sheiza
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 7,565
- 11,480
Nakumbuka ilikuwa 25 septemba 2018 tuliposhuhudia hekaheka za uzinduzi wa zilizoitwa sera mbadala za Chadema.
Zoezi hili liliendana na sherehe zilizofana katika hotel ya Bahari Beach jijini Dar es salaam ikiwemo matumizi makubwa ya fedha yaliyoambatana na uchapishaji wa vitabu pamoja na ununuzi wa magari kadhaa aina ya ford ranger ili yatumike katika zoezi hilo.
Leo haijamaliza hata miaka miwili toka uzinduzi huo mkubwa ufanyike. Hatuoni sera mbadala wala machapisho yoyote kama ilivyoahidiwa.
Mbaya zaidi hata wale viongozi na wabunge ambao tuliona siku za mwanzo wako bize akiwemo heche na kilewo kupost mitandaoni kwa sasa hatuoni tena wakizinadi kwenye kurasa zao.
Kibaya zaidi hakuna hata mrejesho wa hiyo program yenyewe.
Sasa tujiulize je; sera mbadala
1. zilikosa mvuto kwa wananchi?
2. Hazikuwa na kitu kipya?
3. Zilikosa uungwaji mkono kwa viongozi na wabunge wa chadema?
4. Au ilikuwa utaratibu wa kawaida wa mwenyekiti kuhalalisha matumizi mabaya ya ruzuku? Maana hata machapisho yake haikutangazwa tender yeyote.
Labda watajitetea walizuiliwa kufanya mikutano. Lakini zuio la mikutano limetoka 2015 na sera zimezinduliwa 2018 kwa gharama kubwa. Pia hata mitandaoni waliacha kupost au nako walizuiliwa pia?
Hili nalo limepita wana ufipa wameshasahau.
Safari bado ndefu sanaaa.
Nawakilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app