huru na wa haki. Naunga mkono Sera yao ya „Utawala wa Majimbo“, na ningependekeza kwamba waiweke hadharani tangu mapema ili iweze kufanyiwa „Pannel beating“ kwenye „Vijiwe“, „Media“, „Mitandao“ na „Forums“ mbali mbali. Wakati mwafaka ukifika wataunda tu kamati maalum kuchambua maoni yatakayokuwa yametolewa na wadau na kutoa kitu kilicho bora - kinachokubalika na kinachowezekana! Ningetamani kwa sasa waainishe bayana yafuatayo:
  i. Ni jinsi gani wataigawa Tanzania ki-Majimbo i.e. Majimbo mangapi na mipaka yake ki-Jiografia.
  ii. Mfumo wa Utawala utakavyokuwa – ngazi ya Taifa na ngazi ya Jimbo.
  iii. Mfumo wa uchaguzi utakaotumika kuwapata viongozi ya Kitaifa na wa Majimbo.
  iv. Mipaka ya Utawala/Maamuzi – Kitaifa na katika Majimbo.
  v. Mfumo wa Utawala wa Fedha – Kitaifa na katika Majimbo.
  vi. Nk, nk, nk,….. – waweza kuongeza vipengele kadiri ya upeo wako!

  My Take:
  i. Hili litapunguza muda na gharama za „Uelimishaji Umma“ wakati utakapofika.
  ii. Itawezesha wanachama wengi zaidi kuifahamu vema sera ya Chama chao na kuweza kuinadi katika ngazi na nafasi zao.
  iii. Itawezesha wanachama wanaotamani kuwania nafasi mbali mbali za Uongozi kuanza kujipanga mapema kwa nafasi za Kitaifa na katika Majimbo.
  iv. Nk, nk, nk………Waweza kuongeza
   
Loading...