Separation of Powers: Waziri Mkuu Majaliwa atofautiana na Rais Magufuli. Nani mkweli, Nani muongo?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,761
121,810
Wanabodi,

Leo katika kipindi Cha Maswali ya Papo Kwa Papo na Waziri Mkuu, kumeibuka swali kuhusu "the doctrine of the Separation of Powers"

Waziri Mkuu amesema Tanzania ni nchi inayofuata Katiba na sheria kupitia mihimili mitatu ya dola ambayo iko sawa iko huru na haiingiliani.

Lakini kwenye Mkutano wa Rais na waandishi wa habari alisema japo mihimili hii mitatu inaelezwa kuwa sawa, lakini kuna muhimili mmoja umejichimbia chini zaidi!.

Haiwezekani wote wawili wakawa sawa, Haiwezekani mihimili hii ikawa sawa halafu hapo hapo ikawa si sawa kama kuna muhimili uliojichimbia chini zaidi.

Hapo kuna mmoja ni mkweli na kuna mmoja ni muongo.

Sasa Kati ya Rais na Waziri Mkuu, nani mkweli na nani ni muongo?

Angalizo: Katika kuchangia uzi huu naomba kutoa angalizo muhimu kuhusu ukosoaji

Soma pia: Mwito Kwa Wana JamiiForums Kuhusu Ukosoaji wa Rais Magufuli

Paskali
Rejea
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...
Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of ...
 
Mmmh hili swali mkuu halijakaa vizuri, swali limekaa kimtego, mimi ninachoweza kusema wote tumewasikia wakitoa kauli hizo kama ulivyosema, na mihimili mingine haijasema kitu, ila katiba ipo wazi kabisa kuwa mihimili yote ni sawa, kwa kuwa awamu hii haifuati katiba na sheria za nchi basi mh. Raisi yupo sahihi
 
Theoretically, Waziri Mkuu yupo sawa kabisa. Hata sisi tulifundishwa hivyo kwenye Somo la Uraia.

Practically, Magufuli yupo sawa kabisa.

Huwezi kusema wapo sawa. Wakati Jaji Mkuu, Majaji wote wanateuliwa na Raisi. Huwezi kusema wapo sawa, Kula kwako kunamtegemea mwingine. Huwezi kusema wapo sawa wakati Raisi anateua miongoni mwenu.

Raisi ni Mkuu wa Serikali, na Mkuu wa Nchi. Amiri Jeshi Mkuu. Raisi ni sehemu ya Bunge. Kwa maoni yangu pia, Raisi ni sehemu ya Mahakama. Ila Spika wala Jaji Mkuu si sehemu ya Executive.

Hata kwenye kukaimu Uraisi. Ikitokea Raisi hayupo, anakaimu Makamu wa Raisi, asipokuwepo, anakaimu M/Raisi, asipokuwepo anakaimu PM...wakiwa hawapo hao...labda...hao wengine.

Mizizi ya Executive ipo chini sana.
 
Hapa ijulikane kabisa Waziri mkuu ni muoga tu hataki kusema boss wake kakosea ni mambo mengi tu huyu boss anakosea
/-kumlinda Lipumba na kumpa ruzuku
/-kuzuia mikutano ya kisiasa
/-kuzuia maandamano
/-kutisha vyombo vya habari
/-kuzuia bunge kuwa mubashara
/-kuhonga mahakama pesa ili wafunge wapinzani
/-kutumia polisi vibaya bila kujali haki za watu
/-kunyanganya bunge meno na kuwapangia kamati .
/-kujaza raia uoga
/-vyeo kutolewa kwa makada wa chama
/kutumia jeshi letu vibaya kila chaguzi Zanzibar .
 
Separation of powers is a classical poli sci myth. It was, it's and will never be practical in any society.
Legally (legislature- and judicial-wise) it's supposed to be so, but not when executing policies (The executive).
Kwa hiyo wote wapo sawa.
 
Theoretically, Waziri Mkuu yupo sawa kabisa. Hata sisi tulifundishwa hivyo kwenye Somo la Uraia.

Practically, Magufuli yupo sawa kabisa.

Huwezi kusema wapo sawa. Wakati Jaji Mkuu, Majaji wote wanateuliwa na Raisi. Huwezi kusema wapo sawa, Kula kwako kunamtegemea mwingine. Huwezi kusema wapo sawa wakati Raisi anateua miongoni mwenu.

Mizizi ya Executive ipo chini sana.

Mkuu Foundation kimsingi mzizi wa mapato ya serikali ni watu (The People). Katiba pia inatajwa kuwa na nguvu toka kwa watu, kwa hiyo hakuna cha anayetoa pesa au anayetegemea kupata pesa; suala ni mgawanyo wa majukumu, kiuhalisia huwezi kuwa na mihimili mitatu halafu yote ikakusanya mapato, itageuka chaos! Mhimili wa Executive moja ya majukumu yake ni kukusanya pesa zitakazotumiwa na mihimili (Judicially & Legislation) yote katika kuwahudumia watu- ambao ni chimbuko la mamlaka yao.

Ndo maana katiba zote zilizoandikwa kidemokrasia zinataja mamlaka yake kutoka kwa watu. Kwa hiyo ukiniuliza mimi nitasema, PM yuko sawa, ila figisu toka vyama vya siasa za kujikusanyia madaraka hasa toka tawala za kiafrika ndizo zinazotuvika miwani zenye mawaa hatuoni tofauti za mihimili hii.
 
Hapa ijulikane kabisa Waziri mkuu ni muoga tu hataki kusema boss wake kakosea ni mambo mengi tu huyu boss anakosea
/-kumlinda Lipumba na kumpa ruzuku
/-kuzuia mikutano ya kisiasa
/-kuzuia maandamano
/-kutisha vyombo vya habari
/-kuzuia bunge kuwa mubashara
/-kuhonga mahakama pesa ili wafunge wapinzani
/-kutumia polisi vibaya bila kujali haki za watu
/-kunyanganya bunge meno na kuwapangia kamati .
/-kujaza raia uoga
/-vyeo kutolewa kwa makada wa chama
/kutumia jeshi letu vibaya kila chaguzi Zanzibar .
48 Laws of Power.
# Never outshine your master.

PM yuko sahihi
 
Kwa aina ya mfumo uliopo ni yule tu asiyetumia fikra sahihi ataona kuwa mihimili hii mitatu kuwa sawa.
Executive inateua Jaji Mkuu kuongoza mhimili wa Mahakama.
Executive ina pandisha vyeo watu wa mhimili wa mahakama
EXECUTIVE haibanwi kutekeleza maazimio ya mhimili wa Bunge (rejea Escrow na Operesheni Tokomeza)

Bado umeamua kuamini kuwa mihimili hii ipo sawa?
 
Watu wengine wanavitu vya ajab ajab tu
Hiv wewe hujui kuwa rais yuko juu ya mihimili yote mitatu
Eti iko huru!!!
Hiyo hiyo katiba inasemaje
Nani anayeajiri wanasheria
Nani anayeajiri wabunge
Ukiguatilia ni rais tu.
Mpaka vyama vya siasa
Viko chini ya rais
Vinamtegemea akusanye fedha awalipe kwa hata bajeti yao ni yeye anayelipa
 
Theoretically, Waziri Mkuu yupo sawa kabisa. Hata sisi tulifundishwa hivyo kwenye Somo la Uraia.

Practically, Magufuli yupo sawa kabisa.

Huwezi kusema wapo sawa. Wakati Jaji Mkuu, Majaji wote wanateuliwa na Raisi. Huwezi kusema wapo sawa, Kula kwako kunamtegemea mwingine. Huwezi kusema wapo sawa wakati Raisi anateua miongoni mwenu.

Raisi ni Mkuu wa Serikali, na Mkuu wa Nchi. Amiri Jeshi Mkuu. Raisi ni sehemu ya Bunge. Kwa maoni yangu pia, Raisi ni sehemu ya Mahakama. Ila Spika wala Jaji Mkuu si sehemu ya Executive.

Hata kwenye kukaimu Uraisi. Ikitokea Raisi hayupo, anakaimu Makamu wa Raisi, asipokuwepo, anakaimu M/Raisi, asipokuwepo anakaimu PM...wakiwa hawapo hao...labda...hao wengine.

Mizizi ya Executive ipo chini sana.
Rudia kusoma paragraph yako ya mwisho. Unaowataja ni sehemu ya executive. Unataka kujenga hoja gani.
 
Theoretically, Waziri Mkuu yupo sawa kabisa. Hata sisi tulifundishwa hivyo kwenye Somo la Uraia.

Practically, Magufuli yupo sawa kabisa.

Huwezi kusema wapo sawa. Wakati Jaji Mkuu, Majaji wote wanateuliwa na Raisi. Huwezi kusema wapo sawa, Kula kwako kunamtegemea mwingine. Huwezi kusema wapo sawa wakati Raisi anateua miongoni mwenu.

Raisi ni Mkuu wa Serikali, na Mkuu wa Nchi. Amiri Jeshi Mkuu. Raisi ni sehemu ya Bunge. Kwa maoni yangu pia, Raisi ni sehemu ya Mahakama. Ila Spika wala Jaji Mkuu si sehemu ya Executive.

Hata kwenye kukaimu Uraisi. Ikitokea Raisi hayupo, anakaimu Makamu wa Raisi, asipokuwepo, anakaimu M/Raisi, asipokuwepo anakaimu PM...wakiwa hawapo hao...labda...hao wengine.

Mizizi ya Executive ipo chini sana.
Unajitahidi kutetea ujinga j apo huenda wewe sio mjinga
 
Watu wengine wanavitu vya ajab ajab tu
Hiv wewe hujui kuwa rais yuko juu ya mihimili yote mitatu
Eti iko huru!!!
Hiyo hiyo katiba inasemaje
Nani anayeajiri wanasheria
Nani anayeajiri wabunge
Ukiguatilia ni rais tu.
Mpaka vyama vya siasa
Viko chini ya rais
Vinamtegemea akusanye fedha awalipe kwa hata bajeti yao ni yeye anayelipa
Nakuomba usome katiba. Pamoja na rais kuwateua:
- hana uwezo kumfukuza jaji wala hakimu.
- hana uwezo wa kumfukuza mbunge.
Rais pia hawezi kuvifuta vyama vya siasa, akifanya hivyo atakuwa dictator.
Nani aliyekudanya kuwa rais anaajiri wabunge.
Ni busara kukaa kimya kuliko kujidhalilisha kwa kiwango hiki.
 
Back
Top Bottom